Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, February 3, 2014

MBEYA CITY WALIA NA MWAMUZI KIPIGO CHA YANGA

TIMU ya soka ya Mbeya City ya jijini Mbeya imelia na waamuzi wa mchezo kati yake na timu ya Yanga ya Dar es salaam ikisema ndiyo wealiosababisha iambulie kipigo cha goli 1-0. Mwamuzi Abdalah Kambuzi kutoka Shinyanga ni mmoja kati ya waamuzi wa mchezo huo waliolalamikiwa na Mbeya City waliobainisha kuwa kama hakukuwa na makubaliano ya kuibeba Yanga basi hakuwa na uwezo wa kuchezesha mchezo huo. Msemaji wa Mbeya City Fredy Jacksoni alielezea malalamiko hayo alipozungumza na mwandishi wetu mara baada ya timu hiyo kutua jijini Mbeya ikitokea Dar es salaam ilikopata kipigo kwa mara ya kwanza tangu ilipotinga ligi kuu. Jackson alisema udhaifu wa mwamuzi Kambusi ulijidhihirisha wazi katika maamuzi mbalimbali aliyoyafanya uwanjani ikiwa ni pamoja na kumpa kadi nyekundu kiungo wa Mbeya City Steven Mazanda pasipo watu wote uwanjani kujua tatizo ilikuwa nini kwani ilipaswa ipigwe mpira wa adhabu. “Mpaka kadi inatolewa tayari mwamuzi alikuwa ameruhusu upigwe mpira wa adhabu ndogo.Hakuna anayejua sababu ya kocha huyu kutoa kadi nyekundu.Tungeweza kusema Mazanda alimtolea lugha chafu lakini walikuwepo wachezaji wa Yanga na wa kwetu hakuna aliyesikia neon lolote lililotamkwa wala ishara yoyote inayoashiria lugha mbaya” alisema. “Nadhani mwamuzi alilenga kuinyong’onyesha Mbeya City hatua inayoonekana ni kuendeleza Uyanga na Usimba ndani ya soka la Tanzania.Lakini wadau watambue kuwa kuendelea kwa vitendo hivi ni kusdidimiza soka letu nchini na tutambue kuwa kamwe hatutakuja pata timu bora ya Taifa kwa namna hii.” Alisema. Alisema Mbeya City inaamini kuwa ni kutokana na kuzibeba timu kubwa na kuziwezesha kutwaa kombe la ligi kuu ndiyio sababu timu hizo zimekuwa zikishindwa kufanya vyema pale zinapovuka mpaka wan chi na kwenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano mbalimbali ya kimataifa kwakuwa hazina sifa. Msemaji huyo alilitaka shirikisho la soka nchini(TFF) kuangalia upya uwezo wa waamuzi wanaochezesha mechi za ligi kuu na kuwapanga kuchezesha kwa kuzingatia uwezo wa mwamuzi mmoja mmoja na kuoanisha na mchezo husika. Alisema waamuzi wako wengi lakini sui kila mmoja anao uwezo wa kuchezesha michezo yote na kubainisha kuwa hata Ulaya baadhi ya mechi zilizo ngumu zimekuwa zikipangiwa waamuzi walio na uwezo zaidi ili kuufanya mchezo husika uweze kuchezeshwa katika hali ya usawa.

No comments:

Post a Comment