Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, May 28, 2017

SIMBA WAPATA AJALI WAKIRUDI DAR ES SALAAM KUTOKA DODOMA






Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Gari aina ya Land Cruiser iliyokua imebeba wanachama kadhaa wa timu ya Simba na pia Nahodha wa Simba Jonas Gerrard Mkude ikitokea Dodoma kuelekea Dar Es Salaam imepinduka na kuharibika vibaya, maoneo ya Dumila.



Taarifa za awali zinadai kuwa Wanachama hao wa Simba hali zao ni mbaya lakini mmoja wao aliyetajwa kwa jina la Shose anaeonekana katika picha mbili hapo juu amefariki dunia.
Jonas Mkude(katika picha hapo juu) yuko vizuri na yuko na majeruhi wenzake katika hospitali ya mkoa Morogoro wanakoendelea kupata matibabu.


Hao unaowaona katika picha za juu zaidi ni Mashabiki waliokua kwenye Magari Mengine

Thursday, May 25, 2017

Ratiba ya Sportpesa Super Cup


YANGA WALIVYOPOKELEWA BUNGENI BAADA YA KUETEA UBINGWA VPL

 Wabunge mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa pamoja na viongozi na wachezaji wa timu hiyo nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
 Wabunge mashabiki wa timu ya Yanga wakishika kombe pamoja na viongozi na wachezaji wa timu hiyo nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.

Wabunge mashabiki wa timu ya Yanga wakinyanyua kombe kwa furaha.

Wednesday, May 24, 2017

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo


KAMPENI YA UTALII KUFANYIKA JIJINI MBEYA LEO

 Afisa uhusiano mkuu wa Bodi ya Utalii nchini,Geofray Tengeneza akizungumza na waandishi wa Habari jijini Mbeya jana juu ya Kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani iliyopewa njina la Utalii wa ndani uanze na mtanzania mwenyewe ambayo itaendeshwa katika mikoa mine ya Kigoma,Iringa,Mbeya na Mwanza.
 Kwa mkoani Mbeya kampeni inafanyika leo latika viwanja vya chuo cha uhasibu TIA majira ya jioni. hakuna kiingilio watu nyote mnakaribishwa.

 Tengeneza anasema baada ya kampeni katika mikoa ya Kigoma na Iringa sasa ni zamu ya mkoa wa Mbeya na itamalizimia mkoani mwanza lengo likiwa ni kukutana na makundi mbalimbali ya watanzania na kuwaeleza umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo.

Tuesday, May 23, 2017


UMITASHUMITA ILIVYONOGA KATIKA KATA YA IGALE

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Usongwe lililopo Mbalizi Wilayani Mbeya,Idd Omary akikabidhi mipira mitano kwa Mratibu Elimu Kata ya Igale,Ezekia Masebo kwaajili ya Mashindano ya Michezo ya wanafunzi wa Shule za msingi(Umitashumita) kwenye hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo katika ngazi ya kata jana
 Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Usongwe lililopo Mbalizi Wilayani Mbeya,Idd Omary akizindua kwa kupiga penati Mashindano ya Michezo ya wanafunzi wa Shule za msingi(Umitashumita) ngazi ya kata ya Igale 


Mratibu Elimu Kata ya Igale,Ezekia Masebo akizungumza jambo kabla ya kuzinduliwa kwa mashindano

Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Michezo ya wanafunzi wa Shule za msingi(Umitashumita) kata ya Igale,Mwalimu Atupakisye Jabir.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Usongwe lililopo Mbalizi Wilayani Mbeya,Idd Omary akizungumza na wanafunzi,walimu na wazazi waliofika kushuhudia michezo mbalimbali.



 Afisa biashara wa Benki ya NMB Tawi la Usongwe lililopo Mbalizi Wilayani Mbeya,Yusuf Ahmed Juma akizungumza jambo na kuahidi kuzitembelea shule zote kuzungumza na walimu na wanafunzi juu ya umuhimu wa kuhifadhi fedha benki badala ya kuweka kwenye kibubu. 




