Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, January 30, 2013

TALAKA (2)

KUACHANA/TALAKA TALAKA ni amri inayotolewa na mahakama kuwaamuru wanandoa kuachana milele.Mume au mke anaweza kuiomba mahakama itoe talaka MATOKEO YA KUACHANA/TALAKA (i)Ndoa kuvunjika (ii)Mgawanyo wa mali zilizochumwa kwa pamoja na wanandoa (iii)Matunzo na malezi ya watoto kama wapo MUHIMU Kwa kawaida hairuhusiwi kuvunja/kutenganisha au kuomba talaka mahakamani kabla ya muda wa miaka miwili kupita tangu wanandoa hao waoane,isipokuwa kwa ruhusa/hati ya mahakama tu.Hati hiyo ya mahakama itatolewa ikiwa imethibitika kuwa mwombaji ana hali ngumu isiyo ya kawaida,isiyoweza kuvumilika kwa muda huo wa miaka miwili ITAENDELEA KESHO

Tuesday, January 29, 2013

HII SI SAWA HATA KIDOGO

MILANGO YA MOJA YA JENGO LILILOPO KATIKA KITUO CHA AFYA CHA KATA YA MALANGALI WILAYANI ILEJE MKOANI MBEYA KAMA ILIVYOKUTWA NA LyAMBA Lya Mfipa

TALAKA NO 1

Nchini Tanzania sheria inayotawala masuala ya kuachana na kutengana ni sheria ya Ndoa ya mwaka 1971. KUTENGANA Ni kitendo cha wanandoa(Mume na mke) kwa amri ya mahakama au hiari yao wenyewe kuishi mbalimbali kwa muda.Kutengana kwa wanandoa hutokana na wanandoa hao kutoelewana.Mume au mke ana haki ya kuomba kutenganishwa na mwenzake.Baada ya muda fulani wanandoa hao wanaweza kurudiana tena au kuachana kabisa ITAENDELEA KESHO...............

Saturday, January 26, 2013

VURUGU ZA MASASI MTWARA

WATU WAWILI WAUAWA NI KATIKA VURUGU ZILIZOIBUKA BAADA YA MADEREVA WA BODABODA KUVAMIA KITUO CHA POLISI KUSHINIKIZA WENZAO WAACHIWE HURU TUNAAMBIWA SASA VURUGU ZIMETULIA POLISI WAMEFANIKIWA KUDHIBITI Endelea kuwa nasi

Tuesday, January 22, 2013

MUME AJINYONGA BAADA YA KUMNYONGA MKE

WATU wane wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la mume kujinyonga kwa kamba ya manira muda mfupi baada ya kumnyonga shingo hadi kumuua mkewe kutokana na wivu wa mapenzi. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman aliwataja marehemu katika tukio hilo kuwa ni Richard Mwakalukwa(23) na mkewe Agnes Kalinga(18) wote wakazi katika kitongoji cha Mkeje kijiji cha Mwalisi kata ya Ngana wilayani Kyela. Kamanda Athuman alisema tukio hilo lilitokea Januari 21 mwaka huu majira ya saa 9:00 alasiri ambapo wakiwa chumbani kwao mume alimnyonga shingo mkewe mpaka kuivunja na baada ya kuona amemuua akachukua kamba ya manira na kujinyonga katika mti wa mkorosho nje ya nyumba yao. Alitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu wa mapenzi kwani mume Mwakalukwa kwa muda mrefu alikuwa akimtuhumu mkewe kutokuwa mwaminifu katika ndoa yao kutokana na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine. Katika tukio jingine lililotokea Januari 21 majira ya saa 12:30 jioni katika kijiji cha Hanseketwa wilayani Mbozi barabara ya Mbeya/Tunduma Gari lenye namba T 451 BRK Toyota Coasta lililokuwa likiendeshwa na Willy Songelamaarufu kama Muasisi(46) liligonga pikipiki yenye namba T 201 CCT aina ya T-Better na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki hiyo Tito Nyondo(20) mkazi wa Tunduma. Ajali hiyo pia alimsaababishia majeraha mwanafunzi wa shule ya sekondari Msika Baraka Nyondo(19) ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mbozi iliyopo katika mji mdogo wa Vwawa. Kamanda Athumani alisema tukio la tatu ni la kifo cha mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Mwanyanje Halaika Bushiri(7) kilichosababishwa na ajali ya moto iliyotokea nyumbani kwao Uyole jijini Mbeya. Alisema tukio hilo lilitokea januari 21 majira ya 7:45 za mchana wakati mtoto huyo alikuwa amelala kwenye kochi lililokuwa kwenye korido ulipoanzia moto lakini baadaye ukazimwa.

