Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inatarajia kwenda nchini Azerbaijan Kwaajili ya mashindano madogo ya FIFA Series yatakayo husisha timu nne kutoka mabara tofauti.
Lyamba Lya Mfipa
Na Joachim Nyambo
Tuesday, February 20, 2024
Taifa Stars kuanza na Bulgaria "FIFA Series"
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inatarajia kwenda nchini Azerbaijan Kwaajili ya mashindano madogo ya FIFA Series yatakayo husisha timu nne kutoka mabara tofauti.
Saturday, January 13, 2024
SBL YAZIDI KUGAWA MAOKOTO
Meneja mauzo wa Kampuni ya SBL mkoani Mbeya, Karolina Mwamaso( kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi 500,000 kwa mshindi wa promosheni ya Maokoto inayoemndeshwa hiyo, Patrick Mrema wa jijini Mbeya katika hafla iliyofanyika New City Pub jijini Mbeya(Na Mpigapicha Wetu)
Thursday, January 11, 2024
DK. TULIA ASHIRIKI BONANZA LA PAMOJA ZANZIBAR
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki Bonanza la pamoja lililohusisha michezo mbalimbali kati ya Baraza la Wawakilishi Sport club, Bunge Sport club na NMB Sport Club lililofanyika Visiwani Zanzibar leo tarehe 11 Januari, 2024
Thursday, December 21, 2023
FAINALI LIGI YA MKOA STELLA FIYAO CUP SONGWE FURAHA NYINGINE YA X-MASS
FINAL LIGI YA MKOA STELLA FIYAO CUP SONGWE. kupigwa tarehe 24/12/2023 katika viwanja vya Tunduma day Sekondari iliyopo tunduma Kati ya MKWAJUNI FC kutoka Wilaya ya SONGWE na LAMBYA FC kutoka wilaya ya ILEJE kuanzia majira ya saa kumi jioni shamlashamla za fainal zitaanza mapema sana mwambie rafiki ni bonge Moja la fainal.LIGI YA MKOA STELLA FIYAO CUP 2023/2024 IMEDHAMINIWA NA MBUNGE VITI MAALUMU MKOA SONGWE MH.STELLA FIYAO
Thursday, October 26, 2023
KenGold wataka kujiimarisha zaidi kileleni Championship
NA MWANDISHI WETU
CHUNYA YAENDELEA KUWABURUZA WAPINZANI SHIMISEMITA DODOMA
Timu ya wanawake ya kuvuta Kamba ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ikiongozwa na Kiongozi mwanamama mwenye misuli Bi Devotha Mwasaga ikiendeleza ubabe wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Jijini Dodoma
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bingwa mtetezi wa mchezo wa kuvuta Kamba SHIMISEMITA msimu uliopita msimu huu bado inaendelea kuwabuluza wapinzani wake katika michezo ya watumishi inayoendela jijini Dodoma baada ya Timu ya wanawake kuvuta Kamba kuingia nusu fainali wakati Timu ya wanaume kuvuta kamba iko Robo Fainali
Chunya DC Vs Moshi DC (ME) mshindi CHUNYA DC
Chunya DC Vs Tunduma TC (KE) mshindi CHUNYA DC
Kwa matokeo hayo Chunya Dc wanaume wametinga hatua ya robo fainali (Mtoano) ambapo watakutana uso kwa uso timu ya watumishi kutoka Arusha jiji huku timu ya Chunya DC wanawake wao wametinga hatua ya nusu fainali ambapo watavaa na timu Kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam (DAR CC) ambayo ni kesho asubuhi.
Kuelekea Mchezo wa Nusu Fainali kepten wa timu ya wanawakeChunya DC Kuvuta kamba Bi Devotha Mwasaga amesema kilichobaki kutoka kwa wanachunya ni dua, Sara na Maombi ili kufanikisha azma ya kuleta ushindi Chunya na hatimaye kuiheshimisha wilaya ya Chunya kwani upande wa Maandalizi hakuna changamoto yoyote timu iko salama.
