Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, March 25, 2013

JAMBAZI AUAWA KWA RISASI

JAMBAZI mmoja ameuawa baada ya kupigwa risasi wakati wa majibizano ya risasi kati ya polisi na majambazo wane. Majibizano hayo ya risasi kati ya pande hizo mbili yalitokea (Machi 25) majira ya saa 10:00 alfajiri katika eneo la Mlimanyoka nje kidogo ya jiji la Mbeya. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani Athuman alisema jambazi aliyeuawa alipigwa risasi mbili moja kiunoni na nyingine ubavu wake wa kulia. Kamanda Athumani alisema baada ya kumpekua jambazi huyo alikutwa na kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la Emanuel Blasius Mdendemi aliyezaliwa 1984 eneo la Matamba wilayani Maketena makazi yake ni Uwemba Njombe. Alisema awali jambazi huyo akiwa na wenzake watatu walikuwa wamefunga barabara kuu ya Mbeya/Iringa kwa kuweka mawe wakiwa na lengo la kuteka magari yatakayopita usiku huo na walipoona mwanga wa taa za gari walijitokeza kutoka vichakani pasipo kujua kama ilikuwa gari ya polisi. Alisema baada ya polisi kufika eneo hilo walitoa amri ya kuwataka jambazi hao kujisalimisha lakini badala ya kutii walianza kurusha hovyo risasi na ndipo ikawalazimu polisi kuanza kujibu. Hata hivyo majibizano ya risasi yaliyodumu kwa muda mfupi yalifanikiwa kumjeruhi jambazi huyo mmoja aliyefariki muda mfupi baadaye huku wenzake watatu wakifanikiwa kutoroka kwa kukimbilia msituni. Alisema pamoja na kumuua jambazi huyo pia polisi walifanikiwa kukamata bunduki aina ya Sub Machine Gun(SMG) iliyokuwa na risasi 22 kwenye magazine yake pamoja na mapanga mawili. Kamanda huyo pia alisema uchunguzi umebaini kuwa jambazi aliyeuawa ni sehemu ya mtandao wa majambazi waliokamatwa hivi karibuni ukihusishwa na matukio mbalimbali ya uharifu yaliyofanyika katika mikoa ya Mbeya,Iringa na Njombe likiwamo la mauaji ya askari wa kituo kidogo cha Mkwajuni wilayani Chunya PC Jafari yaliyotokea februari sita mwaka huu.

No comments:

Post a Comment