Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, September 30, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 30.09.2014.


  KATIKA TUKIO LA KWANZA:

KIKONGWE MWENYE UMRI WA MIAKA 90 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAPONDO NGAO MKAZI WA KIJIJI CHA UKWILE WILAYANI MBOZI ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI UKWILE, KATA YA ISANDULA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATU HAO WALIMVIZIA MAREHEMU AKIWA AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE NA KISHA KUMVAMIA NA KUANZA KUMKATAKATA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.

CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KUFAHAMIKA. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA MAWILI YA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI. MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI PEKE YAKE MAENEO YA MASHAMBANI UMBALI WA ZAIDI YA KILOMITA TANO [05] KUTOKA MAKAZI YA WATU.

HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI, MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO ILI AZITOE MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA KATIKA SHULE YA MSINGI SANZYA WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VALIUD SIAME@KIMUNDE (13) MKAZI WA KIJIJI CHA KAONGA ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAONGA, KATA YA CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WAKATI TUKIO HILO LIKITOKEA MAREHEMU ALIKUWA NA WANAFUNZI WENZAKE WAKICHIMBA NA KUBEBA MCHANGA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA KULALA WAALIMU SHULENI HAPO.

MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUTOA UANGALIZI WAKUTOSHA IKIWA NI PAMOJA NA KUWASIMAMIA WATOTO KATIKA SHUGHULI WANAZOWATUMA KUFANYA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment