Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, May 7, 2012

MBUNGE MWANJELWA AKANUSHA KUTANGAZA KUHAMIA CHADEMA

MBUNGE wa viti maalumu (CCM) mkoani Mbeya Mary Mwanjelwa amepinga kutoa kauri za kuonyesha nia ya kukihama chama chake na kuhamia katika chama cha demokrasia na maendeleo.
 
Tamko la Mwanjelwa alilolitoa kwa waandishi wa habari leo(Mei 7) na gazeti moja la hapa nchini kumkariri kuwa ana niaa ya kukihama chama chake kutokana na rais Jakaya Kikwete kuteua wabunge ndani ya muda mfupi na kuwapaa nafasi ya uwaziri.

Gazeti hilo lilimkariri mbunge huyo ambaye ndiye kipindi chake cha kwanza kuwa miongoni mwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania akisema uteuzi wa rais Kikwete kwa mawaziri haukumridhisha kwakuwa wapo wabunge akiwemo yeye waliopaswa kupewa wadhfa huo kwakuwa wabunge wa muda mrefu.

Lakini Mwanjelwa anakanusha kuzungumzia suala la yeye kuhama na kusisitiza kuwa habari zilizoandikwa si za kweli na kulitaka gazeti lililochapisha habari hiyo kuomba radhi kabla hajachukua hatua za kisheria dhidi ya mwandishi wa habari hizo pamoja na kampuni husika.

No comments:

Post a Comment