Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, August 30, 2015

MAKADA WALIOPAMBA KAMPENI ZA DK.MAGUFULI MKOANI MBEYA HAWA HAPA

 Dk.Mary Mwanjelwa ni Mbunge viti maalumu mkoa wa Mbeya.Anaamini ushindi wa Dk.Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao utakuwa wa kishindo na utawawezesha watanzania kuanza maisha mapya na yenye mabadiliko makubwa kimaendeleo.Hapa akizungumza na maelfu ya wakazi wa jiji la Mbeya kwenye mkutano wa Dk.Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya Ruandanzovwe.

Charles Mwakipesile-Alishika nafasi ya tatu katika kura za maoni ndani ya CCM kwa nafasi ya ubunge Mbeya mjini.Anasema Dk.Magufuli ni chaguo la watanzania walio wanaCCM na vyama vingine vyote vya siasa.Anaamini ushindi wa Dk.Magufuli upo tena wa kutosha.Hapa pia ni katika mkutano wa Dk.Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya Ruandanzovwe.

 Amani Kajuna-Alishika nafasi ya pili kwenye kura za maoni ubunge Mbeya mjini.Anasema yuko tayari kuunga mkono mgombea wa nafasi hiyo Sambweee Shitambala,mgombea wa urais Dk.John Pombe Magufuli na wagombea wa udiwani wote kupitia CCM.Ni katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Ruandanzovwe.
Wasanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Chege na Temba wanasema kwa Dk.Magufuli wapinzani lazima wakae.Ni walipowaburudisha wakazi wa jijini Mbeya katika mkutano wa Dk.Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya Ruandanzovwe.

Filipo Mulugo a.k.a ahadi umepata-Ni mgombea ubunge jimbo la Songwe.Anasema kwa Magufuli hapa kazi tu.Hapa ni katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya sabasaba mjini Chunya.


Dk.Harison Mwakyembe -Mgombea ubunge jimbo la Kyela.Anasema wagombea urais kupitia CCM na Ukawa wote amefanya nao kazi hivyo anawafahamu vizuri sana.Anasrma Dk.Magufuli ni chaguo sahihi.Hapa ni katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mjini Kyela.

John Mwakipesile-Mkuu wa mkoa wa Mbeya mstaafu.Anasema kwa kipindi cha miaka 10 hajafurahi ila sasa anafurahi.Anasema anamfahamu vizuri Dk.Magufuli na anaamini ndilo chaguo sahihi la watanzania.Anasema waliomzushia kuhamia Chadema walikosa kazi ya kufanya.Hapa ni katika mkutano wa Dk.Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mjini Kyela.

 
 

No comments:

Post a Comment