Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, May 30, 2024

TULIA ADHAMINI TULIA CUP UYOLE 2024 AMWAGA 11M NA VIFAA VYA MICHEZO


Mchezaji wa zamani wa soka Simon Sanga aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa akizungumza jambo
Meneja wa Taasisi isiyo ya serikali ya Tulia Trust, Jacqueline Boaz akisalimiana na wachezaji kabla ya mtanange wa ufunguzi kuanza




Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya Sadiki Jumbe akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi


 Na Mwandishi Wetu

Michuano ya soka Tulia Trust kwa ushirikiano na Raphael Group imezinduliwa rasmi katika Uwanja wa Mawinji Uyole ya Kati Mgeni rasmi akiwa ni Simon Sanga mchezaji wa zamani wa soka.


Meneja wa Taasisi isiyo ya serikali ya Tulia Trust Jacqueline Boaz amesema michuano hiyo inadhaminiwa kwa mwaka wa nne mfululizo na taasisi hiyo ambapo mwaka huu udhamini ni wa Shilingi 11,450,000.

Boaz amesema lengo la Taasisi ni kukuza michezo na kutoa fursa ya ajira kwa vijana na jumla ya timu thelathini na nne zinashiriki michuano hiyo na kila timu imepatiwa seti ya jezi na mipira.

Awali Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa Miguu Jiji la Mbeya John Gondwe amesema michuano hiyo imekuwa ikiibua vipaji kwa vijana Jijini Mbeya.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya Sadiki Jumbe amemuomba Mgeni rasmi kuwa mdhamini wa Chama Cha Wanawake mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya.

Akijibu ombi la ulezi wa Chama Cha mpira wa Miguu Simon Sanga amekubali kuwa mlezi wa Chama hicho.

Sanga ameomba wadau kutovamia Viwanja vya michezo ili vijana wapate maeneo ya kucheza waweze kuepukana na vitendo viovu.

Hata hivyo ameomba kutilia mkazo zaidi soka la Wanawake ambalo halijapewa kipau mbele Mkoani Mbeya.

Katika kutia hamasa michuano hiyo Taasisi ya Tulia Trust itatoa zawadi kwa mfungaji bora, golikipa bora na timu yenye nidhamu.

Mshindi wa kwanza atapata kikombe na pesa shilingi milioni tano,mshindi wa pili shilingi milioni tatu,wa tatu shilingi milioni mbili na mshindi wa nne atapata shilingi milioni moja.

Golikipa bora atapata shilingi laki moja, mfungaji bora shilingi laki moja,timu yenye nidhamu itapata shilingi laki moja mfungaji na kikundi chenye hamasa kitajinyakulia pia shilingi laki moja na mwandishi bora wa michezo atajinyakulia shilingi elfu hamsini.

No comments:

Post a Comment