Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, April 27, 2014

WAWILI AKIWEMO MWANAFUNZI WAHOFIWA KUFA MTO KIWIRA

WATU wawili akiwamo mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mwigo ya wilayani Kyela mkoani Mbeya wanahofiwa kufa maji katika Mto Kiwira. Hofu ya kufa maji watu hao inakuja baada ya mtumbwi waliokuwa wakiutumia kusafiri mtoni humo wakitokea kijiji cha Ibungu kwenda kitongoji cha Ndandalo kilichopo Kyela kati kupitia mto Kiwira uliojaa maji kutokana na mvua nyingi zilizoinyesha ukanda wa juu na kusababisha mafuriko katika mto huo. Hofu ya vifo hivyo vya watu wawili inaweza kufikisha idadi ya watu waliopoteza maisha tangu kutokea kwa mafuriko ya kihistoria wilayani hapa kufikia saba. Akizungumza na waandishi wa habari juzi mara baada ya kutokea ajari hiyo Mwenyekiti wa kitongoji cha Ndandalo Rameck Mbembela maarufu kwa jina la Mwinama alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 10.30 jioni baada ya watu watano kupanda katika mtumbwi mmoja wakivuka kutoka kijiji cha Ibungu kwenda Kyela mjini. Mwenyekiti huyo alisema kuwa wakiwa katikati ya mto huo mtumbwi uliyumba kutokana na udogo wake ikilinganishwa na uwingi wa maji yaliyokuwa pia na kasi kubwa na ndipo watu hao walipotumbukia mtoni na kuwa katika harakati za kujiokoa watu watatu akiwemo mwongozaji walifanikiwa kujiokoa na kushindwa kuwaokoa wenzao ambao wanadaiwa hawakujua kuogelea. Mbembela aliwataja watu hao waliozama kuwa ni Mzee Akupenda (70) mkazi wa kijiji cha Ibungu na kijana Stevin Stivin (15)mkazi wa Kyela aliyekuwa anasoma kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Mwigo aliyepata kadhia hiyo alipokuwa anavuka mto kwenda kumsalimia shangazi yake anayeishi kitongoji cha Kyela kati kilichopo ng’ambo ya mto huo. Aliongeza kuwa juhudi za kuitafuta miili ya watu hao bado zinaendelea na kwamba aliwataka wananchi wanaotumia njia hiyo ya mitumbwi waache na badara yake watumie njia kuu ambayo lipo daraja kubwa la kijiji cha Ipyana hadi pale serikali itakapo jenga daraja ili kunusuru madhara makubwa yasitokee. Alisema kuwa katika sehemu hiyo ya kivuko lilikuwepo daraja dogo (kityepu tyepu)ambalo lilibomolewa na serikali baada ya kuonekana kuwa ni hatarishi kwa wananchi waliokuwa wakivuka kwa kutumia daraja hilo na kufanya zoezi la kuvuka kuwa gumu hasa kwa wanafunzi wanaosoma kwenye shule zilizopo nga”ambo ya mto huo. Mbembela aliitaka serikali kupitia halmashauri ya wilaya kuliangali kwa jicho la tatu tatizo hilo hasa kufanya haraka kujenga daraja katika mto huo ambao hutumiwa na watu wengi ambao hufuata huduma za msingi Kyela mjini na wengine hufuata huduma nga”mbo ya pili hasa wanafunzi,wakulima pamoja na wafanyabiashara hivyo kutokuwepo kwa daraja ni tatizo kubwa ambalo hupunguza uchumi kwa wananchi na serikali kwa ujumla. Mwenyekiti huyo pia aliitaka Serikali wilayani humo kufanya tathimi ya uhakika ya maafa yaliyotokea kwa wilaya mzima bila kufanya ubaguzi wowote na si kukimbilia vijijini pekee na kwamba katika kata ya Kyela kati maafa ni makubwa kwa upande wa kitongoji cha Ndandalo pekee kinawahanga 26 waliobomokewa na nyumba zao akiwemo mwenyekiti kufuatia mvua hizo za mafuriko zilizotokea. Aidha Mwenyekiti huyo aliwaasa wanasiasa kuacha kutumia maafa haya kama mtaji wa kisiasa kwao na badara yake watoe misaada ya hali na mali kwa wahanga na kuwa wafanye jitihada za kuboresha miundombinu ya kujenga mifereji itakayotiririsha maji kwenye mito ili kujaribu kunusuru uharibifu wa barabara uliopo wilayani humo.

