Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, October 4, 2018

ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGE LUGOLA MKOANI MBEYA

 Akipokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Ulrich Matei ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya,Albert Chalamila.
 Akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Magereza,katika Gereza la Luanda Mbeya.
 Akikagua ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Mbalizi
 Akizungumza na mkaguzi wa magari wa Jeshi la Polisi.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

                         Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                   Mkoa  wa  Mbeya,                                                                                  
Namba ya simu 2502572                                                                                               S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                   MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
              tanpol.mbeya@gmail.com
                                                       
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 03.10.2018.

ZIARA YA KIKAZI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MKOANI MBEYA.

Tarehe 03.10.2018 kuanzia majira ya saa 09:30 asubuhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa KANGI LUGOLA amefanya ziara ya kikazi Mkoani Mbeya ambapo alianza kwa kutembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa ALBERT CHALAMILA na kisha kuongea na waandishi wa habari kuhusu lengo la ziara yake.

Mhe. KANGI LUGOLA ameeleza kuwa lengo la ziara yake ni kukagua na kufanya ufuatiliaji wa maelekezo aliyoyatoa mnamo tarehe 04.07.2018 alipofika Mkoani Mbeya kukagua eneo ilipotokea ajali Mlima Iwambi na kusababisha vifo vya watu 20 na majeruhi 28.

Baada ya kukagua eneo la ajali, Mhe.Waziri alitoa maelekezo ya kufanya ukaguzi wa magari kabla na baada ya safari, kukagua na kufanya uhakiki wa leseni za madereva, kuwapima ulevi madereva pamoja na kudhibiti mwendo kasi.

Katika ziara yake Mhe. KANGI LUGOLA ametembelea na kukagua Gereza la Ruanda na kuongea na mahabusu na wafungwa waliomo gerezani humo pamoja na kujione shughuli mbalimbali zinazofanywa na wafungwa katika Gereza hilo.

Pia alitembelea eneo la Iwambi na kukagua zoezi la ukaguzi wa magari linalofanywa na maafisa wa Polisi [Vehicle Inspectors] sambamba na kujionea mkakati wa kuzuia ajali maeneo ya milima ambapo magari ya abiria na mizigo hupita tofauti katika maeneo hayo ili kuzuia ajali au kupunguza madhara makubwa yasitokee pindi ajali zinapotokea.



Aidha ziara ya Mhe.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi imekamilika kwa kutembelea na kukagua ujenzi unaoendelea wa kituo kipya cha Polisi Mbalizi, ujenzi unaofanywa kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Katika ukaguzi wake Mhe.KANGI LUGOLA amesisitiza wananchi kuendelea kuchangia ujenzi wa Kituo Kipya cha Polisi Mbalizi kilichopo Wilaya ya Mbeya Vijijini ili kikamilike kwa wakati. Aidha katika kuzuia uhalifu, Mhe Waziri amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi hasa katika utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu.

               Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment