Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, April 11, 2015

UVCCM MBEYA YASISITIZA WAHITIMU KUENDELEZA VIPAJI ILI VIWAPE AJIRA


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna Mwenye suti Nyeusi akiwa katika  mahafali ya kidini ya kasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani Mbeya.
Burudani ikitolewa kwa wanafunzi wa shule hiyo wakati wa  mahafali ya kidini ya kasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill.
Wahitimu wakiwa wamepoz katika eneo lao maalumu wakitafakari na kubadilishana mawazo juu ya uwepo wao shuleni hapo






Burudani ikitolewa na baadhi ya wanafunzi katika   mahafali ya kidini ya Ukwasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani Mbeya.Vijana hawa wanauwezo mkubwa wa kutunga mashairi na kuimba pasipo hata uwepo wa vyombo vya muziki.
Ubunifu mwingine uliooneshwa na baadhi ya wanafunzi wanaobaki shuleni hapo ni kucheza muziki wa injili





Sasa ni wakati muafaka wa kukata keki iliyoandaliwa na wahitimu
Mezi wa kiroho wa wahitimu akimlisha keki mgeni rasmi Aman Kajuna kwenye sherehe hiyo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna akizungumza katika  kwenye mahafali ya kidini ya Ukwasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita.
Aman Kajuna akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake kwenye mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa shule.


Viongozi wa kidini wakifanya maombi maalumu kuwaombea wahitimu

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna akigawa vyeti kwa hatimu.


                                           HABARI KAMILI

WAHITIMU katika shule za sekondari nchini wameshauriwa kuviendeleza vipaji vya sanaa wanavyoonesha kwenye sherehe mbalimbali wakiwa shuleni wakitambua kuwa vina mchango mkubwa katika kuwapa ajira maishani mwao.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna alitoa ushauri huo kwenye mahafali ya kidini ya Ukwasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa.



Kajuna alitoa ushauri huo baada ya kukunwa na vipaji mbalimbali vya sanaa walivyoonesha wahitimu na wanafunzi wanaobaki kama ilivyowafurahisha pia waalikwa wengine ukumbini hapo.



Miongoni mwa vipaji vilivyooneshwa na wanafunzi wa shule hiyo ni pamoja na uimbaji wa nyimbo za injili uliodhihirisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi hao wanao uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba tenzi na mashairi ya nyimbo mbalimbali.



Sanaa nyingine ni uchezaji wa aina mbalimbali wa nyimbo za injili,Uongozaji wa sherehe,uchekeshaji na upigaji wa vyombo vya muziki zikiwemo ngoma na kinanda.



Kajuna alisema si wakati tena kwa wanafunzi kuacha sanaa hizo zikaishia mashuleni,badala yake wahakikishe wanaziendeleza hata wafikapo katika vyuo na baadaye wazifanyie kazi katika kuwapa ajira badala ya kubaki wakitegemea kuajiriwa pekee.



“Kama mna vipaji kama mlivyoonesha hapa sidhani kama mnapaswa kuwa miongoni mwa watanzania ambao katika miaka kadhaa ijayo watatakiwa watembee kutwa nzima na bahasha za kaki wakipita kila ofisi kuomba kazi.Unatembea mchana kutwa mpaka bahasha inachanika upande wa juu.Uliiweka kiganjani baadae unaamua uiweke kwapani”



“Tumieni vipaji vya sanaa mliyoonesha hapa kujiajiri katika miaka hiyo.Huu ni utajiri tosha unaoweza kuwapa maisha bora tena pasipo kutumia gharama kubwa kama ilivyo kwa wengine.Mmeonesha mnaweza” alisisitiza mwenyekiti huyo wa uvccm mkoa.



Hata hivyo Kajuna alisema mchango wa wazazi,walezi na wadau wengie ndiyo msingi mkubwa katika kuendeleza vipaji vya sanaa walivyo navyo wanafunzi hivyo akawaasa kutambua vipaji wal;ivyonavyo watoto wao.


No comments:

Post a Comment