Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, October 10, 2011

Kandiro-Jiulizeni mpo kufanya nini




MKUU WA mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka madiwani na watendaji katika halmashauri za wilaya kila mmoja kujiuliza yupo katika nafasi yake kwaajili ipi.

Kandoro amesema kwa kufanya hivyo kila mmoja alipo ataweza kutambua wajibu wake na kuhakikisha anautekeleza akilenga kuyabadili maisha ya wananchi waliomwajiri.

Mkuu huyo wa mkoa,aliyasema hayo juzi(Oktoba 10) katika kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ileje kilicholenga kujadili taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali CAG.

Alisema wapo baadhi ya madiwani na watendaji ambao wamekuwa wakiyasahau majukumu yao na kujikuta wanaendekeza siasa katika kila wanalofanya pasipo kutambua kuwa kufanya hivyo kunawacheleweshea maendeleo wananchi katika maeneo yao.

Aliwataka madiwani kuhakikisha wanakuwa na mshikamano katika kutafuta sukluhu za changamoto zinazowakabili wananchi badala ya kuendeleza makundi yaliyotokana na kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Kandoro alisema ushirikiano wa pamoja baina ya wadau hao kwa kushirikiana na wananchi ndio unaoweza kuongeza kipato cha mwananchi mmojammoja ambaye kwa mafanikio hayo ataweza kuuchangia uchumi wa wilaya hiyo na kuiondoa katika hali ya utegemezi wa asilimia 98 ya bajeti yake kutoka serikali kuu.

Alisema ni vema wadau hao wakaona aibu kwa halmashauri yao kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa asilimia mbili pekee wakati ambao mkakati wa serikali ni kuona halmashauri zinajitegemea kwa asilimia 50.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Glads Dyamvunye alisema ukosefu wa vyanzo vya mapato ni changamoto kubwa kwa halmashauri yake hali inayopelekea kuendelea kuwa tegemezi kwa serikali kuu.


Sunday, October 9, 2011

Mbunge Kirufi Siku alipokamatwa ofisini kwake






Safari yangu kijijini Luhanga wilayani Mbarali




Kijiji kunufaika na uwekezaji


 
SERIKALI ya kijiji cha Luhanga wilaayani Mbarali imesisitiza kuwa uwekezaji wa kilimo unaolengwa kufanywa na Umoja wa wakulima wa Luhanga unalenga kuwanufaisha wakazi wa kijiji hicho na haupo kwa maslahi ya watu binafsi.

Uongozi wa kijiji hicho umesema makubaliano ya mkataba na umoja huo ni pamoja na umoja kutekeleza mambo makuu matatu ikiwemo kujenga ofisi ya kisasa ya kijiji,kuleta maji kijijini hapo kwaajili ya matumizi ya kilimo pamoja na kulipia ardhi waliyopewa kwaajili ya shughuli zao.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Muhamed Msonsa alisema jana kuwa umoja huo utapaswa kulipa shilingi 5000 kwa kila hekari moja ya eneo walilopewa na kijiji hivyo kijiji kila mwaka kitakuwa kikikusanya jumla ya shilingi milioni 62 kwa hekari 5000 zilizotolewa.


Kwa upande wa afisa mtendaji wa kata ya Luhanga Aloyce Joseph alisema wapo wanasiasa wanaoonekana kuingilia kati uwekezaji huo na kuwalaghai wananchi kuwa kilichofanyika ni unyang’anyi wa ardhi hali ambayo imeonekana kuwagawa wanakijiji katika makundi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali George Kagomba alisema uwekezaji wa Umoja huo utakinufaisha kijiji kwani kabla hata ya kuanza kwa shughuli husuika tayari umoja huo umeonesha nia kwa kuanza kuwasaidia wanakijiji kutatua changamoto mbalimbali.


Saturday, October 8, 2011

Mbunge Mbaroni


MBUNGE wa Mbarari Modestus Dickson Kilufi aliyekuwa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutishia kuua atafikishwa mahakamani kesho jumatatu(Oktoba 10) na kwa sasa yupo nje kwa dhamana.

Mbunge Kilufi alikamatwa juzi(Oktoba 7) saa 10 jioni akiwa ofisini kwake ambapo kwa mujibu wa maelezo yake askari waliofika kumkamata ofisini hapo walimweliza kuwa alitishia kumuua ofisa mtendaji wa kata ya Ruiwa Jordan Masweve.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alithibitisha kuachiwa kwa dhamana mbunge Kirufi alipozungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu.

Nyombi alisema mbunge huyo yupo nje kwa dhamana na atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu kusomewa shitaka la kutishia kuua kwa maneno.

Hata hivyo kamanda huyo hakutaja mbunge atafikishwa katika mahakama ipi bali alisema ofisi ya mwanasheria wa serikali mfawidhi mkoa wa Mbeya ndiyo inayotambua mahakama hiyo kwani hata kukamatwa kwake kulilenga kutekeleza agizo la ofisi hiyo.

“Baada ya askari wetu kumkamata jana,leo hii tumemfikisha katika ofisi ya mwanasheria wa serikali na wao ndiyo watamfikisha mahakamani.Lakini hivi sasa yupo nje kwa dhamana na shitaka linalomkabili ni kutishia kuua kwa maneno” alisema Nyombi

Kwa upande wa Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya umesema hauhusiki na mashitaka yanayomkabili mbunge huyo kwani ni masuala yake binafsi na si ya chama.

Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Verena Shumbusho alisema jana kuwa shitaka la kutishia kuua linalomkabili mbunge kirufi chama hakiwezi kulitolea tamko lolote.

“Kama chama hatuwezi kutoa tamko lolote juu ya kukamatwa kwake wala shitaka linalomkabili.Hilo ni suala lake binafsi na chama hatulitambui kabisa” alisema Shumbusho.

Sunday, October 2, 2011

MATOKEO IGUNGA

Kwa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo mtandao wa JF zinatanabaisha kuwa
Matokeo Igunga.(Jumla kuu ni CCM 26266. CHADEMA 22443)
 

 Na haya ni kata kwa kata...
Mboto CCM 730- CHADEMA 302
Nguvu moja CCM 694 CHADEMA 284
Nkinga CCM1479. CHADEMA 1085
Itumba CCM1079 CHADEMA 590
Nanga. CCM 897. CHADEMA 645
Igurubi CCM 925 CHADEMA 592
Mwisi CCM 926. CHADEMA 992
Mbutu. CCM 1186. CHADEMA 1426
Kinungu. CCM 505 CHADEMA 268
Ngulu CCM 622 CHADEMA 412
Igunga CCM 3181 CHADEMA 3358
Choma CCM 1227 CHADEMA 918
Kining. CCM 700 CHADEMA 451
Mwashiku. CCM 798 CHADEMA 484
Nsimbo CCM 738 CHADEMA 1016
Itunduru CCM 738 CHADEMA 784
Mwamashimba CCM 1224 CHADEMA 1421
Mbutu CCM 1335 CHADEMA 1427
Bukoko CCM 1136 Chadema 931
Nyandekwa CCM 691 Chadema 631
Ndembezi CCM 866 Chadema 806
Chabutwa CCM 545 Chadema 581
Ziba CCM 1053 Chadema 860
Igoweko CCM 1051 Chadema 880
Sungwizi CCM 1225 Chadema 718
Isakamaliwa CCM 525 Chadema 593