Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, May 29, 2012

ADHA YA USAFIRI MBEYA-SUMBAWANGA RUKWA

MAANDALIZI UMISETA MBEYA YAIVA


TIMU shiriki za mashindano ya michezo mbalimbali kwa shule za Sekondari (UMISETA) mkoani hapa jumatano hii jioni zitaingia kambini tayari kwa mashindano hayo yatakayoanza kimkoa Mei 31 mwaka huu.

Afisa michezo mkoa wa Mbeya George Mbijima ameiambia LYAMBA LYA MFIPA kuwa mashindano hayo yataendeshwa kwa muda wa siku nne katika viwanja vya shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya na yatashirikisha timu kutoka halmashauri nane zilizopo mkoani hapa.

Mbijima amesema mashindano hayo pia yatalenga kuchagua wachezaji wa timu itakayouwakilisha mkoa katika mashindano ya Umiseta kanda ya nyanda za juu kusini yatakayofanyika mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Ameitaja baadhi ya michezo katika mashindano kuwa ni mpira wa miguu na mkono,wavu,riadha,kikapu,mpira wa meza ma bao yote hiyo ikiwa ni kwa wavulana na wasichana pamoja na mchezo wa netibal kwa wasichana pekee.

Afisa michezo huyo amesisitiza kuwa wachezaji wa timu shiriki ni lazima wawe wanafunzi katika shule za sekondari walio katika utaratibu maalumu unatambuliwa na serikali na si mamluki kutoka mitaani,vituo vya elimu binafsi wala wanaojiandaa kurudia mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne au cha sita.

Aidha,ametoa wito kwa wazazi na walimu kuwaruhusu watoto ama wanafunzi wao kushiriki mashindano hayo kwakuwa hiyo pia ni fursa ya wao kuonesha vipaji walivyonavyo na pia kwa kuzingatia umuhimu wa michezo katika afya za miili yao.

Monday, May 28, 2012

ZIWA TANGANYIKA

Katika ufukwe wa ziwa Tanganyika kijijini Kirando wilayani Nkasi mkoani Rukwa

WAJAWAZITO WAJIFUNGULIA GIZANI


WANAWAKE wajawazito wanaopata huduma zao katika kituo cha afya cha Kirando wilayani hapa wanalazimika kujifungulia gizani kufuatia uhaba wa mafuta kwaajili ya jenereta unaokikabili kituo hicho.Mwandishi mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Joachim Nyambo akizungumza na mama aliyekutwa anamlea mgonjwa ambaye ni mtoto wake katika wodi ya watoto kwenye kituo cha afya cha Kirando Uchunguzi uliofanywa na Lyamba Lya Mfipa na kuthibitishwa na uongozi wa kituo hicho umebaini wajawazito wanaotoka katika familia masikini kuwa na wakati mgumu mno wanapokwenda kujifungua kituoni hapo.

Hali hiyo inatokana na kila mjamzito ama mgonjwa yeyote anayelazwa katika kituo hicho ambacho wakazi wa vijiji vilivyopo pembezoni na ndani ya ziwa Tanganyika wanakiona kama hospitali ndogo kutakiwa kwenda na vibatali,karabai ama taa ya mafuta kutoka majumbani mwao.


Iwapo mgonjwa aliyelazwa kituoni hapo atakosa uwezo kabisa wa kuja na kibatari,karabai ama taa basi hulazimika kukaa gizani usiku kucha iwapo katika wodi alimolazwa hakutakuwa na mgonjwa mwingine anayetoka kwenye familia iliyo na unafuu wa kiuchumi.Victoria Mafulwa(Wa kwanza kulia) mwanamke aliyelazimika kufanyiwa upasuaji baada ya mimba yake kuharibika kutokana na kuchelewa kufikishwa katika kituo cha afya akitumia usafiri wa boti ya kukodi akizungumza na Lyamba Lya Mfipa 
 
Uchunguzi wa kina wa Lyamba Lya Mfipa pia umebaini hali kuwa mbaya kwa wagonjwa hususani wajawazito wanaokwenda hapo na kutakiwa kufanyiwa upasuaji ambapo pia hutakiwa kununua mafuta ya jenereta ndipo wahudumiwe na iwapo watakosa basi huwa na wakati mgumu iwapo hawatojitokeza wasamalia wema kuwachangia.

