Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, July 30, 2013

MTOTO AUAWA KWA KUCHINJWA SHINGO BAADA YA KUBAKWA

MTOTO wa miaka sita amebakwa na kisha kuuawa kikatili kwa kukatwa shingo na mkono kwa panga na kijana mwenye umri wa miaka 14. Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 29 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Ijoka kata ya Mpombo wilayani Rungwe wilaya ambayo inashiriki katika kuendesha mradi wa majaribio wa kupinga ukatili wa jinsia na watoto(GBV) unaoendeshwa na shirika la Watereed kwa ufadhili wa watu wa marekani kupitia mfuko wa rais wan chi hiyo. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athumani alimtaja mtoto aliyetendewa ukatili huo kuwa ni Janeth Mwailima mkazi wa Ijoka ambapo kabla ya kuawa alibakwa. Alimtaja mtuhumiwa wa vitendo hivyo vya kinyama kuwa Narbeth Haule anayedaiwa kuwa mkulima na mkazi wa kijiji cha Ijoka hali inayodhihirisha alitenda unyama huo pasipokujali udugu wa kuheshimiana na kusaidiana katika mambo mbalimbali ambao wamekuwa nao wakazi wa vijiji vya wilayani Rungwe na mkoa wa Mbeya kwa ujumla. Kamanda Athuman alisema awali baada ya kubakwa mtoto Janeth aliapa kwenda kuwaambia wazazi wake akiwemo baba yake juu ya unyama aliotendewa na ndipo kijana huyo aliamua kwenda nyumbani kwao kuchukua upanga na kuja kumkata mtoto huyo shingoni na mkono wake wa kulia lengo likiwa ni kupoteza ushahidi wa kubaka. Alisema tayari jeshi hilo linamshikilia kijana huyo na kuwa taratibi mbalimbali za kisheria zinaandaliwa ili aweze kufikishwa mahakamani na mkono wa sheria kuchukua mkondo wake kwa roho ya unkatili na unyama aliyo nayo dhidi ya binadamu wenzake. “Lengo lake ilikuwa kupoteza ushahidi kwakuwa mtoto aliyembaka alitishia kwenda kuwaeleza wazazi wake juu ya aliyotendewa na mkazi mwenzao.Lakini badala ya kupoteza ushahidi amezidi kujiweka matatani” alisema kamanda.

Monday, July 29, 2013

JIWE MBUJI NI KIVUTIO KINGINE WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA

MOJA KATI YA SIFA ZA JIWE HILI LILILOPOKATIKA TARAFA YA MBUJI NI PAMOJA NA WAKAZI WA MAENEO YA JIRANI KULITUMIA KAMA ENEO LA KUFANYIA MATAMBIKO MBALIMBALI.

JE WAJUA?

MENDE ANAWEZA KUISHI WIKI KADHAA BAADA YA KUKATWA KICHWA?

Thursday, July 25, 2013

SIKU YA MASHUJAA MBEYA YAFANA

Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro ambaye pia ni mwenyekiti wa wakuu wa wilaya za mkoa huo ndiye aliongoza maadhimisho hayo akimwakilisha mkuu wa mkoa Abbas Kandoro aliyeko likizo.Picha ya Kwanza Kinawiro akisalimiana na viongozi mbalimbali wa vikosi vya ulinzi na usalama.PATA PICHA ZAIDI HAPA CHINIWANAHABARI PENDO FUNDISHA(KULIA) NA AMANI MBILO WAKIWA WAMESHIKANA MIKONO KWA HOFU YA KISHINDO CHA MIZINGA MITATU ILIYOPIGWA IKIWA NI ISHARA YA KUWAKUMBUKA ASKARI MASHUJAA WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE VITA KUU YA PILI YA DUNIABAADA YA KUPIGWA MZINGA WA KWANZA HALI ILIKUWA NAMNA HII JAPO HAKUNA MTU ALIYERIPOTIWA KUPATA MAJERAHA YA AINA YOYOTE YATOKANAYO NA MSHITU JAPO WAPO WACHACHE WALIOTIMUA MBIO KUKIMBIA ENEO LA TUKIO

Wednesday, July 24, 2013

ZIARA YA WANAHABARI KUTEMBELEA KIWANDA CHA BIA CHA TBL MBEYA ILIVYOFANA

HAPA WAANDISHI WA HABARI WAKIELEKEZWA NAMNA UJI WA KUTENGENEZEA BIA UNAVYOPIKWA IKIWA NI HATUA YA MWANZONI KABLA YA KUINGIA KWENYE HATUA NYINGINE.HAPA WAKIELEKEZWA NAMNA BIA INAVYOKAMULIWA NA KUTENGANISHA KATI YA MAJI NA MACHICHA TAYARI KWA KUINGIA KATIKA HATUA NYINGINEBAADA YA KUTEMBELEA MITAMBO MBALIMBALI NDANI YA KIWANDA HICHO CHA KWANZA KWA UKUBWA BARANI AFRIKA UKAFIKA MUDA WA SHINDANO LA KUONJA BIA KAMA UNAVYOONA HAPA CHINI WANAHABARI MBALIMBALI WAKISHIRIKI SHINDANO HILO NA MWISHO WAKAPATIKANA WASHINDI WALIOPEWA ZAWADIKATIKA SHINDANO LA KUONJA BIA WASHINDI WA KWANZA WALIPATIKANA JOSEPH MWAISANGO NA EMANUELI MADAFA WALIOPATA KATONI MBILI MBILI ZA BIA KILA MMOJA HUKU NAFASI YA PILI IKIENDA KWA JOACHIM NYAMBO NA KENETH NGELESI WALIOZAWADIWA KATONI MOJA MOJA.