SAKATA
la unyanyasaji aliofanyiwa mwanamke mjamzito Judith Komba siku ya kujifungua
katika hospitali ya Rufaa kitengo cha wazazi cha Meta limechukua sura mpya
baada ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kuagiza wauguzi waliokuwa zamu
siku ya tukio wachukuliwe hatua stahiki.
Mnamo
usiku wa Mei 13 mwaka huu mwanamke Judith Komba mkazi wa Iwambi jijini Mbeya
alijikuta analazimika kujifungulia katika kitanda cha kubebea wagonjwa ndani ya
hospitali ya Meta pasipo usaidizi wa mtu yeyote na mtoto kunusurika kifo
kutokana na mazingira hatari yaliyoukabili uzazi wake.
Hivi
karibuni Judith alikaririwa na vyombo vya habari akibainisha kuwa alilazimika
kujifungulia kwenye mazingira hayo baada ya kuwafuata mara kadhaa wauguzi
waliokuwa akiwaomba wamsaidie lakini walimpuuza na wakaendelea kulala kwenye
chumba chao.
Mwanamke
baada ya kuzidiwa na kujikuta hawezi kurejea wodini alikokuwa amelazwa
alijikuta analazimika kulala kwenye kitanda cha kubebea wagonjwa akiwa
amezidiwa na uchungu na akajifungulia hapo.
Hatua
hiyo imeonesha kusononesha wadau wengi akiwemo mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye
amemuagiza katibu tawal mkoa kufuatilia suala hilo na kuwachukulia hatua
stahili wauguzi waliokuwa zamu.
Kandoro
alitoa agizo hilo kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mpango wa miaka minne wa
Kusaidia maisha ya Akina mama wajawazito na Watoto kwa halmashauri 10 za mkoani
Mbeya unaofadhiliwa na shirika la Korea International Cooperation Agency(KOICA)
kupitia Unicef.
Kandoro
alisema yapo majibu rahisirahisi yaliyotolewa na utawala wa hospitali hiyo
lakini ukweli ni kuwa majibu hayo hayatoshelezi hata kidogo ikilinganishwa na
uzembe uliotokea siku hiyo.
“Majibu
yametolewa kirahisi rahisi.Mimi nasema siyakubali na naagiza katibu tawala
uhakikishe unafuatilia jambo hilo na waliohusika wawajibishwe.Kwani
hawafahamiki waliokuwa zamu siku hiyo?Kwa nini utawala utumie lugha rahisi
rahisi”
“Hatuwezi
kuruhusu mtu atoe matatizo yake nyumbani kwake ayalete kazini na kuwaumiza
wasio husika na matatizo hayo.Tumeambiwa hapa moja ya vitu vinavyochangia vifo
vya wajawazito na watoto wachanga ni uzembe wa watoa huduma.Hili lazima
tulifanyie kazi haraka” alisema Kandoro.
No comments:
Post a Comment