Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, December 27, 2014

ZIARA YA DK.MWAKYEMBE NA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU MKOANI MBEYA SIKU YA 1

 Waziri wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe akitoa ufafanuazi kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu juu ya namna kiwanda cha kusaga kokoto cha Kongolo kilichopo Mswiswi wilayani Mbarali kinachomilikiwa na Shirika la reli la Tazara kinavyofanya kazi ya uzalishaji wa kokoto kwaajili ya kuimarishia miundombinu ya reli.Katikati ni mwenyekiti wa kamati ya bunge Prof.Juma Kapuya akifuatiwa na kaimu meneja wa mgodi kokoto Juma Mizambwa
 Msafara Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu na waziri wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe ukiangalia namna kokoto zinavyozalishwa katika mgodi wa kuzalishia kokoto wa Kongolo uliopo katika kijiji cha Mswiswi wilayani Mbarali.

 Hapa wajumbe wa kamati walishauri uongizi wa kmgodi kona uwezekano wa kukopa fedha ili kuboresha mitambo na kuongeza uzalishaji wa kokoto ili kutengeneza faida zaidi ya sasa.
 Baada ya kutoka katika mgodi wa kusaga kokoto,safari ikaendelea mpaka kilipo kiwanda cha kutengenezea mataluma ya Reli kwa kutumia saruji maalumu badala ya chuma.
 Kaimu meneja wa mgodi kokoto Juma Mizambwa akielezea namna mataluma ya reli yanavyotengenezwa kwa kutumia saruji na si chuma
 Mataluma ya Reli yaliyotengenezwa kwa kutumia saruji maalumu yakiendelea kukaushwa kabla ya kuondolewa kwenye mtambo wa kutengenezea.


Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiangalia mataluma ya reri yaliyotengenezwa kwa kutumia saruji ambayo ni mbadala wa mataluma ya chuma hali inayopunguza gharama za ununuzi na usafirishaji wa mataluma ya chuma kutoka nje ya nchi.Mataluma haya ya saruji yanazalishwa na Tazara katika kiwanda kilichopo Mswiswi wilayani Mbarali.




 Ziara ikaendelea kurejea jijini Mbeya hadi ilipo karakana ya Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) maeneo ya Iyunga kama inavyoonyesha hapa chini.
 Hapa wabunge walielezwa namna Tazara mkoa wa Tanzania ilivyodhamiria kufufua vichwa vya treni vilivyoharibika kutokana na ajali mbalimbali.Usishangae kusikia mkoa wa Tanzania,Tazara inaendeshwa katika mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Tanzania na mkoa wa Zambia.
 Wabunge walishauri kuangaliwa upya kwa sheria ya uanzishwaji wa Tazara ili kupunguza migongano ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikiibuka na kusababisha utendaji wa shirika hilo kuendelea kuzorota,hivyo kulifanya lisiwe na tija katika maendeleo ya uchumi wa taifa.Wamunge walisema ni muhimu sheria ikabadilishwa ili bajeti ya Tazara mkoa wa Tanzania iwe inapelekwa katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.

 Hiki ni moja kati ya vichwa vya treni vitakavyojengwa upya na Tazara.

 MATUKIO YA SIKU YA PILI YA ZIARA YATAKUJIA KESHO AKSANTE KWA KUWA NASI

Wednesday, December 24, 2014

MERRY CHRISTMASS AND HAPPY NEW YEAR



Kwa niaba ya jopo zima la blogu ya Lyamba Lya Mfipa inayopatikana kwa anuani ya www.jodanyp.blogspot.com,  mhariri mkuu wa LYAMBA Lya Mfipa Bw.Joachim Nyambo anawatakia heri ya Krismasi na Mwaka mpya 2015.Tunatambua mchango wadau wetu na tunawaahidi kuongeza ubora wa huduma zetu za uhabarishaji.

J.D.Nyambo.
Mhariri mkuu Lyamba Lya Mfipa

Tuesday, December 16, 2014

TANESCO YASEMA MGAWO WA UMEME KUBAKI HISTORIA NCHINI

 Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba akitoa taarifa yaa mikakati ya shirika hilo ili kukomesha tatizo la mgawo wa umeme nchini









 Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla akizungumza na maafisa wa Tanesco kabla ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo.

 Afisa Mwandamizi wa Tanesco kanda ya Nyanda za juu kusini Salome Kondola akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya mkuu wa wilaya 
 Maafisa wa Tanesco wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla baada ya kiongozi huyo kufungua mkutano wa baraza lao.
 
                            HABARI KAMILI 
 
SHIRIKA la Ugavi la Umeme nchini(Tanesco) limesema ifikapo mwishoni mwa mwaka 2016 Tanzania suala la mgawo wa umeme litabaki kuwa historia.

Uhakika huo unakuja kufuatia mikakati ya utekelezaji wa miradi ikiwemo Kinyerezi namba moja wa megawati 150 ambao hadi sasa asilimia 90 ya utekelezaji wake umekamilika.

Upo pia mradi wa kinyerezi namba mbili wa megawati 240 ambao serikali iko kwenye hatua za mwisho za maelewano ya kifedha baina ya wizara ya fedha,benki ya Japani na benki ya maendeleo ya Afrika kusini ambapo ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwakani.

Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza kuu la 45 la wafanyakazi wa Tanesco linalofanyika jijini Mbeya.

Mhandisi Mramba amesema miradi ya kinyerezi namba tatu na nne imeanza kwa ubia kwa makampuni mawili ya kichina na utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwakani kama ilivyo kwa kinyerezi namba mbili.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla amewataka watoa huduma kutoka shirika hilo kuwa na lugha zenye kumwelewesha mteja na si kujibu hovyo hovyo.

