Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, April 21, 2015

RATIBA ZA MICHEZO TANZANIA


2015-04-21
VPL
18:00
YANGA
Vs    
STAND UNITED
U/Taifa

2015-04-22
VPL
16:00
SIMBA SC
Vs    
MGAMBO JKT
U/Taifa

2015-04-24
VPL
16:00
RUVU SHOOTING
Vs    
YANGA
U/Taifa

2015-04-25
VPL
16:00
MBEYA CITY
Vs    
KAGERA SUGAR
Sokoine
VPL
16:00
SIMBA SC
Vs    
NDANDA FC
U/Taifa
VPL
16:00
POLISI MORO
Vs    
COASTAL UNION
Jamhuri
VPL
19:00
AZAM FC
Vs    
STAND UNITED
Azam comp

2015-04-26
VPL
16:00
MTIBWA SUGAR
Vs    
JKT RUVU
Manungu
VPL
16:00
T.PRISONS
Vs    
MGAMBO JKT
Sokoine

2015-04-27
VPL
16:00
YANGA
Vs    
POLISI MORO
U/Taifa

2015-05-02
VPL
16:00
NDANDA FC
Vs    
KAGERA SUGAR
Nangwanda
VPL
16:00
T.PRISONS
Vs    
MBEYA CITY
Sokoine
VPL
16:00
MGAMBO JKT
Vs    
JKT RUVU
Mkwakwani
CAF conf
16:00
Etoile Du Sahel
Vs    
YANGA
TUNISIA

2015-05-03
VPL
16:00
COASTAL UNION
Vs    
STAND UNITED
Mkwakwani
VPL
16:00
SIMBA SC
Vs    
AZAM FC
U/Taifa
VPL
16:00
MTIBWA SUGAR
Vs    
RUVU SHOOTING
Manungu

2015-05-07
VPL
16:00
AZAM FC
Vs    
YANGA
U/Taifa

2015-05-10
VPL
16:00
JKT RUVU
Vs    
SIMBA SC
U/Taifa
VPL
16:00
MTIBWA SUGAR
Vs    
COASTAL UNION
Manungu
VPL
16:00
STAND UNITED
Vs    
RUVU SHOOTING
Kambarage
VPL
16:00
MBEYA CITY
Vs    
POLISI MORO
Sokoine
VPL
16:00
KAGERA SUGAR
Vs    
T.PRISONS
Kaitaba
VPL
16:00
NDANDA FC
Vs    
YANGA
Nangwanda
VPL
16:00
AZAM FC
Vs    
MGAMBO JKT
Azam comp

2015-05-17
COSAFA
16:00
LESOTHO
Vs    
TANZANIA
South Africa

2015-05-19
COSAFA
16:00
TANZANIA
Vs    
NAMIBIA
South Africa

2015-05-21
COSAFA
16:00
ZIMBABWE
Vs    
TANZANIA
South Africa

2015-06-18
CHAN qulf
16:00
TANZANIA
Vs    
UGANDA
U/Taifa

2015-09-11
Kirafiki
16:00
TANZANIA
Vs    
BATA BULLETS
U/Azam comp


MBUNGE,MWENYEKITI CCM NUSURA WAZICHAPE KAVU KAVU MBELE YA WAZIRI

 Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu(Kushoto) na Mbunge wa Mbarali Dickson Kilufi wakisaini vitabu vya wageni baada ya kuwasili Ubaruku kuwasikiliza wananchi juu ya mgogoro wa mpaka kati ya vijiji 21 na Tanapa.

 Moja ya mabango yaliyoandikwa ujumbe na wananchi wahanga wa uhamisho
 Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu wakiwa na
Mwenyekiti wa CCM wilaya Mathayo Mwangomo baada ya kuhutubia wananchi.





                                 HABARI KAMILI

KATIKA kuonesha hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Mbarali,mbunge wa jimbo hilo Mbarali Dickson Kilufi na Mwenyekiti wa CCM wilaya Mathayo Mwangomo,hivi karibuni nusura wapigane Mbelea ya waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.

Nyalandu aliwasili wilayani humo majira ya jioni kwajili ya kufuatilia mgogoro wa kimpaka wa ardhi kati ya Tanapa na wakazi wa vijiji vilivyopo jirani na hifadhi ya taifa ya Ruaha katika eneo la Ihefu.

Baada ya kufika wilayani hapa ilikiwa Nyalandu akutane kwanza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya wilaya ya Chama Cha Mapinduzi ili kupata maoni yao kabla ya kukutana na uongozi wa serikali wilaya na kisha wananchi katika kata ya Ubaruku.

Lakini kutokana na waziri kufika kwa kuchelewa alilazimika kushauriana na viongozi wa chama kuahirisha vikao hivyo na badala yake vifanyike kesho yake ili kutoa fursa kwa makundi yote kushirika katika utatuzi wa mgogoro uliodumu kwa takribani miaka saba sasa.

Hata hivyo mbele ya kiongozi huyo,Mbunge Kirufi na mwenyekiti wake wa Chama walishindwa kuficha utofauti walionao na badala yake walianza kurushiana maneno makali(matusi) mbele yake huku kila mmoja akionesha kuwa mbabe zaidi ya mwenzie.

