Tuesday, December 30, 2014
Saturday, December 27, 2014
ZIARA YA DK.MWAKYEMBE NA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU MKOANI MBEYA SIKU YA 1
Waziri wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe
akitoa ufafanuazi kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu juu
ya namna kiwanda cha kusaga kokoto cha Kongolo kilichopo Mswiswi wilayani
Mbarali kinachomilikiwa na Shirika la reli la Tazara kinavyofanya kazi ya
uzalishaji wa kokoto kwaajili ya kuimarishia miundombinu ya reli.Katikati ni
mwenyekiti wa kamati ya bunge Prof.Juma Kapuya akifuatiwa na kaimu meneja wa
mgodi kokoto Juma Mizambwa
Msafara Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu na waziri wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe ukiangalia namna kokoto zinavyozalishwa katika mgodi wa kuzalishia kokoto wa Kongolo uliopo katika kijiji cha Mswiswi wilayani Mbarali.
Hapa wajumbe wa kamati walishauri uongizi wa kmgodi kona uwezekano wa kukopa fedha ili kuboresha mitambo na kuongeza uzalishaji wa kokoto ili kutengeneza faida zaidi ya sasa.
Baada ya kutoka katika mgodi wa kusaga kokoto,safari ikaendelea mpaka kilipo kiwanda cha kutengenezea mataluma ya Reli kwa kutumia saruji maalumu badala ya chuma.
Kaimu meneja wa mgodi kokoto Juma Mizambwa akielezea namna mataluma ya reli yanavyotengenezwa kwa kutumia saruji na si chuma
Mataluma ya Reli yaliyotengenezwa kwa kutumia saruji maalumu yakiendelea kukaushwa kabla ya kuondolewa kwenye mtambo wa kutengenezea.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiangalia mataluma ya reri yaliyotengenezwa kwa kutumia saruji ambayo ni mbadala wa mataluma ya chuma hali inayopunguza gharama za ununuzi na usafirishaji wa mataluma ya chuma kutoka nje ya nchi.Mataluma haya ya saruji yanazalishwa na Tazara katika kiwanda kilichopo Mswiswi wilayani Mbarali.
Ziara ikaendelea kurejea jijini Mbeya hadi ilipo karakana ya Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) maeneo ya Iyunga kama inavyoonyesha hapa chini.
Hapa wabunge walielezwa namna Tazara mkoa wa Tanzania ilivyodhamiria kufufua vichwa vya treni vilivyoharibika kutokana na ajali mbalimbali.Usishangae kusikia mkoa wa Tanzania,Tazara inaendeshwa katika mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Tanzania na mkoa wa Zambia.
Wabunge walishauri kuangaliwa upya kwa sheria ya uanzishwaji wa Tazara ili kupunguza migongano ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikiibuka na kusababisha utendaji wa shirika hilo kuendelea kuzorota,hivyo kulifanya lisiwe na tija katika maendeleo ya uchumi wa taifa.Wamunge walisema ni muhimu sheria ikabadilishwa ili bajeti ya Tazara mkoa wa Tanzania iwe inapelekwa katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Hiki ni moja kati ya vichwa vya treni vitakavyojengwa upya na Tazara.
MATUKIO YA SIKU YA PILI YA ZIARA YATAKUJIA KESHO AKSANTE KWA KUWA NASI

Wednesday, December 24, 2014
MERRY CHRISTMASS AND HAPPY NEW YEAR
Kwa niaba ya jopo zima la blogu ya Lyamba Lya Mfipa
inayopatikana kwa anuani ya www.jodanyp.blogspot.com, mhariri mkuu wa LYAMBA Lya Mfipa Bw.Joachim
Nyambo anawatakia heri ya Krismasi na Mwaka mpya 2015.Tunatambua mchango wadau
wetu na tunawaahidi kuongeza ubora wa huduma zetu za uhabarishaji.
J.D.Nyambo.
