Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, November 28, 2013

UZINDUZI MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA MBEYA

Waziri wa Uchukuzi Djk.Harrison Mwakyembe akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Maonesho ya biashara Mbeya(Mbeya Expo 2013)yanayoendelea katika viwanja vya kituo cha mikutano cha Mkapa jijini Mbeya.Monesho hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara,wamiliki wa viwanda na wakulima(TCCIA) mkoa wa Mbeya yanashirikishawafanyabiashara wa ndani na wa nchi jirani ya Kenya

Tuesday, November 26, 2013

MWAKYEMBE AIFAGILIA PSPF

Waziri wa Uchukuzi Djk.Harrison Mwakyembe akisalimiana na wafanyakazi wa PSPF alipotembelea banda la mfuko huo kwenye maonesho ya biashara Mbeya(Mbeya Expo 2013)yanayoendelea katika viwanja vya kituo cha mikutano cha Mkapa jijini Mbeya. Afisa Uendeshaji wa PSPF Amina Mtingwa akitoa maelekezo ya namna ya kujiunga na Mpango wa uchangiaji kwa hiari mmoja wa wateja waliofika katika banda hilo.Mpango huo unawalenga watu wiote pasipokujali mhusika yuko katika sekta rasmi au isiyo rasmi. . Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Joachim Nyambo naye ni mmoja kati ya waliotembelea banda la PSPF na kupata maelezo juu ya namna ya kujiunga na pia faida za Mpango wa uchangiaji kwa hiari kama anavyoonekana hapa. WAZIRI wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe ameupongeza mfuko wa Penseni kwa watumishi wa umma (PSPF) akisema umekuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia serikali kuwaletea maendeleo wananchi wake. Dkt Mwakyembe ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la PSPF kwenye maonesho ya biashara yanayoendelea mkoani Mbeya yakiwashirikisha wafanyabiashara wa ndani na nchi jirani ya Kenya. Amesema kazi zinazofanywa namfuko huo ni nzuri na zenye tija inayojulikana kwa kila mmoja na kuwataka watendaji wa mfuko huo kuendelea kujituma kutekeleza majukumu yao ili sifa iliyopo iwe endelevu. Kwa upande wake afisa uendeshaji wa PSPF Bibi Amina Mtingwa amesema mfuko huo amesema kasi ya wananchi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa hiari imeendelea kuongezeka ikilinganishwa na mwanzoni mwa mwaka huu ulipoanzishwa mpango huo. Hata hivyo Bi.Mtingwa amesema bado elimu zaidi inahitajika kwa jamii juu ya mpango huo aliosema una faida kubwa hasa kwa watu wanaojiwekea malengo ya kufanya jambo lolote lenye kuhitaji fedha kwakuwa mhusika ataweza kujikusanyia kwa kuweka kiasi kisichopungua shilingi 10,000 kwa kila mwezi.

Sunday, November 24, 2013

WANAHABARI JOACHIM NYAMBO NA VENANCE MATINYA WAIBUKA MABINGWA WA KUPANDA MLIMA MBEYA

Haikuwa kazi rahisi kuufikia msalaba huu uliopo katika safu ya mlima Mbeya.Kilichokuwa kiikitutisha zaidi ni wingu zito lililotanda mara tu baada ya sisi kufika msalabani hapa.Hofu ya kunyeshewa na mvua ikawa mioyoni mwetu.Lakini tulipiga magoti na kumwomba mwenyezi Mungu.Naama sala zetu zikarsikika maada ya manyunyu kidogo wingu hili unaloliona hapa juu likasambaa Mwandishi wa gazeti la Jamboleo Venance Matinya akifurahia kufika katika msalaba huu kabla ya kuendelea na safari ya kupanda mlima hadi ilipo minara ya vituo mbalimbali vya mawasiliano Mwonekano wa jiji la Mbeya ukiwa katika eneo la msalaba mlimani Safari ikaendelea kutoka eneo la msalama na kupanda zaidi mlima hadi kilele kikuu na baadaye kushukia katika kijiji cha Mbeya Peack kabla ya kushuka mlima huo kurejea jijini Mbeya Kuna wakati ilibidi kupumzika kwa muda kama anavyoonekana mwandishi Venance Matinya akiwa hoi na kuliona jiwe hili kama mkombozi kwake kwakuwa maeneo mengine ni vigumu kukaa kwani ungeweza kuhisi kizunguzungu. SAFARI HII IMEFANYIKA JUMAPILI HII AMBAPO WANAHABARI VENANCE MATINYA NA JOACHIM NYAMBO WALIIBUKA MASHUJAA WA KUPANDA MLIMA MBEYA BAADA YA WADAU WENGINE KUINGIA MITINI.

Tuesday, November 19, 2013

Ukiwa jijini Mbeya furahia ulimwengu wa Digitali huku ukiburudika na vinywaji mbalimbali

. MBEYA,NYUMBANI KWA WAKARIBU NA WENYE KUPENDA KUKARIBISHA WAGENI SIKU ZOTE.

SUMBAWANGA MABINGWA UMISAVUTA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

MASHINDANO ya michezo kwa vyuo vya ualimu(UMISAVUTA) kanda ya nyanda za juu kusini umemalizika kwa Chuo cha ualimu Sumbawanga kuchukua ubingwa wa mchezo wa soka. Sumbawanga ilichukua ubingwa huo baada ya kuinyuka Chuo cha Mpuguso cha wilayani Rungwe goli 5-3 kwa mikwaju ya penati iliyopigwa mara baada ya dakika 90 za mchezo wa fainali kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu huku giza likisababisha kutoongezwa kwa dakika 30 nyingine. Katika mchezo wa Voleyball Tukuyu iliinyuka Tandala seti 3-0 huku mchezo wa netiboli Sumbawanga uikaibuka bingwa kwa kuinyuka Mpuguso. Akizungumzia mwenendo wa mashindano hayo tangu kuanza hadi kumalizika kwake.mratibu wa mashindano hayo Doroty Mhaiki ambaye pia ni mkuu wa chuo cha Mpuguso kilichopo Rungwe alitaja ushiriki mdogo wa vyuo kuwa ni changamoto inayopaswa kutafutiwa ufumbuzi. Alisema mikoa ya Rukwa,Mbeya,Iringa,Njombe na Ruvuma ina jumla ya vyuo 17 vya ualimu lakini ni vinane pekee vilivyoshiriki mashindano hayo kwa mwaka huu. Changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti,uhaba wa vifaa vya michezo na viwanja hali iliyosababisha baadhi ya michezo kutochezwa kabisa hususani mchezo wa kikapu na wa mkono. “Ufinyu wa muda nao ulikuwa kikazwa kingine.Wachezaji wamelazimika kucheza kila siku pasipo kupumzika.Kiafya si vizuri na huenda ikawaletea madhara hata baada ya kumalizika kwa mashindano hayo” alisema. Akifunga mashindano hayo,mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela aliwataka waratibu wa mashindano hayo kuanza kuyahusisha mashirika ya hifadhi za kijamii ili yaweze kuwadhamini na kupunguza ukali wa bajeti za mashindano. Meela alisema mashirika hayo ni rafiki na vyuo vinavyozalisha wafanyakazi watarajiwa hivyo urafiki huo unapaswa kuimarishwa kwa mashirika kudhamini mashindano kama hayo ambayo yanafaida kwa wanavyuo ambao ni wateja wa baadaye.