WAJASIRIAMALI
wilayani Mbarali wametakiwa kufanya shughuli zao kwa misingi inayotarajiwa
kubadilisha muonekano wao kutoka walipo na kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
Kaimu
mkuu wa wilaya ya Mbarali Moses Mashala ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo
ya siku nne ya wajasiriamali wilayani humo yaliyoandaliwa na chama cha
wafanyabiashara,wenye viwanda na wakulima(TCCIA) mkoa wa Mbeya.
Bwana
Mashala amesema lengo la serikali pamoja na wadau wengine ni kuona kunakuwepo
na mabadiliko katika shughuli za kibiashara zinazofanywa na wajasiriamali
nchini hivyo ni changamoto kwa kila anayepata fursa ya kupewa mafunzo kama
hayo.
Naye
mwenyekiti wa TCCIA mkoani humo Julius Kaijege alisema lengo la mafunzo hayo ni
kuwawezesha vijana na waanawake kuondokana na makundi yanayohatarisha maisha
yao kwa kujikita katika ujasiriamali.
Mafunzo
hayo yaliyoshirikisha jumla ya wajasiriamali 45 yalilenga utengenezaji wa bidhaa
mbalimbali ikiwemo mishumaa pamoja na sabuni.
No comments:
Post a Comment