Mhariri mkuu Lyamba Lya Mfipa
Tuesday, December 16, 2014
TANESCO YASEMA MGAWO WA UMEME KUBAKI HISTORIA NCHINI
Mkurugenzi
mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba akitoa taarifa yaa mikakati ya shirika hilo ili kukomesha tatizo la mgawo wa umeme nchini
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla akizungumza na maafisa wa Tanesco kabla ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo.
Afisa Mwandamizi wa Tanesco kanda ya Nyanda za juu kusini Salome Kondola akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya mkuu wa wilaya
Maafisa wa Tanesco wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla baada ya kiongozi huyo kufungua mkutano wa baraza lao.
HABARI KAMILI
SHIRIKA
la Ugavi la Umeme nchini(Tanesco) limesema ifikapo mwishoni mwa mwaka 2016
Tanzania suala la mgawo wa umeme litabaki kuwa historia.
Uhakika
huo unakuja kufuatia mikakati ya utekelezaji wa miradi ikiwemo Kinyerezi namba
moja wa megawati 150 ambao hadi sasa asilimia 90 ya utekelezaji wake
umekamilika.
Upo
pia mradi wa kinyerezi namba mbili wa megawati 240 ambao serikali iko kwenye
hatua za mwisho za maelewano ya kifedha baina ya wizara ya fedha,benki ya
Japani na benki ya maendeleo ya Afrika kusini ambapo ujenzi wa mradi huo
unatarajiwa kuanza mwakani.
Mkurugenzi
mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba ameyasema hayo wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa Baraza kuu la 45 la wafanyakazi wa Tanesco linalofanyika jijini
Mbeya.
Mhandisi
Mramba amesema miradi ya kinyerezi namba tatu na nne imeanza kwa ubia kwa makampuni
mawili ya kichina na utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwakani kama ilivyo
kwa kinyerezi namba mbili.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla amewataka watoa huduma
kutoka shirika hilo kuwa na lugha zenye kumwelewesha mteja na si kujibu hovyo
hovyo.
Dk.Sigalla amesema
majibu mabovu ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya watendaji wa shirika hilo
yamekuwa yakisababisha serikali kulaumiwa na kuonekana haifai kwakuwa haiwathamini
wananchi katika kutoa huduma za nishati ya umeme.
Amesema
ni vema wataalamu hao wakawa na lugha zenye ukweli kwa wateja badala ya lugha
za kuwalaghai na kuwadanganya na mwisho wa siku mteja anakuja kubaini ukweli
uliopo na kulichukia shirika na serikali.
Monday, December 15, 2014
MWANACHUO TIA ADAIWA KUTUPA KICHANGA DAMPO
Maiti ya mtoto mchanga ikiwa imetelekezwa kama ilivyokutwa na wakazi wa eneo la Airpot jijini Mbeya(Picha kwa hisani ya mmoja wa wakazi wa eneo hilo)
MWANAMKE asiyefahamika ametupa mtoto mchanga katika Dampo
la taka lililopo katika eneo la Airpot jijini Mbeya jirani na kilipo chuo cha
uhasibu(TIA) tawi la Mbeya.
Wakazi wa maeneo ya jirani na dampo hilo wanasema
waliikuta maiti ya kichanga hicho ikiwa imetelekezwa hapo lakini inasadikiwa
kuwa kabla ya kutupwa mtoto huyo alikuwa hai.
Hili si tukio la kwanza kwa maiti za vichanga na pia
vichanga vilivyo hai kukutwa vimetelekezwa kwenye dampo hili.Baadhi ya wakazi
wa maeneo ya jirani na dampo hili wanahusisha matukio ya utupaji watoto
wachanga na pia maiti za watoto hao na wanafunzi wa chuo cha TIA.
“Hii si mara ya kwanza kukuta maiti ya kichanga
hapa.mara kwa mara tumekuwa tukiokota.Wengi wetu tunaamini wanaofanya ukatili
huu ni wanafunzi wanaosoma humo ndani TIA.Wanaagopa kulea ndiyo sababu wanatupa
vichanga namna hii” alisema mmoja wa wakazi wa maeneo hayo aliyeomba jina lake kutoandikwa katika Lyamba Lya Mfipa.
MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI MKOANI MBEYA
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Makunguru jijini Mbeya wakiwa katika foleni ya kuelekea kupiga kura.
HABARI YA MATOKEO YA AWALI
MATOKEO
ya awali yaliyopatikana mkoani Mbeya
katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaonesha Chama Cha Mapinduzi(CCM)
kuongoza katika maeneo mengi kikifuatiwa
na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mpaka
tunakwenda mitamboni jioni hii matokeo yalipatikana kwenye vitongoji 2047 kati
ya 2567, vijiji 606 kati ya 771 na mitaa 252.
Kwa
upande vijiji,Wilaya ya Chunya yenye vijiji 86 yalikuwa yamepatikana matokeo ya
vijiji 74, ambapo kati ya vijiji
hivyo,CCM ilikuwa imeshinda vijiji 67 na Chadema vijiji saba.
Wilaya
ya Ileje yenye jumla ya vijiji 71 ambapo matokeo yalikuwa yamepatikana ya
vijiji 32 CCM ilikuwa imeshinda vijiji 23 na Chadema vijiji 9.
Kwa
wilaya ya Kyela yenye jumla ya vijiji 93 ambayo matokeo ya vijiji vyote
yalikuwa yamepatikana CCM imeshinda vijiji 79 na Chadema vijiji 13 huku kijiji
kimoja uchaguzi ukiwa haukufanyika.
Wilayani
Mbarali kuliko na jumla ya vijiji 102, matokeo yalikuwa yamepatikana ya Vijiji
97 ambapo CCM ilikuwa imeshinda katika
vijiji 81 na Chadema vijiji 16 na vijiji vitano yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya
ya Mbozi yenye vijiji 125 ambapo matokeo ya vijiji 92 yalikuwa yamepatikana CCM
ilikuwa imeshinda katika vijiji 84,Chadema vijiji 8 na vijiji 33 yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya
ya Rungwe yenye vijiji155,matokeo ya vijiji 150 yalikuwa yamepatikana,CCM
ilishinda vijiji 127,Chadema vijiji 22,CUF kijiji kimoja na vijiji vitano
matokeo yalikuwa yanasubiriwa.
Wilaya
ya Momba ina vijiji 72 kati ya hivyo vijiji 67 yalikuwa yamepatikana,CCM
ilikuwa imeshinda katika vijiji 43,Chadema vijiji 24 na vijiji vitano yalikuwa
yanasubiriwa.
Kwa
upande wa Mitaa Mbeya mjini kuliko na mitaa 181,CCM imeshinda mitaa 106,Chadema
mitaa 71 na Nccr Mageuzi mtaa mmoja wakati katika mji mdogo wa Tunduma wilayani
Momba ulio na mitaa 71 Chadema iliibuka kidedea katika mitaa 46 na CCM
ikaambulia mitaa 25.
Kwa
upande wa Vitongoji,Chunya yenye vitongoji 438 ambapo matokeo ya vitongoji 288
yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 270 na Chadema vitongoji
18.
Kyela
yenye vitongoji 469 CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 377 na Chadema vitongoji 88
huku vitongoji vinne uchaguzi ukiwa unapaswa kurudiwa.
Wilaya
ya Mbozi yenye jumla ya vitongoji 664 ambayo matokeo ya vitongoji 414 yalikuwa
yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 359,Chadema vitongoji 55 na
matokeo ya vitongoji 250 yalikuwa yanasubiriwa.
Wilaya
ya Rungwe yenye jumla ya vitongoji 694,matokeo ya vitongoji 634 yalikuwa
yamepatikana na CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 557,Chadema vitongoji 110,Cuf
vitongoji viwili na TLP kitongoji kimoja na vitongoji 60 yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya
ya Momba ina jumla ya vitongoji 302 kati ya hivyo vitongoji 242 matokeo
yalikuwa yamepatikana ambapo CCM ilikuwa imeshinda 189,Chadema 53 na vitongoji
60 vilikuwa bado matokeo yakisubiriwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)