Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, November 20, 2014

ASKARI ALIYEMUUA MWANAFUNZI HUYU AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA


 Huu ni mwili wa Marehemu kijana Daniel Mwakyusa mara baada ya kufanyiwa uchunguzi baada ya kuuawa.Daniel alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha TEKU
 Haya ni baadhi ya majeraha aliyojeruhiwa askari alipokutwa Univesal Pub siku ya Valentine akiwa na mwanamke aliyesadikiwa kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na askari Maduhu

 Mwili wa mwanafunzi huyo kabla ya kuzikwa mara baada ya kuagwa na ndugu,jamaa na marafiki.Jeshi la polisi liligharamia shughuli za maziko ya mwanafunzi huyo na hapo ndipo shitaka likaanza kuunguruma mahakamani.
                             
                        HABARI KAMILI
MAHAKAMA Kuu kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa askari wa jeshi la polisi F 5842 DC Maduhu aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) Daniel Mwakyusa.

Aidha mahakama hiyo pia imewaaachia huru washitakiwa wengine wawili wa kesi hiyo F 7769 DC Shaban na WP 6545 DC Neema baada ya kuwakuta hawana hatia.

Hukumu hiyo ya kesi namba 16 ya mwaka 2013 imetolewa leo(Nov 19) na jaji Rose Temba baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.

Awali ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali Archiles Mulisa akisaidiwa na Catherine Paul kuwa washitakiwa walifanya mauaji ya kukusudia mnamo Februari 14 mwaka 2012 kinyume cha kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Kwa mujibu wa Wakili Mulisa washitakiwa hao kwa pamoja walihusika na mauaji ya Daniel Mwakyusa baada ya kumpiga marehemu huyo kwa kutumia silaha inayodhaniwa kuwa ni bunduki nje ya ukumbi wa starehe ujulikanao Univesal uliopo Uyole jijini Mbeya.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo,jaji Temba amesema mshitakiwa namba moja DC Maduhu anahusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na ushahidi wa kimazingira ikiwamo yeye kuwa mtu wa mwisho kuondoka na marehemu eneo la tukio na kumpeleka kwenye gari,risasi tatu kupungua kwenye bunduki yake na pia kuwa mtu wa mwisho kurejesha silaha kituoni.

No comments:

Post a Comment