Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, September 23, 2014



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 23.09.2014.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

WATU WANNE WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.200 AKQ AINA YA ISUZU LORI IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUACHA NJIA NA KISHA KUIGONGA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.614 BUK AINA YA T-BETTER ILIYOKUWA PEMBENI YA BARABARA NA KISHA KUPINDUKA.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 22.09.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO MLIMA NYIMBILI, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA, BARABARA YA KAMSAMBA/MLOWO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI 1. SELA MKISI (30) MKAZI WA NTUNGWA 2. ENEA MGALA (42) MKAZI WA NKANGA 3. LUSIANO MTENDA (50) MKAZI WA MKOMBA NA 4. ELITA MASHAKA (02) MKAZI WA NTUNGWA.

AIDHA WATU KADHAA WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI VWAWA KWA MATIBABU. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOPSPITALI YA KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KALONGOTI MWASIMBA (80) MKAZI WA KIKOTA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 22.09.2014 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO MAENEO YA KIKOTA, KATA YA MSASANI, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA TUKUYU/MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA [MADEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO, VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment