Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, March 29, 2013

MAWAZIRI WAZOMEWA MTWARA

MAWAZIRI wawili wa Rais Jakaya Kikwete, jana walionja ‘joto la jiwe’ baada ya wananchi wa Mtwara kuwazomea mkutanoni na hivyo kulazimika kukatiza mkutano wao. Mawaziri hao ni Dk. Abdallah Kigoda wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba, waliokuwa wameongozana na Balozi wa Nigeria hapa nchini, Nshaya Manjabu, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dangote ya Nigeria, Deva Kumar. Tukio hilo limekuja zikiwa ni wiki chache tangu kutokea kwa vurugu kubwa mkoani humo katika wilaya za Mtwara Mjini na Masasi ambapo wananchi waliharibu mali za baadhi ya viongozi wa kisiasa na serikali na kumuua askari mmoja huku watu wengine wanne nao wakiuawa kwa kupigwa risasi. Wananchi hao wa Mtwana na Lindi wamekuwa na msimamo mkali wakipinga serikali kujenga bomba la kusafirisha gesi asili kutoka kwao kwenda jijini Dar es Salaam bila kuwekewa mazingira mazuri ya kiuchumi. Katika kuonyesha kuwa wananchi hao walikuwa wamepania kuwasulubu mawaziri hao, walifika mkutanoni huku baadhi yao wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kuhoji mkutano huo umeruhusiwa na nani wakati serikali imepiga marufuku mikutano na maandano mkoani humo kwa muda. Mara baada ya viongozi hao kufika uwanjani, Waziri Kigoda aliwasalimia wananchi akisema: “Mtwara oyeee!!!” Waziri huyo aliitikiwa na wananchi: “Haitoki hata kama umekuja wewe hatutaki wala hatukuelewi! Mlikuwa wapi kuja huku mapema kutuelewesha habari za viwanda?” Wanachi hao walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe uliosomeka: “Kauli mbiu: gesi haitoki, tunashukuru baada ya kimya kirefu sasa leo mmefungua rasmi mikutano tukianzia huu mkutano wenu na gesi ndio roho yetu.” Wakati ‘zomeazomea’ hiyo ikiendelea, baadhi yao walianza kurusha mawe katika hali iliyowalazimu viongozi kuufunga mkutano huku Jeshi la Polisi likiamuru wananchi kutawanyika katika viwanja vya mkutano. Mara baada ya hali hiyo ya vurugu, Naibu Waziri wa Uchukuzi alilazimika kuwatuliza wananchi ili wasikilize akisema: “Nisikilizeni mtaelewa tu, mwekezaji amepatikana na amemaliza hatua ya kwanza ya kufanya makadilio ya gharama za ujenzi.” Aliongoza kuwa mamlaka ya viwanja vya ndege inafanya mazungumzo naye ili masharti ya uwekezaji yaweze kufahamika na upanuzi wa uwanja kuanza mapema. Hata hivyo, wananchi hao hawakutulia huku wakiendelea kupiga kelele na kuwazomea: “Hilo ni changa la macho, hatutaki propaganda zenu, tumechoka na siasa zenu.” Mkuu wa Mkoa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia, hakupata nafasi ya kuzungumza kutokana na wananchi hao kuzomea huku wakimtaka aondoke. Awali, Kigoda akizungumza katika viwanja vya bandari ya Mtwara na watumishi mbalimbali, alisema kuwa lengo la ujio wake mkoani humo ni makabidhiano ya makontena 38 ya vifaa vya ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dagonte kinachotarajiwa kujengwa katika kijiji cha Msijute, wilaya ya Mtwara vijijini. Makabidhiano hayo yalikuwa kati yake na Naibu Waziri wa Uchukuzi. Pamoja na mambo mengine, Kigoda alisema kuwa serikali itaendelea kupokea wawekezaji mbalimbali watakaoomba kuwekeza katika mkoa huo. Alisema wanaangalia zaidi uwekezaji katika ujenzi wa viwanda kwa kuwa Mtwara ni kitovu cha uchumi wa taifa huku akisisitiza kuwa utafiti wa kitaalamu na kisayansi unaonyesha gesi hapa Mtwara ni nyingi sana. Alisema viwanda vingi vitajengwa hapa na gesi itakayobaki lazima itapelekwa katika maeneo mengine. KWA HISANI YA BLOGU YA JUMA MTANDA

BABA AMUUA MWANAE NA KUMZIKA SEBULENI KWAKE

MTOTO Debora Riziki(3) mkazi katika kitongoji cha Iponjola kijiji cha Isange wilayani Rungwe ameuawa na kisha kufukiwa katika shimo ndani ya nyumba ya baba yake mzazi. Baba wa mtoto Debora aliyefahamika kwa jina la Riziki Mwangoka(27) mkazi wa Iponjola ndiye aliyetajwa kuhusika na mauaji ya mwanaye yaliyogundulika Machi 27 mwaka huu majira ya saa 7:40 mchana nyumbani kwa mzazi huyo. Chanzo cha mauaji hayo kimetajwa kuwa ni mgogoro wa ndoa baina ya Mwangoka na aliyekuwa mkewe Esther Mwambenja(23) anayeishi kwa sasa katika kitongoji cha Kibumbwe kijijini Kiwira wilayani hapo. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani athumani alisema mgogoro wa wanandoa hao waliotengana katika kipindi kisichojulikana ulipelekea wawili hao kuwa na mvutano wa nani aishi ni mtoto wao Debora. Kamanda Athuman alisema kufuatia hali hiyo mnamo Novemba 28 mwaka jana majira ya saa 11:00 jioni Mwangoka alimchukua kwa nguvu mtoto Debora kutoka kwa mama yake na kuondoka nae kijijini kwao. Alisema baada ya kufika huko pasipo huruma wala uchungu na damu yake alimuua mwanaye huyo na kisha kuchimba shimo katika sebule ya nyumba yake na kisha kumzika humo na kufukia. Alifafanua kuwa pasipo hofu yoyote,baba huyo aliendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo yenye kaburi la mwanae ndani hadi juzi ilipogundulika siri aliyoificha katika kipindi hicho chote. Kamanda huyo alisema baada ya kugundulika mwili wa mtoto Debora ulifukuliwa na daktari kuufanyia uchunguzi kisha ukakabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya kuuzika. Kwa mujibu wa Diwani mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na polisi wakati taratibu mbalimbali zikiendelea ili aweze kufikishwa mahakamani.

Monday, March 25, 2013

KAMANDA WA POLISI MKOANI MBEYA DIWANI ATHUMAN AMEPONGEZA HATUA YA WAFUASI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA KUTOKUBALIANA NA AGIZO LA UONGOZI WA CHAMA HICHO KUWATAKA WAANDAMANE HII LEO KUSHINIKIZA MAWAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNZI NCHINI KUJIUZURU.BAADHI YA WANANCHI NAO WAMESEMA HAWAKO TAYARI KUONA WANASHINDWA KUFANYA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI NA KUINGIA BARABARANI KUANDAMANA

JAMBAZI AUAWA KWA RISASI

JAMBAZI mmoja ameuawa baada ya kupigwa risasi wakati wa majibizano ya risasi kati ya polisi na majambazo wane. Majibizano hayo ya risasi kati ya pande hizo mbili yalitokea (Machi 25) majira ya saa 10:00 alfajiri katika eneo la Mlimanyoka nje kidogo ya jiji la Mbeya. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani Athuman alisema jambazi aliyeuawa alipigwa risasi mbili moja kiunoni na nyingine ubavu wake wa kulia. Kamanda Athumani alisema baada ya kumpekua jambazi huyo alikutwa na kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la Emanuel Blasius Mdendemi aliyezaliwa 1984 eneo la Matamba wilayani Maketena makazi yake ni Uwemba Njombe. Alisema awali jambazi huyo akiwa na wenzake watatu walikuwa wamefunga barabara kuu ya Mbeya/Iringa kwa kuweka mawe wakiwa na lengo la kuteka magari yatakayopita usiku huo na walipoona mwanga wa taa za gari walijitokeza kutoka vichakani pasipo kujua kama ilikuwa gari ya polisi. Alisema baada ya polisi kufika eneo hilo walitoa amri ya kuwataka jambazi hao kujisalimisha lakini badala ya kutii walianza kurusha hovyo risasi na ndipo ikawalazimu polisi kuanza kujibu. Hata hivyo majibizano ya risasi yaliyodumu kwa muda mfupi yalifanikiwa kumjeruhi jambazi huyo mmoja aliyefariki muda mfupi baadaye huku wenzake watatu wakifanikiwa kutoroka kwa kukimbilia msituni. Alisema pamoja na kumuua jambazi huyo pia polisi walifanikiwa kukamata bunduki aina ya Sub Machine Gun(SMG) iliyokuwa na risasi 22 kwenye magazine yake pamoja na mapanga mawili. Kamanda huyo pia alisema uchunguzi umebaini kuwa jambazi aliyeuawa ni sehemu ya mtandao wa majambazi waliokamatwa hivi karibuni ukihusishwa na matukio mbalimbali ya uharifu yaliyofanyika katika mikoa ya Mbeya,Iringa na Njombe likiwamo la mauaji ya askari wa kituo kidogo cha Mkwajuni wilayani Chunya PC Jafari yaliyotokea februari sita mwaka huu.

