Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, July 1, 2017

MAJAMBAZI WANE WAUAWA KIBITI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 30/06/2017.
MAJAMBAZI WANNE WAUWAWA HUKO KIJIJI CHA PAGAE KIBITI KATIKA MAPAMBANO NA ASKARI YAPATIKANA NA SILAHA MBILI AINA YA SMG NA RISASI 17.

Jeshi la Polisi Tanzania mnamo tarehe 29/06/2017 saa tatu kamili usiku huko katika kijiji cha PAGAE wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, kwenye barabara inayotoka Pagae kuelekea Nyambunda.

Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita wakitokea barabara kuu ya lami wakifuata barabara hiyo inayoelekea Nyambunda kilomita 100 kutoka barabara kuu.

Watu hao walipogundua kuwa watu waliokuwa mbele yao ni Askari Polisi walikimbia vichakani na ghafla wakaanza kuwashambulia askari kwa risasi.
Askari Polisi walijibu mapigo na kuanza kupambana na watu hao.

Katika mapambano hayo askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanne katika kundi hilo la wahalifu hao.

Aidha katika mapambano hayo zilipatikana silaha mbili aina ya Smg na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao.

Watu hao wanne ambao wanasadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaendesha vitendo vya mauaji katika wilaya za Mkoa wa Pwani.

Majeruhi hao walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na kuvuja damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi waliyopata, milli ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi zitakazosaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivi vya kihalifu kwenye wilaya za Mkoa wa Pwani.

Imetolewa na;
L.SABAS -DCP
MKUU WA OPARESHENI MAALUM ZA JESHI LA POLISI TANZANIA.

No comments:

Post a Comment