Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, February 28, 2014

KAIMU AFISA MTENDAJI WA KIJIJI AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI

MNAMO TAREHE 27.02.2014 MAJIRA YA SAA 01:55HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. TITO HANKUGWE (45) KAIMU VEO WA KIJIJI CHA SHASYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI WAKATI ANATOA MSAADA NYUMBANI KWA FURAHA HANKUGWE AMBAYE ALIVAMIWA NA KUNDI LA WATU NANE NA KUBOMOLEWA NYUMBA YAKE PAMOJA NA KAKA YAKE SIKUJUA HANKUGWE TAREHE 26.02.2014 MAJIRA YA SAA 21:45HRS KATIKA KIJIJI CHA SHASYA, KATA YA HALUNGU, TARAFA YA ITAKA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI WA SOLA NA INVETA AMBAPO FURAHA HANKUGWE ALITUHUMIWA KUIBA NYUMBANI KWA MAPINDUZI MAGWAZA MKAZI WA KIJIJI CHA SHASYA. WATUHUMIWA HAO AMBAO WOTE WANAFAHAMIKA WAKIONGOZWA NA AMANI MAGWAZA – MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA NAMKWENDE, WENGINE NI MASHAKA BOKO, GIVEN MYOMBE, MAWAZO MAGWAZA, YOHANA MAGWAZA, TULINAO NZOWA, KENETH NGOYA, SIKUJUA NZOWA AMBAO WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA HAO ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki

Wednesday, February 26, 2014

ZIARA YA RC KANDORO WILAYANI MBARALI

Ziara ilianzia hukoo kata ya Madibira.Kituo cha kwanza kilikuwa shule ya Sekondari Madibira na mkuu wa mkoa akapokelewa kwa kuvishwa skafu na vijana wa Skauti Mkuu wa mkoa akiwa shuleni hapa aliweza kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tenki la kuhifadhia maji la chini ya ardhi.Aliweza pia kukagua jengo la maabara kwaajili ya masomo ya sayansi,nyumba ya mwalimu iliyojengwa kisasa na choo kilichojengwa pia kisaa kwaajili ya matumizi ya wanafunzi. Kandoro pia alitembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mkunywa.Hapa alikuta hakuna jambo lolote la maana lililokwisha fanyika licha ya mkandarasi kampuni ya JECCS CONSTRUCTION AND SUPPLIERS ya Dar es salaam kulamba zaidi ya milioni 100.Inabainishwa kuwa wafanyakazi wa kampuni hii wamekuwa wakishinda wakilewa pombe eneo la mradi badala ya kufanya kazi hivyo mradi kuendelea kusuasua.Mkuu wa mkoa alionesha kukasirishwa na hatua hiyo ya mradi na kuamuru mkandarasi mshauri kuona uwezekano wa kuishauri halmashauri kuvunja mkataba iwapo mkandarasi ataendelea kusuasua Ziara ikaendelea kwa kukagua miradi mbalimbali na kumalizika siku ya pili katika mradi wa maji wa Igurusi kwa mkuu wa mkoa kukagua Ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji

POWERTILLA IKIWA IMEBEBA MWILI WA MAREHEMU KUELEKEA ENEO LA MAZISHI KAMA ILIVYOKUTWA NA Lyamba Lya Mfipa CHIMALA WILAYANI MBARALI

Wednesday, February 19, 2014

BIG RESULTS NOW(BRN) KATIKA KILIMO CHUNYA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza jambo mara baada ya kukagua shamba la mahindi la shule ya sekondari ya Kanga wilayani Chunya.Shamba hili limekuziwa kwa mbolea aina ya minjingu ambapo Kandoro aliagiza wakazi wa maeneo ya jirani wafike hapo kujifunza namna mbolea hiyo inavyofaa kwa mazao.

