Saturday, October 22, 2016
Wednesday, October 19, 2016
WATU SITA WAFA KWA AJALI MBEYA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa
wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 19.10.2016.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya
misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti
uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine
katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio
makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Mafanikio
yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO]
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Kitongoji cha Masanza
Wilaya ya Chunya aliyefahamika kwa jina la CHRISTINA
PHILIPO [44] akiwa na Pombe haramu ya moshi [gongo] yenye ujazo wa lita 05.
Mtuhumiwa
alikamatwa mnamo tarehe 18.10.2016
majira ya saa 11:00 asubuhi katika
msako uliofanyika huko Kitongoji cha Masanza, kijiji na kata ya Bwawani, Tarafa
ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya.
Aidha
mtuhumiwa alikamatwa akiwa na Mtambo mmoja wa kutengenezea Pombe hiyo haramu.
Taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya pia
linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha
madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii sheria za usalama barabarani.
Aidha kumekuwa na tukio 01 la ajali ya kifo kama ifuatavyo:-
AJALI YA VIFO.
Mnamo tarehe 18.10.2016 majira ya saa
15:50 jioni huko katika Kijiji cha Majimazuri, Wilaya ya Mbeya Vijijini
katika Barabara ya Mbeya/Chunya Gari lenye namba za usajili T.841 BRW aina ya
Isuzu basi likitokea Wilaya ya Chunya kwenda Mbeya likiendeshwa na dereva
aitwaye ELIA ISACK [37] Mkazi wa
Chunya liliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo kwa abiria wanne ambao ni
1.
HAWA MOHAMED [30] mkazi wa
Chunya 2. Mtoto mdogo miaka 2 wa kiume ambaye bado
kufahamika jina lake 3. Mwanaume asiyefahamika
jina na 4. Mwanaume asiyefahamika.
Aidha
katika ajali abiria 22 walijeruhiwa kati
yao wanawake 14 na wanaume 08. Majeruhi walitambulika kwa majina ya 1. HAPPY BAKARI [28] Mkazi wa Mabatini 2. FAIDA MBUYI [47] mkazi wa Igodima
3. AGNESS LUSUPA [45] Mkazi wa Ileje
4. EMMY MWASIMBIHABI [35] Mkazi wa Mwakaleli 5. LONGI MWALUVANDA [45]
Mkazi wa Chunya 6. SIWANGU PAUL [28]
Mkazi wa Simike 7. RODA GUNZA [38] Mkazi wa Chunya 8. ANITHA FRANK [18]
Mkazi wa Igodima 9. MAGDALENA ALMASI
[19] Mkazi wa Iganzo 10. AGNESS NDOKILE [38] Mkazi wa Iganzo
11.
ELIZA GIDION [21] Mkazi wa Chunya 12.
JULIANA MWAMPASHI [36] Mkazi wa Chunya 13.
SARAH ENOCK umri wa mwaka mmoja na nusu Mkazi wa Chunya na 14. EMMA ANGETILE [35]
Mkazi wa Chunya.
Majeruhi
wengine ni 1. MOSES JACKSON [29]
Mkazi wa Itaka 2. JOHNPHANCE SAMSON
[35] Mkazi wa Mbozi 3. PETRO LYANGA [24] Mkazi wa Tunduma 4. ISSA KALINGA [18] Mkazi wa Chunya 5. RICHARD KIHAMI mkazi wa Chunya 6. STARD MWASHITETE [34] Mkazi wa Mbozi 7. MWANDALIMA JOSEPH miaka kati ya 35 – 40 na 8.
CHEYO NDELE [32] Mkazi wa Mbeya.
Chanzo
cha ajali ni mwendo kasi. Majeruhi wote wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Dereva amekamatwa, Upelelezi
unaendelea.
Mnamo tarehe 18.10.2016 majira saa 21:41 usiku huko eneo la Mlima Nyoka, Kata
ya Itewe, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Gari lenye namba za
usajili T.660 APR aina ya Toyota Pick up ikiendeshwa na dereva aliyefahamika
kwa jina la JACOB SANGA iliacha njia
na kupinduka kisha kusababisha kifo cha RAHEL
SASITA [55] Mkazi wa Itewe.
Aidha
katika ajali hiyo watu wawili walijeruhiwa ambao ni 1. ANNA SANGA [45] Mkazi wa Chemchem na 2. VENANCE OSIA [50] Mkazi wa Mwanyanje. Chanzo cha ajli ni mwendo
kasi. Majeruhi wamelazwa Hospitali ya Igawilo. Dereva alikimbia mara baada ya
tukio. Upeleleziunaendelea ikiwa ni pamoja na kumtafuta mtuhumiwa.
Mnamo tarehe 18.10.2016 majira ya saa 20:50 usiku huko katika Kijiji na kata
ya Itope, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, Gari lenye namba
za usajili T.574 BNQ aina ya Toyota Coaster mali ya Kanisa la Uinjilisti Kiwira
ikiendeshwa na dereva JAFARI SIMON [27]
mkazi wa Tukuyu ilimgonga mpanda baiskeli aliyefahamika kwa jina la WEMA EDWIN [10] mwanafunzi wa darasa la
tano katika Shule ya Msingi Mbogola na kusababisha kifo chake papo hapo. Chanzo
cha ajali ni mwendo kasi. Dereva amekamatwa. Upelelezi unaendelea.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada
zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala
salama. Kumekuwa na tukio 01 la mauaji kama ifuatavyo:-
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la JAMSON
SANGA [42] fundi ujenzi, mkazi wa Nsalaga – Uyole alifariki dunia akiwa
anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Awali
mnamo tarehe 17.10.2016 majira ya saa 13:00 mchana marehemu akiwa njiani
akirudi nyumbani kutoka shambani eneo la Mlimanyoka, kata ya Itewe, tarafa ya
Tembela alivamiwa na watu wasiofahamika na kisha kumjeruhi kwa kumkatwa kwa kitu
chenye ncha kali.
Marehemu
alifariki tarehe 18.10.2016 majira ya saa 12:45 mchana. Upelelezi unaendelea ili kuwabaini na
kuwakamata waliohusika katika tukio hili.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi
DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito
kwa madereva kuwa makini kwa kuzingatia na kufuata sheria na alama za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika. Pia Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za mtu/watu au
kikundi cha watu wanaojihusisha na uuzaji na upikaji wa pombe haramu ya Moshi @
gongo ili wakamtwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A.
KIDAVASHARI - DCP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Subscribe to:
Posts (Atom)