MIUNDOMBINU duni na ukosefu wa vifaa vya michezo katika Shule mbalimbali wilayani Mbeya imetajwa kuwa changamoto inayokwamisha jitihada za kuendeleza sekta ya michezo mashuleni.

Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Michezo ya wanafunzi wa Shule za msingi(Umitashumita) kata ya Igale,Mwalimu Atupakisye Jabir alibainisha hayo alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya michezo mashuleni kwenye uzinduzi wa mashindano hayo jana.

Mwalimu jabiri alisema miundombinu ya michezo ni duni na iliyopo haiko katika hali nzuri huku akisema pia vifaa vya michezo kama mipira,sare,nyavu,filimbi,saa za michezo na ngoma havitoshelezi.

Alisema pia kutokana na ukosefu wa usafiri kwaajili ya shughuli za michezo mashuleni,walimu na wanafunzi wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kwa miguu pale yanapoandaliwa mashindano au michezo ya kirafiki kati ya shule moja na nyingine au shule za kata moja na nyingine.

“Zipo shule hata baadhi ya viwanja hakuna hasa vya netiboli,wavu na mpira wa mezani.Hata vimiko vya kupigia mpira wa mezani hatuna.Lakini kutokana na ukosefu wa bajeti kwaajili ya usafiri tunalazimika kutembea kwa miguu.Tunapokwenda kwenye mashindano ya tarafa au wilaya tunakosa nauli hata ya daladala kutoka kwenye kata yetu hadi yanakofanyika mashindano husika” alisema Mwalimu Jabiri.

Aliwasihi wadau mbalimbali kuona uwezekano wa kuzisaidia shule katika tasnia ya michezo kwakuwa mashuleni ndiko kuliko na msingi bora wa kuwapata wachezaji wazuri wanaoweza kuliwakilisha taifa katika mashindano mbalimbali kama inavyoonekana hivi sasa kwa timu ya Serengeti Boys ambayo sasa ni gumzo ndani nan je ya nchi.

Akifungua mashindano ya Umitashumita katika ngazi ya kata ya igale inayoshirikisha jumla ya shule tano za msingi,Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Usongwe lililopo Mbalizi Wilayani Mbeya,Idd Omary sambamba na kukabidhi msaada wa mipira mitano aliahidi kuendelea kushirikiana na shule zote wilayani hapa katika suala la michezo lengo likiwa ni kushiriki kuibua na kukuza vipaji vya michezo.

Omary alisema pamoja na faida nyinginezo lukuki za michezo,NMB inatambua kuwa nidhamu ya mtumishi yeyote kazini inatokana na msingi bora uliojengwa tangu angali mdogo hivyo kwa mwanafunzi kushiriki michezo ni sehemu ya kujifunza nidhamu bora.

“Michezo,taaluma na nidhamu vinakwenda pamoja hii ndiyo sababu mwisho wa siku hapa tutakuja kupata viongozi na watumishi na hata wachezaji wakubwa walio na nidhamu.Michezo ni sehemu muhimu sana kwa umri wenu.Wapo wazazi na walezi wasiotaka kutoa fursa kwa watoto kushiriki michezo,hii si sawa tuwape fursa watoto hawa” alisema Omary.

Aliwasihi wanafunzi kutoitumia fursa ya michezo kujiingiza katika masuala ya matumizi ya dawa za kulevya na ulevi kwakuwa kufanya hivyo kunaweza kuwasababishia kutofikia malengo yako kimichezo na hata kitaaluma.

Kwa upande wake Afisa Elimu Utamaduni wilaya ya Mbeya,Ashanuru Malange alisisitiza umuhimu wa Michezo mashuleni akisema Mwili wenye Afya huleta Akili yenye afya na ili afya ipatikane ni lazima mwili husika ufanye mazoezi.

