Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, February 16, 2014

TUNDUMA WABOMOA KINGO ZA BARABARA MPYA YA LAMI KUIBA KOKOTO

SERIKALI mkoani Mbeya imeagiza kukamatwa mara moja kwa mtu yeyote atakayebainika kukusanya kokoto na mchanga pembezoni mwa barabara mpya iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka mji mdogo wa Tunduma kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ametoa agizo hilo jana baada ya kubaini uwepo wa baadhi ya wakazi katika mji wa Tunduma ambao wamekuwa wakitumia zana mbalimbali kubomoa barabara na kisha kuiba kokoto hivyo kuhatarisha uimara wa barabara hiyo iliyojengwa hivi karibuni. Akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Momba,Kandoro ameshuhudia uharibifu huo wa barabara pasipo uoga baadhi ya wakazi wamekutwa wakikusanya kokoto hizo na kuzirundika pembezoni mwa baarabara wakisubiri wateja. Meneja mradi wa mradi wa barabara hiyo kutoka wakala wa Barabara(Tanroads) Eliazary Rweikiza alisema takribani kilometa tano za kipande cha barabara hiyo zimeathiriwa na wizi huo unaohatarisha uimara wa barabara. Akizungumzia uharibifu huo,mkuu wa mkoa aliyeonekana kukasirishwa na vitendo hivyo,ameamuru kukamatwa mara moja kwa wezi hao pamoja na wateja wanaonunua kokoto zilizoibwa na kufikishwa katika mikono ya sheria. Alisema lengo la serikali kuwekeza mamilioni ya fedha katika miundombinu ya barabara ni kurahisisha mawasiliano kupitia njia hiyo ili maendeleo yaweze kupatikana kwa urahisi hivyo haivumiliki kuona watu wachache wakikwamisha jitihada hizo.

No comments:

Post a Comment