Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, August 1, 2015

UCHAGUZI KURA ZA MAONI CCM ILEJE WAINGIA DOSARI

UCHAGUZI wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mpainduzi CCM mkoa wa Mbeya umefanyika kwa amani na utulivu japo kulikuwa na kasoro chache zilizojitokeza kwenye baadhi ya maeneo.

Wilayani Ileje lilikuwa eneo lililokumbwa na changamoto kubwa ambapo taarifa kutoka wilayani huko zinabainisha kura kuchelewa kuanza kupigwa hadi saa tisa alasiri wanachama walipoanza kupiga.

Taarifa hizo zinabainisha kuwa zoezi la upigaji kura lilichelewa kutokana na fomu za kupigia kura kukamatwa usiku wa kuamkia siku ya kura hivyo ililazimu uongozi wa chama kuchukua jukumu la kufuta fomu za awali na kuchapa fomu nyingine.

Hata hivyo jitihada za Lyamba Lya Mfipa kuwasiliana na katibu wa CCM wilayani hapo Hamida Mbogo zimezonga mwamba kwani katibu huyo kila alipopigiwa simu na mhariri wetu kujitambulisha kwake kuwa ni mwandishi alikata simu.

Taarifa kutoka vyanzo vya uhakika wilayani hapo zinaeleza kuwa hadi tunakwenda mitamboni baadhi ya vituo kikiwemo cha  Ikuga katika kata ya Mlale shughuli ya kupiga kura ilikuwa haijaanza bado.

No comments:

Post a Comment