Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimu mafunzo yao ya siku tano
Mkufunzi Somo Ahmed Kimwaga ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya TAVA akifundisha washiriki namna ya kucheza mchezo wa wavu
WALIMU 26 kutoka shule za msingi na sekondari za
wilaya mbalimbali mkoani Mbeya wamehitimu mafunzo ya awali ya mchezo wa wavu
mkoani Mbeya yaliyoandaliwa na chama cha mchezo huo nchini(TAVA).
Mafunzo hayo yaliyoanza Septemba 15 mwaka huu
yamemalizika leo chini ya mkufunzi kutoka TAVA Somo Ahmed Kimwaga ambapo
lengo ni kuhamasisha mchezo huo mashuleni.
Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa Kimwaga
amesema sambamba na mafunzo hayo washiriki watapata fursa ya kuanzisha chama
cha wavu mkoa ili kiwezo kuwa sehemu ya hamasa ya mchezo huo.
Aliwataka washiriki kuhakikisha wanakwenda
kuyafanyia kazi yale waliyojifunza badala ya kujijengea sifa kwa kupata chetio
na kwenda kukitundika ukutani.
Hata hivyo Kimwaga alisema kukosekana kwa vyama vya
wavu katika ngazi za mikoa ni changamoto inayokwamisha utekelezaji wa Tava
katika kuhamasisha mchezo huo.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mwalimu
Davis Mwakalinga alisema iwapo mchezo wa wavu utapata wadau wa kuuwezesha ni
mchezo mzuri na wenye heshima yake katika jamii.
Amesema ni mchezo unaoweza kuiwezesha nchi kujipatia
umaarufu mkubwa kimichezo iwapo mikakati ya dhati itawekwa kuuwezesha.
Mshiriki mwingine Mwalimu Yasinta Mafuru amesema ushiriki
mdogo wa wanawake katika mafunzo hayo ambao wako wawili pekee kati ya washiriki
26 inatokana na hamasa ndogo katika jamii juu ya ushiriki wa mwanamke katika
michezo.
No comments:
Post a Comment