“Tunachokihitaji kutoka kwa wananchunya ni maombi kila mmoja kwa Imani yake ili timu iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa kwani upande wa maandalizi kila kitu kiko vizuri, wachezaji wana ari na morali wa kuhakikisha ubingwa unakuja Chunya hivyo tuiheshimishe Chunya yetu”.
Kwa upande wa timu wanaume kuvuta kamba kepteni wa Timu hiyo Ridhiwani Mshigati amesema bado timu iko Imara na iki tayari kwa michezo yote iliyo mbele yetu huku lengo ni lile lile kuchukua tena ubingwa katika mashindano hayo hasa kwa upande wa Mchezo wa Kuvuta Kamba.
“Kwenye mchezo wa kuvuta kamba tumeendelea na kutetea ubingwa wetu na ndo maana tumeshinda 2 bila kwa maana ya kwamba tuliocheza nao tumefunga awamu zote mbili, na kamba ina mbinu za kupata ushindi, sisi tumehatika kupata mtaalamu anatuongoza vizuri na kwasasa tuko kambini tunaendelea kupeana mbinu na kutunza nidhamu. kurudi mikono mitupu kwa Mwajiri ni aibu kubwa ambayo sisi hatutaki itokee kwetu kulingana na huduma tulizopewa na mwajili wetu.
Na tunashukuru Halmashauri jirani za Rungwe na Tunduma wanatusapo, ingawa Tunduma Tc walifungwa na timu ya wanawake kuvuta kamba tuliwaomba radhi na kuwambia kwa hili hatuna ujirani tukawatoa, Tunaomba watu wa Chunya waendelee kutuombea ili kutetee ubingwa wetu na lengo ni siku ya kufungwa kwa Mashindano haya Halmashauri yetu ya Chunya Itajwe na Mgeni rasmi na Bendera yetu iweze kupepea mbela ya Halmashauri zaiidi ya Mia moja zilizoshiriki Mashindano hayo” amesema Mshigati.
Utofauti wa hatua yaani Timu ya wanaume kuwa hatua ya Robo Fainali (Mtoano) huku timu ya wanawake kuwa hatua ya Nusu Fainali umetokana na Idadi ya timu zilizoshiriki mchezo huo kwani Timu za wanawake zilikuwa chache kulinganisha na timu za wanaume hivyo kupelekea kupelekea baadhi ya hatua za mashindano kuwa na mzunguko mfupi kulingana na timu za wanaume.
Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndiye Bingwa Mtetezi wa Mchezo wa Kuvuta Kamba Taifa kwa msimu wa mwaka 2022 na sasa timu zote ziko hatua nzuri kutetea ubingwa mwaka huu 2023, Maombi, bahati pamoja na kujituma vitaendelea kuhitajika ili timu zetu ziendelee kufanya vizuri
Saturday, August 12, 2023
Friday, August 11, 2023
USHIRIKI WA MASHUJAA FC LIGI KUU TANZANIA KUONGEZA CHACHU YA MAENDELEO KIGOMA
Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema ushiriki wa Timu ya Mashujaa FC katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara utaongeza chachu ya Maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa wa Kigoma.
Andengenye ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Uwanja wa CCM Lake Tanganyika Stadium utakaotumiwa na Timu ya Mashujaa kwa ajili ya michezo ya nyumbani katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara Msimu wa 2023/2024.
Ameeleza kuwa, kutokana na ushiriki wa timu hiyo, Mkoa utapokea wageni kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kushuhudia michezo ya ligi kuu ambapo kuanzia wafanyabiashara wakubwa hadi wajasiriamali wadogo watapata fursa ya kunufaika kiuchumi kutokana na kuwahudumia wageni hao.
"Pamoja na kupata burudani, michezo inatoa fursa mbalimbali za kujiimarisha kiuchumi kupitia biashara, nitoe wito kwa wafanyabiashara na wakazi kwa ujumla tuchangamkie fursa za kiuchumi zitakazojitokeza ambazo zitatokana na wageni watakaokuja kwa ajili ya kushuhudia michezo mbalimbali ya ligi kuu" amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Upande wake Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mha. Francisco Magoti amesema ukarabati huo unahusu maeneo ya majukwaa, vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji, ukumbi wa mikutano, vyoo pamoja na eneo la kuchezea mpira.