Sunday, February 16, 2014

SIMBA YAIPIKU YANGA MAPATO NYUMBANI KWA MBEYA CITY

MCHEZO wa Mbeya City na Simba uliochezwa jumamosi katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya umeingiza jumla ya shilingi 125 milioni. Akitangaza mapatona ya kiingilio cha mchezo huo na mgawanyo wake,mwenyekiti wa Chama cha soka mkoani Mbeya(MREFA) Eliasi Mwanjala alisema kiasi hicho cha pesa kimetokana na watazamaji 21,000 walioingia kushuhudia mchezo huo kwa kiingilio sha shilingi 5000 kila mmoja. Kwa mapato hayo,mchezo wa Mbeya City na Simba umeingiza kiasi kikubwa cha fedha ikilinganishwa na kile kilichovunwa wakati Mbeya City walipochezaa na timu ya Yanga katika uwanja huo ambapo zilipatikanaN shilingi milioni 100 kiingilio kikiwa ni shilingi 5000 pia kwa kila mtazamaji aliyeingia uwanjani. Akizungumzia mgawo wa mapato ya mchezo huo,Mwanjala alisema shilingi 16,016,000 sawa na asilimia 18 ya fedha zote zilitolewa kwaajili ya kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT na kiasi kilichosalia kugawanywa kwa kila timu kupata shilingi 25,316000 sawa na asilimia 29.5. Alisema shilingi 12,872,000 sawa na asilimia 15 zilikwenda kwa wamiliki wa uwanja,gharama za mechi shilingi 7,723,000 sawa na asilimia tisa,kamati ya ligi 7,723,000 sawa na asilimia tisa pia,mfuko wa maendeleo ya soka 3,861,000 huku Chama cha soka mkoa kikiambulia shilingi 3,003,000. Wakati Mrefa ikitangaza mapato hayo,kwa upande mwingine wadau wa soka mkoani hapa wamelalamikia ubadhirifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya viongozi wa kutumia vikundi vya watu kuuza tiketi bandia na wao kuzipitisha kama tiketi halali wawapo milangoni. Meneja wa uwanja wa Sokoine Modesrtus Mwaluka hakusita kulitupia lawama shirikisho la soka nchini (TFF) akisema lina baadhi ya watendaji wabadhirifu ambao wamekuwa wakitumia mechi kubwa kujinufaisha kwa kuwapa jukumu la kuuza tiketi bandia vijana wanaotoka nao Dra es salaam maarufu kama makomandoo kuja nao mikoani. Mwaluka alitolea mfano katika mechi ya Mbeya City na Simba akisema zilikamatwa tiketi nyingi bandia lakini baadhi yawasimamizi milangoni kutoa TFF walionekana kuziruhusu tiketi hizo wakidai zilikuwa halali hali iliyoleta migongano katika milango ya dimba la Sokoine.

TUNDUMA WABOMOA KINGO ZA BARABARA MPYA YA LAMI KUIBA KOKOTO

SERIKALI mkoani Mbeya imeagiza kukamatwa mara moja kwa mtu yeyote atakayebainika kukusanya kokoto na mchanga pembezoni mwa barabara mpya iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka mji mdogo wa Tunduma kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ametoa agizo hilo jana baada ya kubaini uwepo wa baadhi ya wakazi katika mji wa Tunduma ambao wamekuwa wakitumia zana mbalimbali kubomoa barabara na kisha kuiba kokoto hivyo kuhatarisha uimara wa barabara hiyo iliyojengwa hivi karibuni. Akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Momba,Kandoro ameshuhudia uharibifu huo wa barabara pasipo uoga baadhi ya wakazi wamekutwa wakikusanya kokoto hizo na kuzirundika pembezoni mwa baarabara wakisubiri wateja. Meneja mradi wa mradi wa barabara hiyo kutoka wakala wa Barabara(Tanroads) Eliazary Rweikiza alisema takribani kilometa tano za kipande cha barabara hiyo zimeathiriwa na wizi huo unaohatarisha uimara wa barabara. Akizungumzia uharibifu huo,mkuu wa mkoa aliyeonekana kukasirishwa na vitendo hivyo,ameamuru kukamatwa mara moja kwa wezi hao pamoja na wateja wanaonunua kokoto zilizoibwa na kufikishwa katika mikono ya sheria. Alisema lengo la serikali kuwekeza mamilioni ya fedha katika miundombinu ya barabara ni kurahisisha mawasiliano kupitia njia hiyo ili maendeleo yaweze kupatikana kwa urahisi hivyo haivumiliki kuona watu wachache wakikwamisha jitihada hizo.