Tuesday, March 19, 2013

MWANAFUNZI MBARONI KWA NOTI BANDIA

WATU wawili akiwemo mwanafunzi wa shule ya sekondari Ndembela wilayani Rungwe wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukamatwa na noti bandia. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman alisema watu hao walikamatwa jana (Machi 18) majira ya saa 1:20 asubuhi katika Benki ya NBC tawi la Tukuyu wilayani Rungwe. Kamanda Athuman aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni mwanafunzi Chasco Nsaji(18) waliyekuwa na mkulima Hanberd Sanga(49) mkazi wa eneom la Kiwira road katika mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe. Alisema kwa pamoja watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na noto bandia nane zenye thamani ya shilingi 10,000 kila moja wakiwanataka kuingiza fedha hizo kwenye akaunti ya shule kwaajili ya malipo ya karoya mwanafunzi huyo. Alisema mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo Ezekia Mwambwanji(50) ndiye aliyebaini fedha hizo kuwa zilikuwa bandia na kuamua kutoa taarifa kituo cha polisi na kuwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wote. Alisema kati ya noti hizo noti tatu zilikuwa na namba AA 4243040,na nyingine moja moja zilikuwa na namba AA 0012030,CQ 1547949,BH 0012032,BF 1547938 na DT 1547949.

Monday, March 4, 2013

MWANDISHI APIGWA KIBAO NA MWALIMU MKUU

walimu wa shule ya msingi Tunduma leo walinyangánya kamera ya mwanahabari huyu Keneth Goliama pichani baada ya kuwapiga picha ,wakati walimu wakiwa katika operation ya kuwachapa viboko wanafunzi asubuhi saa mbili,wakiongozwa na mkuu wa shule hiyo na kutaka kuivunja lakini mwalimu mmoja aliyeonyesha kujua nini maana ya habari akawaamuru kutoivunja kamera hata kama walilkuwa na makosa, "Walimu hao ambao wakati wa maongezi walisema Serikali inatutesa na nyinyi waandishi mnataka kutuonyesha tunavyofanya watesa wanafunzi na kusema hili halitawezekana lakini baada ya muda nikawaruhusu kuivunja kamera kusubiri sharia kuchukua mkondo lakini wakaacha na kuzifuta picha".anasema Goliama na kuongeza "walimu walijipanga mistari huku wanaichi wakishaangaa barabarani sasa wakati natoka home naenda kazini , nikaona mwalimu anampiga fimbo wanafunzi wakati amesimama nikaamua kupiga baada ya hapo walimu watatu wakaja mkuu wa shule akaninipiga kibao halafu badaye akaomba msamaha kwasabu najua journalist ni challenge nikaamua kumsamehe ilikuwa saa mbili na dakika 10"

HATARIIIIIIIIIIIIII

MBWA AKIWA HOI BAADA YA KUNYWA POMBE NA KUVUTA SIGALA

HARUFU YA MGOGORO WA ARDHI INAANZA KUNUKIA WILAYANI MBOZI.NI BAADA YA MAAFISA ARDHI KUGAWA VIWANJA NA KURUHUSU UJENZI WA NYUMBA KWENYE ENEO LA ARDHI OEVU

