WANYAMA Tembo watatu wamemvamia na kumjeruhi na
kimsababishia kifo Kikongwe aliyefahamika kwa jina la Sixbertha Mtundu(88)
mkazi wa kitongoji cha Mbuyuni mtaa wa Ihanga kata ya Rujewa wilayani Mbarali
Afisa Mtendaji wa Kata ya Rujewa wilayani Mbarali,John
Mpangala amesema tukio limetokea juzi saa 11 za jioni maeneo yaliyopo jirani na
Ikulu ndogo ya wilaya ya Mbarali.
Mpangala amesema kikongwe huyo amevamiwa na tembo
hao wakati akitokea shambani kwake na inasadikika kutokana na umri wake mkubwa
huenda hakuwaona wanyama hao mapema na pia alishindwa kukimbia baada ya
kuvamiwa.
Hata hivyo Afisa mtendaji huyo amesema tukio hilo
liligunduliwa na msamaria mwema mmoja aliyepita eneo hilo na kukuta kikongwe
huyo akiwa amelala njiani huku amejeruhiwa vibaya kwa kukanyagwa na tembo na
ndipo mkazi huyo alikwenda kwa mwenyekiti wa kitongoji na kumjulisha na ndipo
wakaenda eneo husika ikiwa ni majira ya saa moja na nusu usiku lakini wakakuta
amekufa.
Afisa mtendaji huyo amesema walichokifanya baada ya
tukio hilo ni kuwapa taarifa wenyeviti wa vitongoji vya maeneo ya jirani ili
waweze kuwapa tahadhali wananchi kuwa bado tembo hawajulikani walipo japo njia
waliopikuwa wakielekea inakwenda eneo la Hifadhi ya Mpanga Kipengele hivyo
huenda wapo au wamekwenda hifadhini.
Amesema eneo la tukio kwa miaka ya nyuma ilikuwa
njia(Shoroba) ya wanyama lakini baada ya shughuli mbalimbali za kibinadamu hususani
kilimo na makazi kukithiri wanyama hawakuendelea kupita tena.
No comments:
Post a Comment