Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, November 11, 2013

ALIYEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA AACHIWA HURU BAADA YA KUSOTA GEREZANI KWA MIAKA 14

MSHITAKIWA ambaye awali alihukumiwa kifungo cha maisha jela na kuchapwa viboko 10 mwaka 1999 kwa kosa la ubakaji ameachiwa huru na Mahakama kuu kanda ya Mbeya. Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Samweli Karua ametoa hukumu ya kumwachia huru mshitakiwa leo baada ya rufaa namba 17 ya mwaka 2013,iliyowasilishwa mahakamani hapo ambapo mshitakiwa Isack Righton(34) ameachiwa huru kutokana na kile kilichoelezwa na jaji Karua kuwa vigezo vya hukumu dhidi ya mshitakiwa kukiuka baadhi ya vifungu vya sheria. Awali akisoma maelezo ya kosa la mshitakiwa huyo,mwendesha mashtaka wa Serikali, Ahmed Sitambuli amesema mshitakiwa huyo alifikishwa mbele ya mahakama ya Wilaya ya Mbozi Juni 1, 1999 akikabiliwa na shitaka la kutenda kosa la ubakaji kinyume na vifungu vya sheria namba 130 na 131 (3) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Sitambuli amesema mshitakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo April 4, 1999 wakati huo akiwa na miaka 20 baada ya mhanga wa tukio hilo(jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa anaishi na wazazi wake wakiwa wapangaji katika nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na mshitakiwa. Amesema kuwa siku ya tukio lililofanyika katika kitongoji cha Kaloleni kilichopo katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Mbozi kwa wakati huo na sasa ni wilayani Momba majira ya saa moja usiku, wazazi wa mhanga walikuwa wamemwacha binti yao nyumbani ili hali wao wakiwa shambani ambapo baada ya kurudi walimsikia binti yao akilia huku akitokea chumbani kwa mtuhumiwa na kumkuta akiwa na damu pamoja na mbegu za kiume sehemu zake siri baada ya kufanyiwa uchunguzi. Lakini katika hukumu ya Jaji Karua leo katika rufaa ya mtuhumiwa huyo, amesema hukumu iliyokuwa imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, FCP Mdendemi ilikuwa na makosa matatu ya kiushahidi aliyoyataja kuwa ni pamoja na uwasilishaji wa kielelezo ambacho ni Fomu namba tatu ya Polisi(Pf3) kuwasilishwa mbele ya mahakama na shahidi ambaye ni mzazi wa mhanga Moses Simwanza badala ya Daktari aliyemfanyia uchunguzi. Amelitaja kosa la pili kuwa ni binti aliyefanyiwa kitendo hicho kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa ushahidi huku sababu ya tatu ikiwa ni ushahidi uliotolewa mahamani hapo kuwa haukutosheleza kumtia hatiani mtuhumiwa kwa sababu ya kutolewa na mashahidi watatu ambao ni baba mzazi wa mhanga, mama mzazi na Askari Polisi Wp 381 Sajent Neema. Kutokana na maelezo hayo Jaji karua alimwachia huru mshtakiwa huyo ambaye tayari amesota gerezaji kwa miaka 14 tangu kuhukumiwa katika hukumu ya awali.

No comments:

Post a Comment