Chanzo cha habari cha uhakika kilichokuwepo eneo la tukio kilieleza kuwa viongozi hao waliendelea kurushiana matusi hadi pale Nyalandu alipoamua kuingilia kati kuwasuluhisha na baadaye yeye kuamua kwenda jijini Mbeya kupumzika kabla ya kurejea wilayani hapa kesho yake.

Uthibitisho wa tukio hilo ulibainika katika ukumbi wa CCM wilaya,wakati Nyarando alipowataka wawili hao wapeane mkono kuashiria hali ya jana yake imekwisha mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya huku pia akiwasisitiza viongozi hao kuwa na umoja katika kupigania maslahi ya chama na wananchi wanaowaongoza.

Hata hivyo Mbunge Kilufi katika kuonesha kuwa bifu halijakwisha licha ya kukubali kupeana mikono ukumbini,alipopanda jukwaani mbele ya wananchi wa kata ya Ubaruku alionesha kuendelea kuwa na kinyongo mbelea ya baadhi ya viongozi wa CCM wilaya japok hakuwataja majina.

“Hata kama unamchukia Kilufi,endelea kumchukia,lakini katika suala la mpaka kati ya Tanapa na wananchi naomba tuungane kuwatetea watu wetu” yalikuwa maneno ya Kilufi jukwaani.

Baadhi ya wakazi wilayani hapa wanasema ugomvi baina ya wawili hao unatokana na kuwa ufuasi katika makundi mawili tofauti ya watu wanaowania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao ambao mbunge anatajwa kuwa katika kundi la waziri wa zamani Edward Lowasa.

Lakini wapo pia wanaosema mwenyekiti wa chama wilaya amekuwa akipingana na mbunge huyo katika suala la mpaka kati ya Tanapa na vijiji vya jirani kwa kile wanachoeleza kuwa amekula rushwa kutoka Tanapa tuhuma alizozitaja pia mwenyekiti huyo alipozungumzia suala la mpaka akiwa ukumbini.

“Mh.waziri suala hili la mpaka wengine hata limetupaka matope,wapo wanaosema tumeingizwa mifukoni mwa Tanapa.Wanasema Tanapa wametununua kwa kutupa fedha ili tusiwatetee wananchi.Tunaomba tulipatie ufumbuzi ili mambo haya yasiendelee” alisema Mwangomo alipokuwa ukumbini.

Monday, April 20, 2015

MOTO WATEKETEZA MADUKA TUNDUMA


Wananchi wakijaribu kuokoa mali zilizopo katika maduka hayo.Picha na Saimen Mgalula


Kikosi cha Zimamoto kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo kuuzima moto huo ambao umetekteza maduka zaidi ya Manne katika eneo hilo Mtaa wa Unyamwanga Kisimani mjini Tunduma.
 

MOTO mkubwa umeteketeza maduka zaidi ya Manne    katika mtaa wa Unyamwanga Kisimani Mjini Tunduma  mkoani Mbeya  April 19 mwaka huu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa moto huo ulitokea saa 2   usiku mtaa wa unyamwanga ambapo maduka hayo yaliyoteketea yalikuwa katika  jengo moja linalomilikiwa Albart Ndembwike mkazi wa Tunduma .
Kamanda Msangi amesema  moto huo ulitokea katika moja ya duka kati ya hayo Manne yaliteketea kwa moto ambapo chanzo chake bado hakijafahamika mara moja ambapo uchunguzi wa tukio bado unaendelea .

Amesema changamoto kubwa iliyopo katika eneo hilo LA Mji wa Tunduma ni ukosefu wa gari la zima moto hivyo katika tukio la jana walilazimika kuomba msaada kwa majirani zao Zambia ambao walifika mara moja na kuuzima moto huo kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.

Amesema changamoto hiyo inatokana na wananchi wenyewe kufanya uhalibifu katika gari la zima moto lililokuwepo katika mjini huo ambalo lilihalibiwa vibaya kwa kutupiwa mawe kipindi nyuma ambalo kwa sasa lipo katika matengenezo.

Aidha jeshi la polisi limelaani mtindo unaoota mizizi hivi sasa wa wananchi kujichukulia sheria mkononi kwani kwa kufanya shambulio kwa kikosi cha zima moto mara kinapo wasili katika eneo la tukio.

Amesema mashambulio ya aina hiyo yamekuwa yakisababisha hasara ikiwa ni pamoja na kuvunjwa vioo vya gari, kupotea kwa vitendea kazi pamoja na baadhi ya askari wa zimamoto kujeruhiwa kitendo ambacho kinavunja moyo kwa askari hao.

Aidha mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza kuwa moto huo ulishika kasi kwa haraka kutokana na hali ya hewa kuwa ya upepo mkali licha ya juhudi za wananchi kuuzima lakini uliwashinda nguvui hadi pale kikosi cha zima moto kutoka nchini Zambia kilipo fika na kuuzima moto huo.