Wednesday, April 23, 2014

MAFURIKO KYELA

Baadhi ya wakazi wa eneo la Kajunjumele wakilazimika kupita katika maji katika barabara ya kutoka mjini Kyela kwenda bandari mpya ya Kiwira iliyopo wilayani Kyela baada ya barabara kufunikwa na maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya ikiwemo wilaya ya Rungwe ambayo maji yake hutiririka wilayani Kyela kabla ya kuingia ziwa Nyasa

Sunday, April 20, 2014

POLISI MWIZI WA MTOTO

AFISA mmoja wa jesjhi la polisi anashikiliwa na jeshi hilo mkoani Mbeya akituhumiwa kuiba mtoto mchanga wa siku saba. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi alimtaja jana askari anayeshikiliwa kuwa ni Detactive Constable Priscar Kilwai mwenye namba WP 5367 ambae eneo lake la kazi ni mkoa maalumu wa kipolisi wa Ilala katika kanda maalumu ya Dar es salaam. Kamanda Msangi alisema WP Priscar alikamatwa juzi(April 17) majira ya kati ya saa nne na saa tano asubuhi akiwa katika eneo la Meta jijini Mbeya alikokutwa akiwa na kichanga alichoiba. Akizungumzia kisa cha wizi huo,kamanda msangi alisema mtoto mchanga aliyeibwa alifahamika kwa jina la Goodlack Salehe ambaye alizaliwa April 6 mwaka huu huko mjini Kyela. Aliwataja wazazi wa mtoto aliyeibwa kuwa ni Mboka Mwakibabile makazi wa eneo la Njiapanda mjini Kyela ambaye ni mama wa mtoto na Salehe Isa Mwangosi mkazi wa Kasumulu ambaye ni baba wa mtoto huyo na ambaye pia anashikiliwa. Alisema siku moja kabla ya siku ya tukio baba wa mtoto huyo alimjulisha mzazi mwenzie kuwa kuna shangazi yake ambaye kesho yake angefika nyumbani kwa mama wa mtoto kwa lengo la kumwona mtoto na pia aweze kumsindikiza kumpeleka mtoto huyo kliniki. Alisema siku iliyofuaata yaani April 6 mwaka huu majira ya kati ya saa sita na saa saba mchana shangazi huyo ambaye ni WP Priscar alifika nyumbani kwa mkwewe na baada ya kumsalimia mtoto huyo waliongozana wote wawili kukipeleka kichanga kliniki kama mzazi mwenza alivyokuwa amependekeza. Alisema baada ya kufika kliniki walitakiwa kuwa na daftari na kwakuwa hawakwenda nalo ikalazimu jitihada za kwenda dukani kununua daftari hilo zifanyike. Kamanda huyo alisema shangazi huyo bandia alitoa kiasi cha shilingi 2000 na kumpa mama wa mtoto aliyekwenda moja kwa moja dukani huku akimwacha mwanaye kwa WP Priscar akijua kamwacha sehemu salama kwani alijua ni bibi yake yaani shangazi wa mzazi mwenzie. Ajabu ni kuwa mama huyo aliporudi na daftari lake hakumwona mkwewe wala mtoto hali iliyolazimu aanze kuuliza watu waliokuwepo jirani ambao baadaye walimwambia kuwa walimwona mtu aliyemwachia mtoto akipanda pikipiki na kutokomea kusikojulikana. “Baada ya hapo mama huyu akalazimika kutoa taarifa kituo kidogo cha polisi kilichopo pale Kyela na jitighada za kutafuta zilianza mara moja.Hatua ya kwanza ilikuwa ni kumkamata baba wa mtoto kwakuwa moja kwa moja alionekana kuhusika katika njama za wizi huo” alisema. Alisema baada ya kumkamata baba wa mtoto jitihada ziliendelea hadi juzi(April 17) alipokamatwa maeneo ya Meta jijini Mbeya akiwa na kichanga hicho. “Baada ya kumkamata na kupata tetesi kuwa ni afisa wa jeshi tulianza kupeleleza na ndipo tukabaini ukweli na kuwa anatokea mkoa maalumu wa kipolisi wa Ilala Dar es salaam” Kamanda Msangi alisema kinachoendelea hivi sasa baada ya kumkamata ni mashitaka ya kijeshi ili kumfukuza kazi ikithibitika juu ya tuhuma zinazomkabili na hatimaye kufikishwa mahakamani. Alisema pia uchunguzi wa awali unaonesha hakuna mahusiano yoyote ya undugu kati ya askari huyo na baba wa mtoto isipokuwa mahusiano yaliyopo ni ya kibiashara ambapo ilionekana kuna biashara ambazo wamekuwa wakifanya kwa kushirikiana.