" Mafundi wapo kazini na tutahakikisha maboresho muhimu yanakamilika kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara ili kuruhusu michezo ifanyike kama ilivyopangwa huku uwanja ukiwa katika ubora unaotakiwa" amefafanua Magoti.
Upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Kigoma, Edward Manase amesema wameridhishwa na maendeleo ya kazi mbalimbali zinazofanyika za marekebisho ya uwanja huo huku akiwahimiza watendaji kutanguliza uzalendo na kuzingatia ubora.
Thursday, June 15, 2023
Wednesday, June 14, 2023
SINGIDA BIG STARS YAPIGWA MNADA
MICHUANO TULIA TRUST BODABODA CUP 2023 YAZINDULIWA RASMI.
Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa akisalimiana na wachezaji wa timu za Madereva Bodaboda za Uyole na Stendi kuu kwenye uzinduzi wa Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.
Na Joachim Nyambo,
Mbeya.
MEYA wa jiji la Mbeya
Dormohamed Issa amezindua rasmi michuano ya Tulia Trust Bodaboda Cup 2023
yatakayoshirikisha timu nane kutoka kanda za madereva bodaboda zilizogawanywa
kwenye makundi mawili ya A na B.
Michuano hiyo imerejea
tena baada ya kusitishwa kwa misimu miwili mfululizo ambapo kwa mara ya kwanza
yalifanyika 2019 lakini kwa miaka iliyofuata haikufanyika kutokana na
changamoto mbalimbali ikiwemo mlipuko wa Covid-19
Kwa upande wa kundi A timu
zinazoshiriki michuano hiyo ni za madereva bodaboda kutoka kanda za Iyunga,
Stendi Kuu, Soweto na Kabwe wakati kundi B zipo timu za kanda za Mafiati, Sae,
Uyole na Kadege.
Akizindua michuano hiyo
katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge, Meya wa jiji la Mbeya Meya Issa ameipongeza
Taasisi ya Tulia Trust inayoyaandaa akisema yana mchango mkubwa katika kuibua
na kukuza vipaji vya vijana.
Amewasihi madereva
bodaboda kutumia michuano hiyo situ kwa kuibua vipaji vyao bali pia kuimarisha
afya zao hivyo kuwataka kuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote yatakapokuwa
yanaendelea.
“Mpira unaanza kucheza
chini lakini haujui huko mbele utafika wapi…naamini kabisa kuna wachezaji
miongoni mwenu mkionyesha nidhamu mkazingatia yale mnayofundishwa na walimu
kuyafuata ipo siku mtafika mbali.”
“Mpira ni nidhamu..na
ukitaka kufanikisha katika jambo lolote weka nidhamu mbele..ukiamua kuwa padre
weka nidhamu mbele, ukitaka kuwa shekh weka nidhamu mbele na hata ukitaka kuwa
kiongozi wajali watu wako.” Amesisitiza Issa.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Kamati ya mashindano ya Chama cha soka Mbeya mjini(Mufa), Ramadhan Nyambala amesema
kutokana na ari ya mpira wa miguu katika mkoa wa Mbeya ni muhimu wadau wengi
kuzidi kujitokeza kuandaa mashindano mbalimbali.
Amesema kuandaliwa kwa
mashindano kama ya Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 ni sehemu ya mikakati muhimu
na inayotarajiwa kwenye kuibua na kukuza vipaji vya vijana.
Afisa Habari na
Mawasiliano wa Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema baada ya michuano hiyo
kufanyika kwa mara ya kwanza 2019 iaka miwili mfululizo ilisimama kutokana na
changamoto mbalimbali zilizoibuka ikiwemo cha mlipuko wa ugojwa wa corona.
Mwakanolo amesema michuano hiyo itakayokuwa ikifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge na Magereza Mbeya yanatarajia kufikia tamati mwezi ujao huku akisema zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu zitatangazwa hivi karibuni.
Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa akisalimiana na waamuzi wa mchezo kati ya timu za Madereva Bodaboda za Uyole na Stendi kuu kwenye uzinduzi wa Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.