Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, July 3, 2015

Marekani yafadhiili mafunzo ya ufundi kwa vijana waishio mazingira magumu


Mratibu wa mpango wa mafunzo ya ufundi ya muda mfupi katika chuo cha VETA Mkoa wa Mbeya, Benedict Chuwa (kulia) akitoa maelezo juu ya ugawaji wa vifaa kwa vijana walishiriki mafunzo hayo kwa msaada wa shirika la vijana la Marekani kushoto ni Mkurugenzi wa Veta nyanda Justin Rutha amabaye alikuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo.

Mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini Justin Rutha akizungumza na viijana  washio katika mazingira magumu kutoka jiji la Mbeya kabla ya kuwakabidhi vifaa vya ufundi katika fani mbalimbali vilivyo tolewea na shirika la vijana kutoka Marekani.

 JUMLA ya vijana 69 wanaoishi katika mazingia magumu na hatarishi jijini Mbeya wamehitimu mafunzo ya muda mfupi ya ufundi stadi katika fani mbalimbali zinatolewa na chuo cha Ufundi Veta Mkoani Mbeya.


Akizungumza mbele ya mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Veta Nyanda za juu kusini Justin Rutha,mratibu wa wa mufunzo hayo,Benedict Chuwa alisema kuwa Mafunzo hayo yalifanyika kwa muda miezi mitano ambapo miezi mitatu ilikuwa kwa nadharia ni miezi miwili ilikuwa kwa vitendo na yalilenga kuwasaidia vijana waishio mazingira magumu.

Mafunzo hayo yanayo fadhiliwa na sahirika na vijana la Marekani (Internation Youth Foundation) ‘IYF’  kwa kulipia ada ya masomo kiasi cha shilingi 400,000/ kwa kila mwanafunzi sanjali na kuwapa  vifaa kila kijana kutokana na fani aliyo somea ili kwenda kuanza maisha ya kujitegemea.

Chuwa alisema kuwa mafunzo hayo yalianza kutolewa Oktoba 2 mwaka jana na kufikia mwisho April mosi mwaka huu walianza vijana zaidi ya 70 lakini ni vijana 69 ndiyo waliohitimu katika fani saba tofauti ambazo ni,Ushonaji,Ujenzi,Mapambo na Saloon,Fundi bomba,Upishi,Uchomeleaji wa Vyuma na fundi magari pamoja na Udereva na kwamba vifaa vilivyo nunuliwa vimegharimu jumla ya shilingi milioni tatu chini ya ufadhili huo.

Akizungumza juu ya zoezi  lilivyo endeshwa  jinsi ya kuwapata vijana hao Chuwa alisema Chuo cha Veta kiliwasiliana na Halmashuri ya jiji la Mbeya ili kuweza kuwabaini vijana wanoishi katika mazingira magumu kutoka baadhi ya kata jiji hapa na baada ya hapo mafunzo yalianza rasmi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Veta nyanda za juu kusini,inayojumisha mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi, Rutha alisema kuwa ni vema vijana hao wakatambua lengo la mafunzo ni kumfanya fundi awe mairi katika fani husika badala ya kuwa wababaishaji.

Rutha aliongeza mafunzo waliopata ni muhimu na yanahitaji  katika jamii na kwamba ni vema ujuzi waliopata ukawa chachu ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi na katika familia zao, kwani kufanya hivyo kutawasukuma wafadhili kuendeleo kutoa misaada kwa vijana wengine ambao  waliokosa fursa hiyo.

‘Kwanza niwapongeza kwa udhubu wenu kukubali na kujitokeza kushiriki mafunzo hayo lakini pia kwa uvumilivu wenu katika miezi yote mitano ya mafunzo ya vitendo na nadharia lakini ni vema mkatambua kuwa fani mlizosomea ni mhunimu na zinahitaji kila kukicha hivyo niwa sii mnapaswa kujituma ili kuchochea maendeloa ya familia zenu na taifa kwa ujumla’alisema Rutha.

‘Na mjua wazi mkifanya vizuri wafadhili wataendelea kuisadia jamii yetu lakini mkifanya vibaya mtakatisha tamaa,pia elimu mliopata hapa haitoshi bali iwe kichocheo cha kujifua zaidi katika masuala ya ufundi’alisema Rutha.

Akitoa ushuhuda mmoja wawa washiriki wa mafunzo hayo Irene Josphat ambaye amesomea katika fani ya Saloon na Mapambo alisema kuwa awali kabla hajashiriki mafunzo hayo alikuwa hana ujuzi lakini sasa amekuwa na utaalamu mkubwa katika masula ya nywele na upambaji.

No comments:

Post a Comment