Friday, April 18, 2014

AFISA WA JESHI LA POLISI ATIWA MBARONI KWA KUIBA KICHANGA CHA SIKU 7.Habari kamili endelea kuwa nasi

Thursday, April 17, 2014

16 WATEULIWA KUENDELEA NA KIKOSI CHA MABORESHO YA TAIFA STARS

WACHEZAJI 16 wameteuliwa kubakia katika kikosi cha Maboresho ya timu ya Taifa(Taifa stars) huku wengine wawili wakipelekwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20. Kocha msaidizi wa timu ya taifa Salum Mayanga alitangaza majina ya wachezaji wanaobaki katika kikosi hicho baada ya kufanyika kwa mchujo wa vijana hao walioanza kambi Machi 22 mwaka huu mjini Tukuyu wilayani Rungwe wakiwa 34. Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni pamoja na mlinda mlango Benedict Mlekwa kutoka Mara wakati walinzi wa kati ni Emma Simwanda kutoka kutoka mkoa maalumu wa kisoka Temeke na Joram Mgeveja kutoka Iringa. Walinzi wa pembeni ni Omari Kindamba kutoka Temeke, Edward Mayunga kutoka Kaskazini Pemba na Shirazy Sozigwa kutoka Ilala huku akiwataja viungo wa Ulinzi kuwa ni Yusufu Mlipili na Said Juma Ally kutoka Mjini Magharibi. Aliwataja viungo Washambuliaji kuwa ni Abubakar Ally Mohamed kutoka Kusini Unguja na Hashimu Ramadhani Magona kutoka Shinyanga, wakati Viungo wa pembeni ni Omari Athumani Nyenje kutoka Mtwara na Chunga Said Zito kutoka Manyara. Aliwataja washambuliaji kuwa ni pamoja na Mohammed Seif Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu Kassim Lipati kutoka Ilala, Abdurahman Othman Ally kutoka Mjini Magharibi na Paul Michael Bundara kutoka Ilala. Kwa upande wa wachezaji wawili walioteuliwa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya Miaka 20 aliwataja kuwa ni Mbwana Mshindo Musa kutoka Tanga na Bayaga Athanas Fabian kutoka Mbeya aliosema tayari wameungana na timu hiyo jijini Dar es salaam tayari kushiriki katika mechi za kirafiki za hivi karibuni. Hata hivyo Mayanga alisema kul;ikuwa na uwezekano wa kupatikana zaidi ya vijana hao kwani wachezaji walioachwa pia walikuwa na sifa na kuanzia sasa wachezaji hao wataendelea kuwa kwenye uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) kwa kuwa mpango wa maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu. Alisema wachezaji 16 walioteuliwa wanataraji kuondoka ijumaa hii kuelekea Dar es salaam kujiunga na kikosi cha Timu ya Taifa cha Awali kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya Kambi ya awamu ya Pili.

Saturday, April 12, 2014

WAENDESHA BODA BODA 37 WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA VURUGU ZA JANA

Waendesha boda boda waliofikishwa mahakamani wakisubiri kusomewa mashitaka yao mara baada ya kufikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Mbeya mjini.

Friday, April 4, 2014

VITUKO MTAANI

SIJUI TRAFIC HUYU KAMA ATATOZA FAIN MPAKA YA KUBEBA KUKU AU LA! KAZI IPO!JAMAA HAONI SHIDA KUKATISHA NA FISI MTAANI.USTAARABU HAPA F WAKATI SUMATRA WAKIPIGA MARUFUKU WATOTO WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA 9 KUBEBWA KATIKA BODA BODA NA BAJAJI KWETU MAMBO YAKO HIVI.

