Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, August 30, 2015

MAKADA WALIOPAMBA KAMPENI ZA DK.MAGUFULI MKOANI MBEYA HAWA HAPA

 Dk.Mary Mwanjelwa ni Mbunge viti maalumu mkoa wa Mbeya.Anaamini ushindi wa Dk.Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao utakuwa wa kishindo na utawawezesha watanzania kuanza maisha mapya na yenye mabadiliko makubwa kimaendeleo.Hapa akizungumza na maelfu ya wakazi wa jiji la Mbeya kwenye mkutano wa Dk.Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya Ruandanzovwe.

Charles Mwakipesile-Alishika nafasi ya tatu katika kura za maoni ndani ya CCM kwa nafasi ya ubunge Mbeya mjini.Anasema Dk.Magufuli ni chaguo la watanzania walio wanaCCM na vyama vingine vyote vya siasa.Anaamini ushindi wa Dk.Magufuli upo tena wa kutosha.Hapa pia ni katika mkutano wa Dk.Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya Ruandanzovwe.

 Amani Kajuna-Alishika nafasi ya pili kwenye kura za maoni ubunge Mbeya mjini.Anasema yuko tayari kuunga mkono mgombea wa nafasi hiyo Sambweee Shitambala,mgombea wa urais Dk.John Pombe Magufuli na wagombea wa udiwani wote kupitia CCM.Ni katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Ruandanzovwe.
Wasanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Chege na Temba wanasema kwa Dk.Magufuli wapinzani lazima wakae.Ni walipowaburudisha wakazi wa jijini Mbeya katika mkutano wa Dk.Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya Ruandanzovwe.

Filipo Mulugo a.k.a ahadi umepata-Ni mgombea ubunge jimbo la Songwe.Anasema kwa Magufuli hapa kazi tu.Hapa ni katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya sabasaba mjini Chunya.


Dk.Harison Mwakyembe -Mgombea ubunge jimbo la Kyela.Anasema wagombea urais kupitia CCM na Ukawa wote amefanya nao kazi hivyo anawafahamu vizuri sana.Anasrma Dk.Magufuli ni chaguo sahihi.Hapa ni katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mjini Kyela.

John Mwakipesile-Mkuu wa mkoa wa Mbeya mstaafu.Anasema kwa kipindi cha miaka 10 hajafurahi ila sasa anafurahi.Anasema anamfahamu vizuri Dk.Magufuli na anaamini ndilo chaguo sahihi la watanzania.Anasema waliomzushia kuhamia Chadema walikosa kazi ya kufanya.Hapa ni katika mkutano wa Dk.Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mjini Kyela.

 
 

Saturday, August 29, 2015

MJUE DK.JOHN POMBE MAGUFULI.

Mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.

Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.
Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.

Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.
Aidha Dk.Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .

Alipohitimu,Dk.Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.

Dk.Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.

Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.

Alianza siasa mwaka 1995
Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.
Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.

Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.
Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.

Anatambulika kuwa Mchapa kazi
Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.

Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.
Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk John Magufuli alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.

Saturday, August 22, 2015

MBUNGE AHAMA VYAMA VITATU KWA WIKI MOJA

KATIKA kuonesha kinachopiganiwa  si kuwatumikia wananchi bali maslahi binafsi,aliyekuwa mbunge wa Mbarali mkoani Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Modestus Kilufi amejikuta anakuwa mwanachama wa vyama vitatu tofauti katika kipindi cha wiki moja akitafuta nafasi ya kutetea nafasi ya ubunge.

Safari ya kuhama kwa Kilufi ilianzia katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya ambapo mbunge huyo aliyemaliza muda wake aliutumia mkutano wa mgombea wa urais kupitia Chadema Edward Lowasa kutangaza kuhama rasmi CCM na kuhamia chama hicho baada ya kushindwa katika kura za maoni.

Hata hivyo makazi ya Kilufi ndani ya Chadema yakashindikana kuwa ya kudumu kwani pamoja na ushawishi wote alioufanya kwa uongozi ndani ya chama hicho katika ngazi za Taifa mkoa na wilaya alijikuta anagonga mwamba baada ya wafuasi wa chama hicho kumzuia kuingia ofisi ya msimamizi wa uchaguzi alipokwenda kuchukua fomu.

Taarifa kutoka Mbarali zinaeleza kuwa juzi kunako majira ya jioni(Agosti 20) wanachama wa Chadema walimzuia Kilufi kuingia kwenye ofisi za msimamizi kwakuwa walitaka nafasi hiyo ibakie kwa mgombea Liberatus Mwang’ombe ambaye tayari alikuwa amekwishachukua fomu baada ya kushinda kwenye kura za maoni ndani ya chama ambako Kilufi hakushiriki.

Baada ya kushawishiwa na kundi la wafuasi wake jana(Agosti 21) Kilufi aliiona Chadema si pahala sahihi tena na akajikuta anaangukia mikononi mwa chama cha ACT Wazalendo na majira ya saa nane mchana alikwenda kuchukua fomu ya kugombea kupitia chama hicho.

Akiwasiliana kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi,msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbarali Adam Mgoi alithibitisha Kilufi kuwa miongoni mwa wagombea nane waliochukua fomu kugombea ubunge na kubainisha kuwa amechukua kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Akizungumzia kuhama kwa mwanachama aliyedumu naye kwa takribani siku sita,mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mbeya Josef Mwachembe China alisema anamuona Kilufi kama msaliti anayeendeshwa na msukumo wa watu wachache.

China alisema Kilufi ni miongoni mwa wanasiasa wasio na msimamo na wasio wazalendo kwa taifa lao na ndiyo sababu anapigania maslahi yake binafsi badala ya maslahi ya watanzania wanyonge.