MBIO ZA BAISKELI MBEYA ZAFANA

BAADA ya kusuasua kwa kipindi cha miaka mine iliyopita hatimaye mashindano ya mbio za baiskeli jijini Mbeya yamefanyika mwishoni mwa wiki jana. Katika mashindano hayo ya kilometa 140 Mashaka Jonas aliibuka bingwa baada ya kutumia masaa matatu na dakika 47 akiwaacha washiriki wengine 15. Mshindi wa pili alikuwa Kiang Samson aliyetumia masaa matatu na dakika 59 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Jailos John aliyetumia muda wa masaa manne na dakika 11 kumaliza kilometa hizo. Mshindi wa kwanza wa mbio hizo zilizondaliwa na kampuni ya Range of Vision Marketing Limited(RVMCL) ya jijini Mbeya alizawadia jumla ya shilingi laki 1.5,mshindi wa pili shilingi 100,000 na wa tatu shilingi 50,000. Akikabidhi zawadi hizo afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya jiji la Mbeya Vicent Msola kwa niaba ya mkuu wa mkoa Abbas Kandoro alisema mbio za baiskeli ni miongoni mwa michezo inayotambuliwa na serikali na kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau wanaoandaa mashindano hayo. Msola alisema jamii inapaswa kutambua umuhimu wa michezo na kusisitiza kufufuliwa kwa michezo mbalimbali ambayo kwa sasa inaonekana kutochezwa ili kutoa fursa kwa vijana kushiriki kwa kila mmoja na kipaji chake.

Sunday, March 3, 2013

WALEMAVU WATAKA UWAKILISHI KWA KUCHAGULIWA

CHAMA cha watu wenye ulemavu (CHAWATA) mkoani Mbeya kimependekeza katiba ijayo iruhusu wawakilishi wa walemavu katika ngazi ya halmashauri na bunge wapatikane kwa kupigiwa kura. Mapendekezo hayo yametolewa na wajumbe waliohudhuria mdahalo wa kuwajengea uwezo walemavu kuchambua katiba ya nchi ya sasa na kuibua mapendekezo ya kuingizwa kwenye katiba mpya uliofanyika katika ofisi za chama hicho jijini hapa kwa ufadhili wa shirika la The Foundation For Civil Society. Mmoja wa wajumbe hao Willium Simwali kutoka wilayani Mbeya amesema mfumo uliopo sasa wa rais kuteua mwakilishi wa jamii ya walemavu bungeni hautoi demokrasia badala yake mwakilishi huyo alipaswa kupatikana kwa kupigiwa kura. Simwali amesema vyama vya watu walio na ulemavu ndivyo vinapaswa kushiriki mchakato wa kutafuta mwakilishi kuanzia katika ngazi za mitaa kwa kila kimojawapo kutoa mgombea na kumshindanisha na vyama vingine vya watu wa jamii hiyo. Naye Isaya Kyando kutoka Mbozi ametaka katiba ijayo itoe maelekezo ya vifaa kwaajili ya walemavu kuuzwa kwa bei zitakazowawezesha kumudu kununua na pia serikali kuwa na fungu kwaajuili ya kuwawezesha watu wa jamii hiyo hususani kwa kuwanunulia vyombo vya usafiri. Mwenyekiti wa Chawata mkoani hapa Jimmy Ambilikile amesema mdahalo huo umehudhuliwa na wajumbe wawakilishi kutoka wilaya zote za mkoani hapa ambao licha ya kutoa maoni yao pia watapeleka mrejesho wa wanachama watakaporejea wilayani kwao

Friday, March 1, 2013

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

CHINI NI KIBAKA ALIYEVAMIA DUKA LA KIBOLOMA BROATHERS KANDO KANDO YA BARABARA YA SOKOINE MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA ALIPOISHIA KUPATA KICHAPO TOKA KWA MMILIKI WA DUKA BAADA YA KUIBA PAKITI 6 ZA SIGARA. WANAFUNZI WA SHULE YA MSOINGI SISIMBA JIJINI MBEYA WAKIGOMBANIA KUNUNUA VYAKULA TOKA KWA AKINA MAMA WANAOUZA NJE YA GETI LA SHULE HIYO.GATA HIVYO BAADAYE MGAMBO WA JIJI WALIINGILIA SHUGHULI HIYO NA KUSABABISHA WANAFUNZI KUKIMBIA WAKATI MGAMBO HAO WALIPOTAKA KUWAKAMATA NA KUISHIA KUBISHANA NA MMILIKI WA BLOGU YA Lyamba Lya Mfipa KAMA INAVYOONEKANA KATIKA PICHA YA MWISHO. HAPA NI KATIKA KIJIJI CHA KITANDA WILAYANI TUNDURU MKOANI RUVUMA AMBAPO GARI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU ILIKWAMA NA KUWALAZIMU ABIRIA WAKE KUSHUKA NA KUANZA KULINASUA KATIKA TOPE KWA KUSUKUMA

COCA COLA MBEYA