Shule zinazounda mashindano ya Umitashumita katika kata ya Igale yatakayotoa timu kwaajili ya kushiriki mashindano hayo kwenye ngazi ya wilaya ni pamoja na shule ya msingi Igale,Izumbwe I,Shongo,Itaga na Horongo.

UWEZESHAJI MDOGO WA MAAFISA USHIRIKA CHANZO CHA KUDOROLA VYAMA VYA USHIRIKA

UWEZESHAJI mdogo unaofanywa na Halmashauri kwa Ofisi za Maafisa Ushirika umetajwa kuwa chanzo cha Migogoro mingi ya kiutendaji ndani ya Vyama mbalimbali vya ushirika nchini.

Hayo yamebainishwa na Menejimenti na wajumbe wa Bodi ya Chama kikuu cha Ushirika cha wakulima wa Tumbaku Wilayani Chunya(CHUTCU) waliohudhuria Semina ya Programu ya kuwajengea uwezo wa Kitaasisi kwa viongozi na wadau wa ushirika ikiwa ni mwendelezo wa utoaji mafunzo hayo kwa wadau wa zao la Tumbaku.

Meneja mkuu wa CHUTCU,Bakari Kasia alisema vyama vingi vya ushirika vinaingia kwenye migogoro kutokana na usimamizi legelege wa Maafisa Ushirika ambao wengi wamekuwa wakijitokeza pale migogoro inapokuwa mikubwa.

Alisema wengi wa maafisa Uhirika wamekuwa kama watu wanaosubiri mambo yaharibike na kasha wao kuja kuwakamata na kuwaweka mahabusu viongozi jambo linalokinzana na wajibu wa nafasi zao wa kutembelea vyama hivyo  mara kwa mara ili kujua mwenendo mzima wa kiutendaji.

“Tunatambua Maafisa hawa si wakaguzi lakini wanapaswa kuvitembelea vyama hivi mara kwa mara ili panapoonekana kuwepo na dalili za mgogoro basi uthibiti wa haraka ufanyike kabla mambo hayajawa makubwa.Lakini kwa sasa wamebaki kusubiri palipo na mgogoro mkubwa ndipo wanaonekana kuja na kuwakamata viongozi na kuwaweka ndani.Siku zote wasimamizi wakiwa legelege vyama navyo vitakuwa legelege” alisema Kasia.

Hata hivyo Kasia alisema utekelezaji huo legelege wa Maafisa Ushirika unatokana na Halmashauri zao kutowawezesha ipasavyo ili kuvifikia vyama vilivyopo kwenye maeneo yao na hivyo kuwasababishia wabaki ofisini wakiwa hawana kazi za kufanya.

Alisema jambo la kushangaza ni kuwa Waajiri wa maafisa hao wasiowapa hata pikipiki za kutembelea ili kuwafikia wateja kwa urahisi,inapotokea migogoro mikubwa kwenye vyama wamekuwa wakiwaagiza kwa ukali kwenda kufuatilia na ufuatiliaji wenyewe unakuwa wa kamata kamata.

Kwa upande wake Kaimu Mrajisi msaidizi wa mkoa wa Songwe ambao pia una vyama wanachama wa CHUTCU kupitia wakulima wa Tumbaku waliuopo wilayani Songwe,Marton Mtindwa alikiri Ofisi nyingi za Maafisa Ushirika kuwa katika hali ngumu kutokana na Halmashauri zao kutotenga bajeti kwaajili ya utekelezaji majukumu yao.

Mtindwa alisema Halmashauri zinazotoa kipaumbele na kutenga bajeti kwaajili ya maafisa ushirika ni zile tu ambazo zinaona kuna mafanikio makubwa yaliyokwisha patikana kupitia vyama vya ushirika vilivyopo na hasa zile zilizopo kwenye maeneo ya kilimo cha mazao makubwa ya biashara kama Tumbaku na Kahawa.

