Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, August 21, 2014

UKATILI HUU MPAKA LINI?



Kama kweli laana ipo,naomba eeh Mwenyezi Mungu walaani watu wanaofanya ukatili huu.Huyu ni mwanamke Suzana Mgasa Mungu (34),aliye na ulemavu wa ngozi(Albino).

Mwanamke huyu alifanyiwa ukatili wa kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake na watu wasiojulikana na hatimaye watu hao kuondoka na sehemu ya mkono wake baada ya kumuua mumewe wakati akijaribu kupambana kumwokoa mkewe.

Tukio hili lilitokea Agosti 15 mwaka huu majira ya saa tano usiku huko Igunga Tabora.Vitendo hivi vya kikatili vimekuwa vikifanyika nchini na kulipa sifa mbaya taifa la watanzania wajiitao kisiwa cha amani.

Ewe mwenyezi Mungu mjaalie afya njema Suzana,na nakuomba andika majina ya waliofanya ukatili huu katika kitabu chenye orodha ya watu wasiopaswa kusamehewa kamwe.

PICHA KWA HISANI YA TANZANIA ALBINISM SOCIETY

No comments:

Post a Comment