Wednesday, January 16, 2013

NG'OMBE WALIOHAMISHWA BONDE LA KILOMBERO WALIVYOTAPAKAA JIRANI NA HIFADHI YA ENEO OEVU LA IHEFU WILAYANI MBARALI

KANDORO AKATAA SOKOMATOLA KUNYANG'ANYWA VIWANJA

HALMASHAURI ya jiji la Mbeya imeshauriwa kumaliza mgogoro kati yake na wakazi wa eneo la Sokomatola kwa kuruhusu wakazi hao kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa wao wenyewe ili waweze kukubaliana na kuuziana nyumba.
Kwa muda mrefu halmashauri imekuwa ikilumbana na wakazi wa eneo hilo ambapo ilitaka kuwahamisha na kisha ichukue ilichukue na kugawa viwanja upya kwa watu walio na uwezo wa kujenga maghorofa lengo likiwa ni kupendezesha mji. Hali hiyo inatokana na nyumba nyingi zilizopo katika eneo la Sokomatola kuwa za kizamani na zilizochakaa hali isiyoendana na madhari ya kisasa yaliyopo kwenye kituo cha mikutano cha Mkapa cha halmashauri ya jiji la Mbeya kilichopo maeneo hayo. Lakini Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameshauri halmashauri kuwaruhusu wamiliki wa nyumba katika eneo hilo kufanya maamuzi wao wenyewe kwa kukubaliana na watu walio na uwezo wa kujenga magorofa na si kuwaingilia. “Tumeona mahala kwingi wafanyabiashara au wawekezaji wakubwa wanawafuata watu walio na viwanja na kufanya mazungumzo nao na wanakubaliana vizuri.Wengine wanawajengea nyumba mbali kisha wanawaachia viwanja ama wanakubaliana ikijengwa ghorofa huyu amiliki vyumba kadhaa na mwenzake vinavyobaki”. “Halmashauri isiingilie makazi ya watu.Mnadumaza eneo la Sokomatola.Na mnatudanganya kusema ninyi mtalinunua kasha muuze viwanja upya pesa hamna mtazitoa wapi.” Kandoro pia alishauri halmashauri kufanya mazungumzo na kituo cha utafiti wa kilimo cha Uyole jijini hapa ili ili iweze kupewa eneo la mbele lililo pembezoni mwa barabara ili litumike kwa ujenzi wa makazi badala ya kilimo kama linavyotumika hivi sasa. Alisema ili kuwa na mji wenye mwonekano mzuri ni vema halmashauri ikajipanga na kuhakikisha hakuna vichaka katikati ya mji badala yake iwezeshe wakazi kupata viwanja kwenye maeneo yaliyo wazi na kujenga

UKIWA MBEYA KULA UTAKACHO

Tuesday, January 15, 2013

WAWILI WAZIKWA HAI

WATU wawili wakazi wa kijiji cha Ivuna wilayani Momba wamezikwa wakiwa hai baada ya wakazi wenzao kuwatuhumu kuwa ni wachawili. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea siku ya jumapili iliyopita ambapo aliwataja waliozikwa kuwa ni Mizinara Matela na Ernest Molela wote wakazi kijijini hapo. Kamanda Athumani alisema wakazi hao walikuwa wakituhumiwa na wanakijiji wenzao kuwa walihusika na kifo cha ndugu yao aliyemtaja kwa jina la Nongwa Molela aliyekufa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Alisema baada ya maziko ya Nongwa ndipo wakazi wa kijiji wakiwemo ndugu wa marehemu walianza kuwanyooshea vidole watu hao wawili wakisema ndiyo waliomuu na kuchukua uamuzi wa kuanza kuwapiga. Alifafanua kuwa kabla ya kuwazika wakiwa hai kundi la wanandugu hao waliwapiga wawili hao kwa marungu na mawe na kabla ya kuwaua wakawatupia kwenye kaburi moja na kuwafukia humo. Baada ya kuwazika wakiwa hai,kundi la wanandugu hao lilikwenda nyumbani kwa Ernest na kuiteketeza nyumba yake kwa moto. Mpaka anazungumza na mwandishi wa habari hizi shughuli ya kufukua miili ya watu hao ilikuwa ikiendelea kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi ambapo alifafanua kuwa baada ya uchunguzi huo kila mwili utazikwa kwenye kaburi lake. Aidha kamanda huyo alisema mpaka sasa watu wawili wanashikiliwa ambapo inasadikiwa kuwa ndiyo waliongoza kundi lililotenda ukatili huo lakini hakuwataja kutokana na sababu alizosema ni za kiusalama. Hii si mara ya Kwanza kwa matukio ya watu kuzikwa wakiwa hai kwa tuhuma za uchawi mkoani Mbeya kwani mwaka jana pia matukio hayo yalikuwa yakielewa kufanyika kwa usiri mkubwa lakini ilikuja kubainika siku ambayo Chifu Merere wa kabila la Wasangu aliponusurika kuzikwa akiwa hai na wakazi wa kijiji cha Ruiwa wilayani Mbarali.