“Kinachopaswa kufanyika kwa Afisa ushirika anaeona halmashauri haimpi kipaumbele kumtengea bajeti ni yeye mwenyewe kujiongeza.Kama ni kuandaa maandiko na kutafuta fedha sehemu yoyote ikiwemo kwa wadau ni yeye kama ni kumshawishi mwajili kwa kutengeneza hoja zenye mvuto ni yeye.Hata sisi warajisi wasaidizi tunalazimika kufanya hivyo” alisema Mtindwa.

Akifungua Semina hiyo ya siku Mbili,Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika nchini Titto Haule kwa mikoa ya Mbeya na Songwe ni wilaya Mbili pekee za Chunya na Songwe ambazo vyama vya Ushirika walau vinaonekana kuwa na Ustawi mzuri lakini wilaya nyingine zote zinazosalia hali si nzuri na inahitajika jitihada za dhati na za ushirikiano wa pamoja kujenga Ushirika.

Haule alisema mpango wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini ni kuona unafanyika Uhakiki wa vyama vya ushirika vilivyo hai nchini ili kuweka mikakati ya kufufua vilivyo kufa na pia kuanzisha vingine vipya lakini sasa vyama vyote vikiwa katika mtazamo wenye kuleta maendeleo kwa wananchi na si wajanja wachache.

Saturday, May 20, 2017

BODI,KAMATI ZA SHULE MBEYA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MAJUKUMU YAKE

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza kwenye Kongamano la Elimu lililowakutanisha wadau wa sekta hiyo wilayani Kyela.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Dokta Hunter Mwakifuna akizungumza jambo kwa wadau wa Elimu kwenye mdahalo.
Wadau wa Sekta ya Elimu wilayani Kyela mkoani Mbeya wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa huo,Amos Makalla kwenye Kongamano la Elimu.



Diwani wa kata ya Itunge wilayani Kyela,Cecilia Jimmy akichangia mjadala wa Elimu katika Kongamano la Sekta ya Elimu lililofanyika mjini Kyela.
Mratibu Elimu kata ya Kyela wilayani Kyela mkoani Mbeya Ester Richard akichangia mjadala wa Elimu katika Kongamano la Sekta ya Elimu lililofanyika mjini Kyela. 

BODI na Kamati za Shule mkoani Mbeya zimeagizwa kutekeleza majukumu zilizopewa ikiwemo kuwawajibisha wanafunzi wanaokwenda kinyume na sharia,kanuni na tararibu za shule ili kurejesha nidhamu mashuleni.

Agizo hilo lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla kwenye Kongamano la Elimu wilayani Kyela ambapo amebainisha kuwa utovu wa nidhamu mashuleni ni moja kati ya changamoto zinazokwamisha maendeleo ya kitaaluma.

Makalla amesema jambo la kusikitisha ni kuwa wanafunzi wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya Utovu wa nidhamu mashuleni huku wajumbe wa Bodi na kamati za shule husika wakishuhudia kwa macho yao lakini hakuna hatua stahiki wanazochukua kama vyombo vilivyopewa wajimu wa kusimamia taasisi hizo.

Mkuu huyo wa mkoa pia ameonesha kusikitishwa na tabia za baadhi ya wazazi wanaokuwa na upendo uliopitiliza kwa watoto wao kiasi cha kuingilia utendaji wa walimu shuleni pale wanapowawajibisha wanafunzi.

Amesema wapo wazazi ambao malezi yao yamesababisha watoto kuwa legelege kwa kulelewa kama mayai na kuwasababishia walimu kukosa sauti juu ya watoto husika kwani pale wanapokosea na kuwajibishwa mashuleni wazazi huja juu na kwenda kuwakalipia walimu.

Aidha Makalla amesema ipo haja ya kurejeshwa kwa mfumo wa elimu ya kujitegemea ili kuwajengea wanafunzi mfumo wa kupenda shughuli mbalimbali za kujiingizia vipato wakiwa bado shuleni na kubainisha yuko yupo tayari kuwajibika iwapo itaonekana alikosea kurejesha mfumo huo.