MCHEZO wa ligi kuu ya
Tanzania bara kati ya Mbeya City ya jijini Mbeya na Simba Sc ya Dar es salaam
umemalizika kwa timu ya samba kukubali kipigo cha goli mbili 2-0.
Ilikuwa dakika ya 45
yaaani sekunde chache kabla ya mapumziko,Paul Nonga alipowanyanyua mashabiki wa
Mbeya City baada ya kufunga goli la kwanza akiunganisha pasi kutoka kwa Deus
Kaseke.
Goli hilo likadumu hadi
timu hizo zinakwenda mapumziko huku katika kipindi hicho cha kwanza timu zote
zikionesha uwezo sawa kwa kufanya mashambulizi kwa zamu lakini kama ilivyokuwa
kabla ya mchezo,kipindi hicho cha mapumziko pia wachezaji wa timu ya Simba
hawakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo na badala yake wakabakia katika
benchi lao wakisubiri kuanza kwa kipindi cha pili cha mchezo.
Kipindi cha pili
kikaanza kwa timu zote kuonesha kuonesha kuwa zilikitumia vyema kipindi cha
mapumziko japo katika kipindi hiki Simba wakaonekana kupwaya kwa Mbeya City
kiasi cha kuruhusu mashambulizi mengi langoni kwao huku safu ya kiungo
ikionekana kushindwa kustahimili kasi ya mchezo.
Dakika ya 69 ya
mchezo,Peter Mwalyanzi maarufu kama afisa mipango,akawanyenyua tena mashabiki
wa Mbeya City waliofurika ndani ya dimba la Sokoine baada ya kupachika goli
safi na la kiufundi kutokana na uwezo wake binafsi uliosababisha walinzi wa
Simba kubakia wakimsindikiza wakati akienda kutekeleza adhma aliyotumwa na timu
yake.
Katika kipindi hicho
cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo wenyeji Mbeya City waliwatoa
Peter Mapunda,Cosmas Fredy na Deus Kaseke na nafasi zao zikachukuliwa na Hamad
Kibopile,Peter Mwalyanzi na Seleman Hassan.
Kwa upande wao Simba
waliwatoa Abdi Banda na Elius Maguli na kuwaingiza uwanjani Awadh Juma na Issa
Abdalah.
Hadi kipenga cha mwisho
cha mwamuzi Zacharia Jackob kutoka mkoani Pwani Mbeya City 2,Simba SC maarufu
kama mnyama bila.
No comments:
Post a Comment