Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, April 10, 2015

SANGOMA AFA AKICHIMBA MIZIZI KICHAKANI



MKAZI wa kijiji cha Ikukwa wilayani Chunya Wahama Wajoga anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 85-90 amekutwa amefariki dunia porini alipokuwa akichimba mizizi kwaajili ya dawa za kienyeji.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji cha Ikukwa, Josta Jiwili mwili wa Wajoga anayedaiwa kuwa alikuwa mganga wa jadi ulikutwa kichakani juzi na pembeni kukiwa na kipande cha nondo alichokuwa akitumia kuchimbia mizizi.

Mwenyekiti huyo alisema inaonekana mpaka anakutwa na mauti tayari alikuwa amekwishachimba baadhi ya m,izizi kwani ilikutwa katika begi dogo alilokuwa nalo.


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema siku moja kabla ya kifo chake walikuwa pamoja na Wajoga wakinywa pombe za kienyeji,na kucheza
muziki katika kilabu cha wazenga,akiwa mzima wa afya njema hivyo kushangazwa na kifo chake.


Kwa upande wake ndugu wa marehemu walisema kifo hicho kimewashangaza sana kwani marehemu hakuwahi kusumbuliwa na tatizo lolote hadi mauti yanamkumba.


Nao Machifu wa kijiji cha Ikukwa walisema kuwa kifo hicho kinadhaniwa
kuhusishwa na imani za kishirikina kutokana na  marehemu kujihusisha na kuagua wagonjwa wanaodhaniwa kulogwa.
 

Mmoja wa machifu hao,Chifu Mwavamba alisema imekuwa ni
kawaida kwa waganga wa kienyeji kupimwa nguvu na watu wanaodhaniwa ni wachawi kwa kuwa inasadikika hawapendezwi na uwepo wa watu wanaotoa tiba kwa wanaologwa na wachawi.

No comments:

Post a Comment