Tuesday, January 8, 2013

MBEYA TAYARI KWA LIGI MKOA

HATIMAYE cha soka mkoani Mbeya(MREFA) kimetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa michuano ya ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa ambapo sasa itaanza kutimua vumbi Januari 19 mwaka huu. Katibu wa Mrefa Seleman Haroub amesema kuwa kuchelewa kuanza kwa ligi hiyo iliyopaswa kuanaza Septemba mwaka jana kulitokana na uongozi mpya kukuta chama hakina fedha za kuendeshea ligi ulipoingia madarakani. Hata hivyo alisema kufuatia ukata unaokikabili chama pamoja na vilabu 17 vitakavyoshiriki uendeshaji wa ligi hautakuwa wa michezo ya nyumbani na ugenini kama shirikisho la soka nchini TFF lilivyoagiza badala yake itaendeshwa kwa mtindo wa ligi katika vituo. Alisema timu shiriki zimegawanywa katikaa makundi mawili ya A na B ambapo kundi A zipo timu za Airpot Rangers na Eleven Boys za Mbeya mjini,Kimondo Sc na Hollywood za wilayani Mbozi,Masukuru FC na Muungano FC za wilayani Rungwe,Boma FC ya Kyela na Chemchemu FC ya Chunya. Kwa upande wa kundi B zipo Juhudi FC na Wenda FC za Mbeya vijijini,Black Scopion na Magereza Ruanda za Mbeya mjini,Tukuyu Stars ya Rungwe,Mahongole FC ya Mbarali,Biashara FC ya Chunya na Ichenjezya Boys ya Mbozi. Alisema ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa ngao ya hisani kati ya Boma Fc ya Kyela na Eleven Boys ya Mbeya mjini zilizoshika nafasi za juu katika ligi hiyo mwaka jana huku akisisitiza kuwa bingwa wa mkoa katika msimu uliopita timu ya Tenenda imeshushwa daraja baada ya kusambaratika ilipotoka kuuwakilisha mkoa katika ngazi ya kanda.

Friday, January 4, 2013

WAWILI WAUAWA KIKATILI MBEYA

WATU wawili wameuawa katika matukio mawili tofauti likiwemo na mkee kuuawa kwa kukatwa mapanga na mumewe akimtuhumu kuwa mshirikina.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani athuman amemtaja Marehemu katika tukio hilo kuwa ni Lena Mbughi(34) huku mtuhumiwa wa mauaji hayo amabye ni mume wa marehemu akitajwa kwa jina la Israel Kayuni. Kamanda Athumani alisema mwili wa marehemu Lena ulikutwa chumbani kwake katika kitongoji cha Sambandolo kijijini Ipapa kata ya Ipunga wilayani Mbozi mnamo Januari 3 mwaka huu majira ya saa nane za mchana. Alisema karibu na mwili huo kulikutwa panga na damu ambapo inasemekana mume ambaye alikimbia mara baada ya mauaji alimvizia mkewe aliyekuwa amejipumzisha katika mkeka na kumtendea unyama huo. Inasemekana kuwa kwa muda mrefu Kayuni alikuwa akimtuhumu mkewe lena kuawa anajihusisha na vitendo vya kishirikina na ndiyo sababu ya kuchukua uamuzi huo usiofaa kwani alipaswa kutumia njia za mazungumzo na si kujichukulia sheria mikononi. Katika tukio jingine dreva Taksi aliyefahamika kwa jina la Emanuel Mbembela(30) mkazi wa mtaa wa Sogea katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba amekutwa akiwa ameuawa na watu wasiofahamika na mwili wake kutupwa kichakani. Kamanda Athumani alisema mwili wa Emmanuel alikutwa Januari 2 mwaka huu majira ya saa 12:30 jioni kaika kichaka kilichopo jirani na Reli ya Tazara eneo la kijiji cha Mlowo barabara ya Mlowo Kamsamba. Alisema awali gari ya dreva tax huyo aina ya Toyota Spacio yenye namba T 381 BMT ilikodiwa na watu wasiofahamika na haikujulikana walimtaka awapeleke wapi hadi pale mwili wake ulipokuja kukutwa kichakani ukiwa na majeraha usoni na utosini. Kamanda Athumani alisema jeshi hilo linaendelea kuwasaka watuhumiwa wa matukio hayo yote na kuomba raia wema walio na taarifa za mahali walipo kulisaidia jeshi hilo.

Wednesday, January 2, 2013

HATARIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

MLINZI KATIKA MOJA YA MADUKA YALIYOPO ENEO LA KABWE JIJINI MBEYA AKIWA AMECHAPA USINGIZI ALIPOKUWA LINDONI KAMA ALIVYOKUTWA NA Lyamba Lya Mfipa.

KAZI YA POLISI MBEYA 2012

BAADHI YA VITU VILIVYOKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA MWAKA 2012
KAMANDA WA POLISI MKOANI MBEYA DIWANI ATHUMAN AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MBELE.MBELE YAKE NI BAADHI YA VITU VILIVYOKAMATWA NA JESHI HILO MWAKA 2012