KWA MWENDELEZO WA HABARI HII ENDELEA KUTEMBELEA Lyamba Lya Mfipa ..............

Saturday, May 26, 2012

YATIMA 140 KUPEWA KITUO


WATOTO zaidi ya 140 walio yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika jijiji cha Mahango wilayani Mbarali wanatarajiwa kunufaika kwa kupata malezi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo kinachojengwa kijijini hapo.

Ujenzi wa kituo hicho unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali na lisilo na maslai yoyote la  “BEZMANY” la  nchini Czech Republic utagharimu zaidi ya shilingi milioni 170.

Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa,mwakilishi wa Bezmany katika nchi zilizopo barani Afrika Chriss Zacharia, alisema lengo la kujenga kituo hicho ni kuwasaidia watoto wa aina hiyo aliosema takwimu zinaonesha uwepo wao kwa wingi kijijini hapo.

Alisema tayari fedha hizo zimeanza kutumika kwa ujenzi wa bweni la wavulana ambalo mpaka sasa limegharimu shilingi milioni 90.

Alifafanua kuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bweni hilo utafuata ujenzi wa sehemu ya chakula,jiko na stoo  utakao gharimu milioni 29 na pia bweni la wasichana litakalogharimu shilingi milioni 55.

 “Kwa ujumla tunataraji kuwa na mabweni mawili kwaajili ya wavulana na wasichana.Kila bweni litakuwa na uwezo wa kuchukua watoto 70 kwa wakati mmoja” alisema Zacharia.

Zacharia alisema shirika halitoishia katika ujenzi pekee bali lipo tayari kugharamia chakula,mavazi na malazi kwa watoto wote watakaoishi kituoni hapo.

Alizitaja huduma nyingine zitakazogharimiwa na shirika kuwa ni  pamoja na kutoa elimu bora,afya na kuwaandaa watoto kuingia kwenye jamii kwa maisha yao ya baadae.

Alisema tayari shirika hilo likishirikiana  na ubalozi wa Marekani limeweza kufungua shule ya awali ya Kajunjumele Nursery School kwa ajili ya watoto yatima wenye umri  kuanzia miaka3-6 wanao jifunza kusoma,kuandika na somo la hisabati.

Alisema,  katika mradi wa kusaidia shule shirika limeweza kununua madawati kwa shule za Mahango na Simike jijini Mbeya na,kufanya  ukarabati  wa madarasa katika shule za msingi kama vile kisa wilayani Rungwe,Galula wilayani Chunya na Ilasilo Mbeya Vijijini

ADHA YA USAFIRI-MBEYA/SUMBAWANGA

TULIPOJIKUTA TUNACHEKANA KAMA NYANI WANAVYOCHEKANA MIKIA.

Friday, May 25, 2012

WAJASIRIAMALI MBARALI WAFUNDWA


WAJASIRIAMALI wilayani Mbarali wametakiwa kufanya shughuli zao kwa misingi inayotarajiwa kubadilisha muonekano wao kutoka walipo na kupiga hatua zaidi kimaendeleo.

Kaimu mkuu wa wilaya ya Mbarali Moses Mashala ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya wajasiriamali wilayani humo yaliyoandaliwa na chama cha wafanyabiashara,wenye viwanda na wakulima(TCCIA) mkoa wa Mbeya.

Bwana Mashala amesema lengo la serikali pamoja na wadau wengine ni kuona kunakuwepo na mabadiliko katika shughuli za kibiashara zinazofanywa na wajasiriamali nchini hivyo ni changamoto kwa kila anayepata fursa ya kupewa mafunzo kama hayo.

Naye mwenyekiti wa TCCIA mkoani humo Julius Kaijege alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha vijana na waanawake kuondokana na makundi yanayohatarisha maisha yao kwa kujikita katika ujasiriamali.

Mafunzo hayo yaliyoshirikisha jumla ya wajasiriamali 45 yalilenga utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mishumaa pamoja na sabuni.