https://www.facebook.com/100001526491541/videos/163778579924492/
Wednesday, June 28, 2023
Thursday, June 15, 2023
Wednesday, June 14, 2023
SINGIDA BIG STARS YAPIGWA MNADA
MICHUANO TULIA TRUST BODABODA CUP 2023 YAZINDULIWA RASMI.
Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa akisalimiana na wachezaji wa timu za Madereva Bodaboda za Uyole na Stendi kuu kwenye uzinduzi wa Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.
Na Joachim Nyambo,
Mbeya.
MEYA wa jiji la Mbeya
Dormohamed Issa amezindua rasmi michuano ya Tulia Trust Bodaboda Cup 2023
yatakayoshirikisha timu nane kutoka kanda za madereva bodaboda zilizogawanywa
kwenye makundi mawili ya A na B.
Michuano hiyo imerejea
tena baada ya kusitishwa kwa misimu miwili mfululizo ambapo kwa mara ya kwanza
yalifanyika 2019 lakini kwa miaka iliyofuata haikufanyika kutokana na
changamoto mbalimbali ikiwemo mlipuko wa Covid-19
Kwa upande wa kundi A timu
zinazoshiriki michuano hiyo ni za madereva bodaboda kutoka kanda za Iyunga,
Stendi Kuu, Soweto na Kabwe wakati kundi B zipo timu za kanda za Mafiati, Sae,
Uyole na Kadege.
Akizindua michuano hiyo
katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge, Meya wa jiji la Mbeya Meya Issa ameipongeza
Taasisi ya Tulia Trust inayoyaandaa akisema yana mchango mkubwa katika kuibua
na kukuza vipaji vya vijana.
Amewasihi madereva
bodaboda kutumia michuano hiyo situ kwa kuibua vipaji vyao bali pia kuimarisha
afya zao hivyo kuwataka kuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote yatakapokuwa
yanaendelea.
“Mpira unaanza kucheza
chini lakini haujui huko mbele utafika wapi…naamini kabisa kuna wachezaji
miongoni mwenu mkionyesha nidhamu mkazingatia yale mnayofundishwa na walimu
kuyafuata ipo siku mtafika mbali.”
“Mpira ni nidhamu..na
ukitaka kufanikisha katika jambo lolote weka nidhamu mbele..ukiamua kuwa padre
weka nidhamu mbele, ukitaka kuwa shekh weka nidhamu mbele na hata ukitaka kuwa
kiongozi wajali watu wako.” Amesisitiza Issa.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Kamati ya mashindano ya Chama cha soka Mbeya mjini(Mufa), Ramadhan Nyambala amesema
kutokana na ari ya mpira wa miguu katika mkoa wa Mbeya ni muhimu wadau wengi
kuzidi kujitokeza kuandaa mashindano mbalimbali.
Amesema kuandaliwa kwa
mashindano kama ya Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 ni sehemu ya mikakati muhimu
na inayotarajiwa kwenye kuibua na kukuza vipaji vya vijana.
Afisa Habari na
Mawasiliano wa Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema baada ya michuano hiyo
kufanyika kwa mara ya kwanza 2019 iaka miwili mfululizo ilisimama kutokana na
changamoto mbalimbali zilizoibuka ikiwemo cha mlipuko wa ugojwa wa corona.
Mwakanolo amesema michuano hiyo itakayokuwa ikifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge na Magereza Mbeya yanatarajia kufikia tamati mwezi ujao huku akisema zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu zitatangazwa hivi karibuni.
Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa akisalimiana na waamuzi wa mchezo kati ya timu za Madereva Bodaboda za Uyole na Stendi kuu kwenye uzinduzi wa Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.