PROF MWANDOSYA ATEULIWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU CHA MUST

CHUO kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST) kimepata viongozi wapya watakaokiongoza kufuatia uteuzi uliofanya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi ya mahusiano ya MUST,Rais Kikwete amemteua Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Kazi maalum Prof.Mark Mwandosya(MB) kuwa Mkuu wa Chuo na kufuatiwa wakati Makamu Mkuu wa Chuo atabaki kuwa Prof. Joseph Msambichaka. Rais pia amemteua Prof. Osmund Kaunde kuwa Naibu mkuu wa chuo upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi Asili na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Prof. Emmanuel Luoga ameteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Chuo wa Chuo hicho kwa upande wa Utawala, Fedha na Mipango wakati kabla ya uteuzi huo Prof Luoga alikuwa Mkuu wa Idara ya Upimaji wa Misitu katika Chuo Kikuu cha Sokoine. Chuo cha MUST kilipanda ambacho awali kilijulikana kama Chuo Cha Sayansi Na Teknolojia Mbeya(MUST) kilipandishwa hadhi ya kuwa chuo kikuu tangu mwaka 2012 na kilianza kutoa mafunzo kama chuo kikuu kuanzia mwaka wa masomo wa 2012/2013 katika fani mbalimabali ikiwemo shahada ya Usanifu Majengo, Uhandisi mitambo,Uhandisi Umeme na fani nyinginezo. Chuo hicho kimepata mafanikio makubwa sana katika utaoji wa wanafunzi wenye ujuzi wa hali ya juu katika fani mbalimbali hali inayotokana na upatikanaji wa maabara na vifaa vya kisasa vya kufundishia. Kwa mujibu wa ofisi ya Mahusiano Chuo pia kimefanikiwa kuunda vyuo ndani ya chuo hicho ikiwemo Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (College of Engineering and Technology), Taasisi ya Sayansi na Technolojia( Institute of science and Technology) na Shule ya biashara( School of Business).

MAISHA YA WANYAMA

. MBWA NI MIONGONI MWA WANYAMA WANAOTAJWA KUWA NA UWEZO MKUBWA WA KUISHI MAISHA YA KUIGA KUTOKA KWA BINADAMU

Tuesday, April 1, 2014

KIKONGWE ACHARANGWA NA SHOKA HADI KUFA AKITUHUMIWA UCHAWI

WATU watatu wamefariki dunia wilayani Chunya mkoani Mbeya katika matukio tofauti likiwamo la kikongwe aliyefahamika kwa jina la Belta Sanzia(68) mkazi wa kitongoji cha Maweni kijiji na kata ya Mkwajuni. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema kikongwe huyo ameuawa akiwa numbani kwake kwa kukatwa na kitu kizito kinachodhaniwa kuwa ni shoka katika maeneo ya kichwani,mkono wa kulia na pia akatobolewa sehemu za ubavu wa kushoto tukio lililotokea usiku wa kuamkia jana(Machi 31). Kamanda Msangi amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina kwani marehemu aliyekuwa akiishi peke yake nyumbani kwake alikuwa akituhumiwa kuwaroga wanakijiji wenzake. Katika tukio la pili mzee aliyefahamika kwa jina la Luchagula Maenzeka(62) mkazi wa kitongoji cha Kininga kijijini Saza wilayani Chunya amekufa maji baada ya kuzidiwa na maji ya mto Saza uliopo kijijini hapo. Kamanda Msangi amesema tukio limetokea jana(Machi 31) saa 3:30 asubuhi katika kitongoji cha Kininga ambapo inadaiwa mzee huyo alishindwa kuyamudu maji ya mto huo alipokuwa akivuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine huku akiwa amelewa pombe na ndipo akasombwa na maji. Tukio jingine ni la mtoto Julieth Christian mwenye umri wa miaka miwili mkazi wa kijiji cha Saza wilayani Chunya aliyekutwa amekufa maji ndani ya kisima kilichopo jirani na nyumba wanayoishi tukio lililotokea jana(Machi 31) saa 5:00 asubuhi.