Wednesday, February 12, 2014

MAISHA HAYA MPAKA LINI?

Nyumba ya mmoja wa wakazi wa kijiji cha Wambishi kata ya Ulenje wilayani Mbeya ambaye hakufahamika jina kwani hakukutwa nyumbani kwakwe ikiwa imeezekwa nyasi na juu yake kuwekwa vumbi la mbao ili kuzuia maji ya mvua yasiingie ndani

Saturday, February 8, 2014

WANAWAKE WAUAWA NA WAUME ZAO KISA WIVU

WATU watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio tofauti yakiwemo ya wanawake wawili kuuawa na waume zao kutokana na wivu wa kimapenzi wilayani Chunya. Kwa mujibu wa kamanda wa Polisisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi,katika tukio la kwanza lililotokea Februari 6 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi katika kijiji cha Shoga wilayani Chunya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Agnes Daud (32) mkazi wa kijiji hicho alikutwa ameuawa na mume wake aliyefahamika kwa jina la moja la Thomas. Kamanda Msangi alisema mume huyo alimuua mkewe kwa kumkata koromeo kwa kutumia kisu na kuwa mwili wa marehemu ulikutwa katika kibanda walichokuwa wanaishi na mume wake katika kambi ya uchimbaji madini mali ya Isack Mambo. Alisema katika tukio la pili lililotokea siku hiyo hiyo majira ya saa 12 jioni huko katika kitongoji cha London wilayani Chunya mwanamke mwingine aliyefahamika kwa jina la Defroza Gidion (18) mkazi wa kijiji cha Isanzu aliuawa kwa kupigwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aliyefahamika kwa jina la Juma Januari. Alisema tukio hilo lilitokea wakati marehemu akiwa nyumbani na kubainisha kuwa vyanzo vya mauaji hayo yote mawili ni wivu wa kimapenzi. Alisema watuhumiwa walikimbia mara baada ya tukio na juhudi za kuwatafuta zinaendelea ambapo kamanda huyo wa polisi mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali walipo watuhumiwa wa matukio hayo azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake, vinginevyo wajisalimishe wenyewe. Wakati huo huo kamanda Msangi alisema mwendesha pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda aliyefahamika kwa jina la Oswald Ndunguru(26) mkazi wa Iganzo amekufa papo hapo amefariki dunia baada ya kugongwa na gari. Alisema tukio hilo lilitokea februari 7 mwaka huu saa 12:00 jioni katika maeneo ya Kilimo Uyole jijini Mbeya ambapo Oswald akiwa anaendesha boda boda yenye namba T 322 CTJ aina ya Shineray aligongwa na gari yenye namba T893 BPD aina ya Isuzu iliyokuwa ikiendeshwa Emanuel Nsolo(31) mkazi wa kijiji cha Kikondowilayani Mbeya. Licha ya dereva wa boda boda kupoteza maisha eneo la tukio pia aajali hiyo ilisababisha majeraha kwa abiria wa pikipiki aliyefahamika kwa jina la Getruda Mwakalobo (28) mkazi wa Iganzo aliyelazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo chanzo cha ajali ni dereva wa gari kukatisha barabara bila kuchukua tahadhari

VIJANA MATATANI KWA NOTI BANDIA

POLISI mkoani hapa inawashikilia vijana wawili kwa tuhuma za kukutwa na noto bandia zenye thamani ya jumla ya shilingi 285,000. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi aliwataja vijana wanaoshikiliwa kuwa ni Patrick Msigwa (34) na Anthony Mwakifwamba (32) wote wakazi wa kijiji cha Isyonje wilayani Mbeya. Kamanda Msangi alisema vijana hao walikamatwa februari 7 mwaka huu saa 9:30 alasiri katika kijiji cha Simambwe kilichopo wilayani Mbeya wakiwa na noti bandia 57 zenye thamani ya shilingi 5000 kila moja. Alisema wakazi wa kijiji cha Simambwe ndio waliowakamata vijana hao walipokuwa wakinunua ships na kutoa noti bandia ya shilingi 5000 na walipobanwa ndipo walipoonesha noti nyingine. Kamanda Msangi alisema taratibu za kuwafikisha vijanahao mahakamani zinaendelea na kutoa rai kwa wananchi kuwa makini kwa kukagua noti wanazopewa wakati wa malipo ya aina yoyote ili kuepeka fedha hizo bandia.

