Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, July 2, 2024

BONANZA BAAAB KUBWA KUFANYIKA WEEKEND HII

 


Timu ya watumishi ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya inataraji kwenda Jijini Mbeya Mwishoni mwa wiki hii July 6, 2024 Kushiriki katika Bonanza la Watumishi Lililoandaliwa na Afisa Michezo Mkoa wa Mbeya, litakalofanyika katika Uwanja wa Sokoine

Timu hii ya Watumishi wilaya ya Chunya katika Mechi nne mfululizo haijafungwa na inakwenda Mbeya kulinda heshima na Hadhi ya Wilaya ya chunya

Monday, July 1, 2024

NDIYOOO!! MWAMBA WA LUSAKA KATUA JANGWANI!

 


MIAKA 33 iliyopita ndipo alizaliwa katika familia iliyosheheni Vipaji vya soka. Akakulia Zambia, Akahitimu elimu ya Sekondari 2009.

 

Kisha akajikita rasmi kwenye Soka akiwa na Zesco United. Akaisaidia Zesco kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa  Afrika

Kipaji kikampeleka kucheza katika nchi mbalimbali zikiwemo Misri, Morocco na Tanzania yenyewe ambako amekuwa Mchezaji bora wa muda wote wa Tanzania.

 

Ni Mchezaji mwenye mguu wa dhahabu, huchoki kumtazama, anakupa matokeo wakati wowote. Anafunga na ana-assit na kuburudisha kwa Pamoja.

 

Si mwingine, huyu ni Fundi Clatous Chama, naam! Ndiye yeye  "Mwamba wa Lusaka" hii leo amejiunga na Klabu ya Yanga SC, Mabingwa wa Soka la Tanzania.

 

Matarajio ya wapenda soka ni kuwa baada ya kutua Jangwani rasmi sasa ataendelea kutamba  kwenye Uwanja wake aliouzoea, Uwanja anaoutumia siku zote kuandika na kuvunja rekodi zake na kuweka mpya, Uwanja wa Benjamin Mkapa... Ndiyo! Lupaso!

 

Je Mwamba wa Lusaka bado yupo yupo sana kuwatesa Mabeki akiwa katika soka la Tanzania? Au mambo yatakuwa tofauti!, Acha Inyeshe Tuone Panapovuja!!!

YUSUF MANJI AFARIKI DUNIA