Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, March 14, 2017

DIWANI WA CHADEMA MBARONI KWA UJANGILI

 Mkuu wa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya akionyesha Mazao ya Misitu ikiwemo mbayo zilizokamatwa kwenye gari ya Diwani wa Kata ya Kambikatoto kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Christopher Mchafu.

DIWANI wa Diwani wa kata ya Kambikatoto wilayani Chunya kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Christopher Mchafu anashikiƙiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ujangili wa mazao ya misitu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Chunya, Rehema Madusa amethibitisha kukamatwa kwa diwani huyo na kubainisha kuwa mtuhumiwa amekuwa akijihusisha na ujangili wa misitu kwa miaka mingi.

Madusa amesema mtuhumiwa alikamatwa usiku wa manane wa kuamkia jana akiwa na gari yake aina ya Toyota Landcruiser yenye namba T 544 BDQ ambayo alikuwa anaiendesha yeye mwenyewe huku akiwa amebeba mbao na milango.

Amesema mtuhumiwa alikamatwa na milango 19 ya nyumba,fremu tisa za milango na mbao 230 ambazo amekuwa akivuna misituni bila utaratibu wala kibali.

Pia Madusa amesema mtuhumiwa amekiuka katazo halali la Serikali ambalo yeye Mkuu wa wilaya alilitoa mwaka jana mwishoni la kusitisha utoaji vibali pamoja na uvunaji wa magogo kwaajili ya mbao na mkaa.

Madusa amesema mtuhumiwa bado anshikiliwa na jeshi la polisi ila anatarajiwa pelekwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayomkabili.

No comments:

Post a Comment