Mwenyekiti huyo ambaye juzi alionekana kutwa nzima wakiwa na Kilufi katika mitaa mbalimbali ya jiji la Mbeya wakifanya mikakati ya mapinduzi ya mgombea wa ubunge Mbarali kupitia Chadema alikana uongozi kununuliwa na mbunge huyo ili ushinikize kumkabidhi nafasi ya kupeperusha bendera ya chama kwenye uchaguzi.

Hata hivyo China alikiri kuwa maagizo ya chama kumpokea Kilufi yalitokea ngazi ya juu yaani makao na kamwe haikuwa ridhaa ya wanachadema wilaya wala mkoa na ndiyo sababu hata uongozi wa Chadema ngazi ya kanda haukuwa na taarifa.

Hata hivyo ujio ndani ya ACT ulionekana kuleta mkanganyiko kwa uongozi ngazi ya wilaya kwani ulipopigiwa simu ulionekana kugawanyika ambapo Mwenyekiti Anzuruni Rashid Anzuruni alisema anachojua ni kuwa mtu aliyechukua fomu kupitia chama hicho ni James Kamanga na Kilufi hamtambui huku katibu wake Erasto Sanga alithibitisha kumpokea Kilufi na kutengua uteuzi wa mgombea wa kwanza.


Thursday, August 20, 2015

REDBRIGED MBEYA YAJITIA MATATANI,POLISI WAHOJI NI JESHI GANI?



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.



 


       R.P.C                                                                                               Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                      Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572                                                                                                        S. L. P. 260,
Fax -+255252503734                                                                                                        MBEYA.
             tanpol.mbeya@gmail.com
Unapojibu tafadhali taja 
  
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
 PRESS CONFERENCE” TAREHE 18.08.2015.

KUFANYA KAZI YA ULINZI NA USALAMA ILIYOKASIMIWA KWA JESHI LA POLISI.

MNAMO TAREHE 14.08.2015 MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA ALIKUJA MKOA WA MBEYA AKIWA AMEANDAMANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA CUF, NCCR – Mageuzi NA NLD KWA DHUMUNI LA KUMTAMBULISHA NA KUOMBA UDHAMINI WA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA KWA NAFASI YA URAIS.

KATIKA MSAFARA WAKE KUTOKA UWANJA WA NDEGE [SONGWE] KULIONEKANA GARI MOJA AINA YA LAND CRUISER – PICK UP YENYE RANGI NYEUSI NA NDANI YAKE LILIKUWA LIMEBEBA VIJANA AMBAO WALIKUWA WAMEVAA MAVAZI MEUSI, KOFIA – BERETI NYEUSI NA MIWANI NYEUSI NA MABUTI. WATU HAO WALIKUWA NA MUONEKANO KAMA ASKARI NA SHUGHULI WALIYOKUWA WAKIFANYA YA KUONGOZA MSAFARA, ULINZI NA KAZI NYINGINE ZIFANYAZO NA JESHI LA POLISI.





KUTOKANA NA MUONEKANO WAO NA SHUGHULI WALIZOKUWA WAKIZIFANYA ILIKUWA IKITAFSIRIKA KUWA NI JESHI LIFANYAZO KAZI HIZO AMBALO HALIKUWA LIKIFAHAMIKA.
KUTOKANA NA SINTOFAHAMU HIYO WANANCHI WENGI WALIKUWA WAKIHOJI “HILO NI JESHI GANI” SAMBAMBA NA KUTUMA PICHA KWA NJIA YA MTANDAO WA KIJAMII [WHATSAPP] WAKIONYESHA WASIWASI WALIOKUWA NAO DHIDI YA KIKUNDI HICHO.
KUFUATIA HALI HIYO, OFISI YA MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOA WA MBEYA ILIFUNGUA JALADA LA UCHUNGUZI ILI KUWAPATA VIJANA WALE KWA LENGO LA KUWAHOJI NA KUKAMILISHA UPELELEZI ILI JALADA LIPELEKWE KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA UFAFANUZI WA KISHERIA. HII NI KUTOKANA NA KUIBUKA KWA MAKUNDI YA AINA HII HASA KWA VYAMA VIKUBWA VYA SIASA HAPA NCHINI.
KATIKA KUFANYA UFUATILIAJI HUO, WAPO WATU WAWILI WALIKAMATWA ALFAJIRI YA LEO TAREHE 18.08.2015 KWA MAHOJIANO NA BAADA YA MAELEZO YAO KUCHUKULIWA WALIPEWA DHAMANA. BAADHI YA VIONGOZI WAO WALIOKUJA POLISI WAMEELEZWA KUHITAJIKA KWA VIJANA WALE WALIOKUWA KATIKA GARI LILE ILI WAHOJIWE NA KUKAMILISHA UPELELEZI WA JALADA HILO MAPEMA ILI MWANASHERIA WA SERIKALI ALITOLEE MWONGOZO WA KISHERIA.


           Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Thursday, August 13, 2015

CRDB WAMEFIKAAAAAA!!!!!!

 Mhariri mkuu wa blogu ya Lyamba Lya Mfipa Bw.Joachim Nyambo akiwa na mfano wa kadi ya malipo katika huduma za afya.


 Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Dk.Charles Kimei akizungumza na waanyakazi katika hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya.
 Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Dk.Charles Kimei na Kaimu mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya Myriam Msalale wakiwa na mfano wa kadi itumikayo kulipia malipo kwaajili ya huduma za afya.
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Dk.Charles Kimei na Kaimu mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya Myriam Msalale wakiwa na watumishi wengine wa hospitali hiyo wakiwa na mfano wa kadi itumikayo kulipia malipo kwaajili ya huduma za afya