MAANDALIZI ya Mashindano ya kuibua
vipaji katika soka Wilayani Mbarali mkoani Mbeya ya Kipye Cup 2016 yamezidi kushika kasi ambapo kesho(Mei 29)
timu 14 zinatarajiwa kupitishwa ili kushirili mashindano hayo.
Kwa mujibu wa mratibu wa Kipye
Cup,Frank Kipye,mashindano hayo ambayo ni msimu wa tatu sasa tangu kuasisiwa
kwake yatashirikisha timu 14 ambapo tati ya hizo 10 zitakuwa zikitokea katika
kata ya Mapogoro wilayani Mbarali na nne ni kutoka nje ya kata hiyo ili kuleta
ushindani.
Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa,Kipye
amesema kamati ya ligi hiyo kesho itakuwa na kazi ya kupitisha timu 14 kati ya
zile zilizochukua fomu kuomba usajiri wa kushiriki mashindano hayo.
Amesema mara baada ya timu shiriki
kuteuliwa,kazi itakayokuwa imesalia ni kutangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa
michuano huku akisisitiza kuwa zawadi kwa msimu huu ni mshindi wa kwanza Ngombe
mwenye thamani isiyopungua shilingi milioni 1.5,mshindi wa pili lakini tano,wa
tatu laki tatu.
“Lengo la mashindano hayo ni kuibua
vipaji vya soka sambamba na kutoa hamasa kwa jamii kupenda michezo kutokana na
faida zake nyingi ikiwemo vijana kuepuka matumizi ya dawa za kulevya,ulevi na
pia ngono zembe.”
Kipye amesema msimu huu mashindano
yanatarajiwa kuwa na mvuto zaidi kutokana na kamati ya maandalizi kuamua
kuongeza idadi ya timu kutoka nje ya kata ya Mapogoro.
“Ligi itaendeshwa katika uwanja
uliopo Mabadaga kata ya Mapogoro.Tumeona tuongeze timu kutoka nje ya kata ili
kuleta mvuto zaidi.Mwaka jana tulishirikisha timu mbili tu kutoka nje ya
kata.”anasema Kipye.
Kwa msimu wa mwaka jana bingwa wa
ligi hiyo ilikuwa timu ya Kapunga FC ambao mwaka huu wanatarajiwa kuwa mabingwa
watetezi.
No comments:
Post a Comment