Dk.Sigalla amesema majibu mabovu ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya watendaji wa shirika hilo yamekuwa yakisababisha serikali kulaumiwa na kuonekana haifai kwakuwa haiwathamini wananchi katika kutoa huduma za nishati ya umeme.

Amesema ni vema wataalamu hao wakawa na lugha zenye ukweli kwa wateja badala ya lugha za kuwalaghai na kuwadanganya na mwisho wa siku mteja anakuja kubaini ukweli uliopo na kulichukia shirika na serikali.

Monday, December 15, 2014

MWANACHUO TIA ADAIWA KUTUPA KICHANGA DAMPO

Maiti ya mtoto mchanga ikiwa imetelekezwa kama ilivyokutwa na wakazi wa eneo la Airpot jijini Mbeya(Picha kwa hisani ya mmoja wa wakazi wa eneo hilo)

MWANAMKE asiyefahamika ametupa mtoto mchanga katika Dampo la taka lililopo katika eneo la Airpot jijini Mbeya jirani na kilipo chuo cha uhasibu(TIA) tawi la Mbeya.

Wakazi wa maeneo ya jirani na dampo hilo wanasema waliikuta maiti ya kichanga hicho ikiwa imetelekezwa hapo lakini inasadikiwa kuwa kabla ya kutupwa mtoto huyo alikuwa hai.

Hili si tukio la kwanza kwa maiti za vichanga na pia vichanga vilivyo hai kukutwa vimetelekezwa kwenye dampo hili.Baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani na dampo hili wanahusisha matukio ya utupaji watoto wachanga na pia maiti za watoto hao na wanafunzi wa chuo cha TIA.

“Hii si mara ya kwanza kukuta maiti ya kichanga hapa.mara kwa mara tumekuwa tukiokota.Wengi wetu tunaamini wanaofanya ukatili huu ni wanafunzi wanaosoma humo ndani TIA.Wanaagopa kulea ndiyo sababu wanatupa vichanga namna hii” alisema mmoja wa wakazi wa maeneo hayo aliyeomba jina lake kutoandikwa katika Lyamba Lya Mfipa.
 


MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI MKOANI MBEYA



 Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Makunguru jijini Mbeya wakiwa katika foleni ya kuelekea kupiga kura.

               HABARI YA MATOKEO YA AWALI

MATOKEO ya awali yaliyopatikana  mkoani Mbeya katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaonesha Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuongoza  katika maeneo mengi kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mpaka tunakwenda mitamboni jioni hii matokeo yalipatikana kwenye vitongoji 2047 kati ya 2567, vijiji 606 kati ya 771 na mitaa 252.

Kwa upande vijiji,Wilaya ya Chunya yenye vijiji 86 yalikuwa yamepatikana matokeo ya vijiji 74, ambapo  kati ya vijiji hivyo,CCM ilikuwa imeshinda vijiji 67 na Chadema vijiji saba.

Wilaya ya Ileje yenye jumla ya vijiji 71 ambapo matokeo yalikuwa yamepatikana ya vijiji 32 CCM ilikuwa imeshinda vijiji 23 na Chadema vijiji 9.

Kwa wilaya ya Kyela yenye jumla ya vijiji 93 ambayo matokeo ya vijiji vyote yalikuwa yamepatikana CCM imeshinda vijiji 79 na Chadema vijiji 13 huku kijiji kimoja uchaguzi ukiwa haukufanyika.

Wilayani Mbarali kuliko na jumla ya vijiji 102, matokeo yalikuwa yamepatikana ya Vijiji 97 ambapo  CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 81 na Chadema vijiji 16 na vijiji vitano yalikuwa yakisubiriwa.

Wilaya ya Mbozi yenye vijiji 125 ambapo matokeo ya vijiji 92 yalikuwa yamepatikana CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 84,Chadema vijiji  8 na vijiji 33 yalikuwa yakisubiriwa.

Wilaya ya Rungwe yenye vijiji155,matokeo ya vijiji 150 yalikuwa yamepatikana,CCM ilishinda vijiji 127,Chadema vijiji 22,CUF kijiji kimoja na vijiji vitano matokeo yalikuwa yanasubiriwa.

Wilaya ya Momba ina vijiji 72 kati ya hivyo vijiji 67 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 43,Chadema vijiji 24 na vijiji vitano yalikuwa yanasubiriwa.

Kwa upande wa Mitaa Mbeya mjini kuliko na mitaa 181,CCM imeshinda mitaa 106,Chadema mitaa 71 na Nccr Mageuzi mtaa mmoja wakati katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba ulio na mitaa 71 Chadema iliibuka kidedea katika mitaa 46 na CCM ikaambulia mitaa 25.

Kwa upande wa Vitongoji,Chunya yenye vitongoji 438 ambapo matokeo ya vitongoji 288 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 270 na Chadema vitongoji 18.

Kyela yenye vitongoji 469 CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 377 na Chadema vitongoji 88 huku vitongoji vinne uchaguzi ukiwa unapaswa kurudiwa.

Wilaya ya Mbozi yenye jumla ya vitongoji 664 ambayo matokeo ya vitongoji 414 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 359,Chadema vitongoji 55 na matokeo ya vitongoji 250 yalikuwa yanasubiriwa.

Wilaya ya Rungwe yenye jumla ya vitongoji 694,matokeo ya vitongoji 634 yalikuwa yamepatikana na CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 557,Chadema vitongoji 110,Cuf vitongoji viwili na TLP kitongoji kimoja na vitongoji 60 yalikuwa yakisubiriwa.

Wilaya ya Momba ina jumla ya vitongoji 302 kati ya hivyo vitongoji 242 matokeo yalikuwa yamepatikana ambapo CCM ilikuwa imeshinda 189,Chadema 53 na vitongoji 60 vilikuwa bado matokeo yakisubiriwa.