Tuesday, February 4, 2014

ZIARA YA RC KANDORO SIKU YA KWANZA MBEYA VIJIJINI

Ziara ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Abass Kandoro(Mwenye suti ya kaki) ilianzia katika Mradi wa ujenzi wa banio la maji kwaajili ya kuwezesha kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Imezu unaoendelea.Akiwa hapa Kandoro akaelezwa namna kikundi cha wajanja wachache kilivyotaka kutafuna fedha kiasi cha shilingi milioni 208 kilipoomba kutoka halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa madai kuwa kilitaka kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji.Baadaye ilibainika kuwa wanakikundi hawakuwa wakazi wa kijiji hicho na ndipo halmashauri ikachukua uamuzi wa kusitisha matumizi ya fedha hizo ambazo zilikuwa zimekwisha inginzwqa katika akaunti ya kikundi hicho. Hata hivyo hadi mkurugenzi wa halmashauri anasitisha matumizi ya fedha hizo tayari wajanja hao walikuwa wamekwishachota kiasi cha shilingi milioni 21.Baadaye kiasi kilichosalia halmashauri ilichukua maamuzi ya kuwasaidia wakazi halali wa kijiji cha Imezu kujenga banio hili hivyo ilihamisha fedha kutoka akaunti ya kikundi cha wajanja wajanja na kuingiza katika akaunti ya kijiji kiasi cha shilingi 187,139,000 ambazo ndiyo zinatumika kutekeleza mradi huu.Agizo la Kandoro ni kuwa ifikapo kesho asubuhi(Februari 5) kaimu mkurugenzi awasilishe taarifa juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliotafuna milioni 21 ikiwa ni pamoja na maafisa kilimo waliohusika kupeleka fedha hizo kwenye akaunti ya kikundi cha wezi kwani fedha hizo lazima zirejeshwe.Kandoro pia ameagiza asubuhi hiyo hiyo kaimu mkurugenzi amfikeshe ofisini kwake afisa aliyetelekeza mizinga iliyokabidhiwa wakati wa mbio za mwenge kwa vikundi vya wafugaji lakini haijawekwa mahali husika hadi mkuu huyo wa mkoa alipoikuta imetelekezwa pembezoni mwa bara bara wakati akitoka kijiji cha Itewe kwenda kijiji cha Wambishi kata ya Ulenje. Akiwa katika kijiji cha Itewe aliweza kutembelea shamba la mmoja wa wakulima walionufaika na mpango wa serikali wa kutoa pembejeo ya mbolea kwa wakulima wasio na uwezo.Haya ni sehemu ya mafanikio ya mpango huo. Ziara ikaendelea hadi katika shule ya sekondari ya Itala iliyopo katika kata ya Ulenje.Hapa ni kutembelea mradi wa maabara ya shule hii ya kata. Hapa mkuu wa mkoa akimsikiliza mkuu wa shule hiyo alipokuwa akizungumza changamoto ikiwemo wazazi kutokuwa na hamasa ya kuchangia chakula kwaajili ya watoto ili wapate chakula shuleni hapo. Ziara kwa siku hii ya kwanza ikamalizika kwa kutembelea jengo la machinjio mapya yanayotarajiwa kuwa ya kisasa.Machinjio haya yanajengwa katika kata ya Utengule Usongwe.Mkuu wa mkoa ameitaka halmashauri kutafuta mbinu mbadala itakayowezesha kupatikana kwa fedha kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo.Moja ya njia sahihi alizoshauri ni kutafuta mwekezaji atakayekubali kuingia ubia na halmashauri kukamilisha ujenzi huo na machinjio yatakapokamilika kutokana na mkataba wa kimakini utakaokuwa umewekwa awe mwekezaji na kuanza kukata kiasi alichowekeza kwenye kodi anayopaswa kuilipa halmashauri.