Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, June 23, 2015

Mafunzo ya uandishi wa habari za SDGs na Mabadiliko ya tabia ya nchi yaendelea

 Washiriki wa Mafunzo ya uandishi wa habari za SDGs na Mabadiliko ya tabia ya nchi wakijadili jambo kwa pamoja katika ukumbi wa Tanzania Media Fund jijini Dar es salaa.Mafunzo haya yamefadhiliwa na shirika la Reuters


 Mkufunzi Royston Martin akifuatilia jambo katika mtandao wakati mafunzo yakiendelea.

 Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Bw.Joachim Nyambo(Kushoto) akifuatilia jambo katika mtandao ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.



Thursday, June 18, 2015

TANZIA TANZIA TANZIA! MTANGAZAJI TBC AFARIKI DUNIA!




Mtangazaji wa TBC Florence Dyauli amefariki dunia leo asubuhi jijini DSM.

Florence ni mwandishi wa habari wa muda mrefu, alikuwa mtangazaji wa RTD sasa TBC Taifa,...Mmoja wa watangazaji waanzilishi wa TVT sasa TBC1.

Florence alisifika kwa kudhibiti matamshi ya maneno wakati akisoma taarifa za habari pia alikuwa mtangazaji mahiri kwa matangazo ya OB (Outside Broadcasting)

Mipango ya mazishi inaedelea DSM. Mungu ailaze roho ya Florence Dyauli Mahali pema peponi Amina.
 

Wednesday, June 17, 2015

ILEMBO,MASOKO WASHEREHEKEA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA MDAHALO,WAZAZI WALAUMIWA

 Wadau mbalimbali waliohudhuria mdahalo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wakitokea katika kata za Ilembo na Masoko wilayani Mbeya wakiwa kwenye piacha ya pamoja.
 Mratibu wa GBV na VAC Patrick Kossima akiimba na kucheza na wanafunzi waliohudhuria mdahalo kijijini Ilembo


 
 Mwanafunzi Sylivia Lugano akichangia mada kwenye mdahalo huo ulioandaliwa na kanisa la Anglikana kupitia mradi wa GBV na VAC unaofadhiriwa na shirika la Watereed.

 Afisa mtendaji wa kata ya Masoko Joseph Lupama akizungumza jambo kwenye mdahalo.
 Mratibu wa GBV na VAC Patrick Kossima akitoa zawadi kama motisha kwa wanafunzi waliowahi kufanya vizuri katika masomo yao shuleni wakapewa zawadi na shule lakini wazazi hawakuwapa zawadi wakati huo






WAZAZI na walezi wilayani Mbeya wametajwa kuwa hufurahia mno pale watoto wao wanaposimamishwa masomo shuleni kwa kutolipa michango wakijua ni wakati muafaka wa kuwatumikisha watoto hao katika shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo.

Tabia hiyo ya wazazi imetajwa kuwa kikwazo kikubwa katika ustawi wa taaluma ya watoto wilayani hapa hali inayozua changamoto kwa wadau wa maendeleo kuona umuhimu wa kuingilia kati ili kuinusuri jamii ya watoto wilayani hapa.

Wanafunzi,walimu na wazazi kutoka kata za Ilembo na Masoko wilayani Mbeya walibainisha kuwepo kwa hali hiyo kwenye mjadala wa pamoja ulioandaliwa na Kanisa la Anglikana kupitia mradi wa Kupinga Ukatili wa kijinsia(GBV) na ukatili dhidi ya watoto(VAC) ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

Wadau hao walisema kutokana na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa elimu,wazazi wengi wamekuwa wakiwanyima fursa watoto wao kwenda shule na badala yake kuwatumikisha mashambani wakiamini kuwa kilimo kina manufaa makubwa ndani ya familia zaidi ya Elimu.

Walisema kutokana na uelewa huo mdogo wazazi hupuuzia sula la kulipa michango mbalimbali wakisubiri uamuzi wa uongozi wa shule kuwasimamisha kwa muda wanafunzi na hapo ndipo wazazi na walezi hao hufurahia kwakuwa hupata sababu ya kuendelea kuwatumikisha watoto mashambani.

“Unapofukuzwa shule kwakuwa hujatoa mchango na kurudi kwa mzazi,mzazi anakwambi hakuna pesa nenda shambani kwani shule inakusaidia nini.Kwao inakuwa ni sherehe lakini wanasahau kuwa tunakosa haki yetu ya msingi” alisema mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Ilembo Jemedari Ezekiel.

“Hata unapokwenda kumuomba mzazi daftari au kalamu jambo la kwanza atakwambia kwanza ukafanye kazi shambani kwake au kwa jirani ili pesa utakayolipwa ndiyo ukanunue mahitaji yako” aliongeza Jemedari.

Nao wali Gabriel Mwandembo kutoka shule ya msingi Mumba na Valina Kamumyana wa shule ya sekondari Ilembo walisema ushiriki mdogo wa wazazi katika kufuatilia taaluma ya mwanafunzi umekuwa ukisababisha watoto wengi kwenda shule kwa lengo la kuhitimu tu darasa la saba na si kupata elimu ya kumsaidia maishani mwake.

Kwa upande wake mratibu wa GBV na VAC Patrick Kossima alisema mijadala zaidi inahitajika ndani ya jamii ili kuwezesha kupanua wigo wa uelewa kwa wazazi hatua itakayosababisha kila upande kutambua wajibu wake na kuijenga jaii yenye upendo.

Kossima alisema kasoro zilizopo ndani ya jamii katika malezi ya mtoto ni miongoni mwa mambo yanayosababisha uwepo wa maambukizi mapya ya Virusi vya ukimwi japo ni wanajamii wachache wanaotambua jambo hilo.