Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, July 1, 2013

WATATU WAUAWA KIKATILI MBEYA

WATU watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti yaliyotokea Juni 30 mwaka huu mkoani Mbeya,yakiwemo mawili ya watu kuuawa na watu wasiojulikana. Mmoja wa waliouawa ni mkazi wa kijiji cha Iyendwa wilayani Momba Geofray Simpungwe(45) aliyekutwa porini ametundikwa mtini kwa kamba mithiri ya mtu aliyejinyonga huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kupigwa. Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Barakael Masaki amesema mwili wa Simpungwe umekutwa majira ya saa 11 jioni umbali wa kilometa mbili kutoka eneo la makazi huku ikidaiwa kuwa marehemu alikuwa akituhumiwa kwa uchawi kijijini hapo. Masaki amesema tukio la pili ni la mauaji ya mkazi wa kijiji cha Nsongwi Mandanji aliyefahamika kwa jina la Ame Dundai(25) aliyekutwa majira ya saa 12 asubuhi kijijini hapo akiwa ameuawa kwa kuchomwa moto kwa kutumia gurudumu la gari huku ikidaiwa kuwa ni mwizi. Tukio la tatu ni ajali ya gari aina ya Noah isiyoifahamika namba wala dereva wake iliyoacha njia na kumgonga mtembea kwa miguu Helena Ukupama(68) mkazi wa Garijembe wilayani Mbeya na kusababisha kifo chake papo hapo majira ya saa 1:30 usiku kijijini hapo. Kaimu Kamanda huyo amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa matukio yote matatu,sambamba na kuwasaka waliosababisha vifo hivyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

No comments:

Post a Comment