Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, October 4, 2018

ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGE LUGOLA MKOANI MBEYA

 Akipokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Ulrich Matei ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya,Albert Chalamila.
 Akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Magereza,katika Gereza la Luanda Mbeya.
 Akikagua ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Mbalizi
 Akizungumza na mkaguzi wa magari wa Jeshi la Polisi.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

                         Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                   Mkoa  wa  Mbeya,                                                                                  
Namba ya simu 2502572                                                                                               S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                   MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
              tanpol.mbeya@gmail.com
                                                       
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 03.10.2018.

ZIARA YA KIKAZI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MKOANI MBEYA.

Tarehe 03.10.2018 kuanzia majira ya saa 09:30 asubuhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa KANGI LUGOLA amefanya ziara ya kikazi Mkoani Mbeya ambapo alianza kwa kutembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa ALBERT CHALAMILA na kisha kuongea na waandishi wa habari kuhusu lengo la ziara yake.

Mhe. KANGI LUGOLA ameeleza kuwa lengo la ziara yake ni kukagua na kufanya ufuatiliaji wa maelekezo aliyoyatoa mnamo tarehe 04.07.2018 alipofika Mkoani Mbeya kukagua eneo ilipotokea ajali Mlima Iwambi na kusababisha vifo vya watu 20 na majeruhi 28.

Baada ya kukagua eneo la ajali, Mhe.Waziri alitoa maelekezo ya kufanya ukaguzi wa magari kabla na baada ya safari, kukagua na kufanya uhakiki wa leseni za madereva, kuwapima ulevi madereva pamoja na kudhibiti mwendo kasi.

Katika ziara yake Mhe. KANGI LUGOLA ametembelea na kukagua Gereza la Ruanda na kuongea na mahabusu na wafungwa waliomo gerezani humo pamoja na kujione shughuli mbalimbali zinazofanywa na wafungwa katika Gereza hilo.

Pia alitembelea eneo la Iwambi na kukagua zoezi la ukaguzi wa magari linalofanywa na maafisa wa Polisi [Vehicle Inspectors] sambamba na kujionea mkakati wa kuzuia ajali maeneo ya milima ambapo magari ya abiria na mizigo hupita tofauti katika maeneo hayo ili kuzuia ajali au kupunguza madhara makubwa yasitokee pindi ajali zinapotokea.



Aidha ziara ya Mhe.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi imekamilika kwa kutembelea na kukagua ujenzi unaoendelea wa kituo kipya cha Polisi Mbalizi, ujenzi unaofanywa kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Katika ukaguzi wake Mhe.KANGI LUGOLA amesisitiza wananchi kuendelea kuchangia ujenzi wa Kituo Kipya cha Polisi Mbalizi kilichopo Wilaya ya Mbeya Vijijini ili kikamilike kwa wakati. Aidha katika kuzuia uhalifu, Mhe Waziri amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi hasa katika utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu.

               Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Thursday, April 19, 2018

TEMBO WAMVAMIA KIKONGWE,WAMJERUHI HADI KIFO


WANYAMA Tembo watatu wamemvamia na kumjeruhi na kimsababishia kifo Kikongwe aliyefahamika kwa jina la Sixbertha Mtundu(88) mkazi wa kitongoji cha Mbuyuni mtaa wa Ihanga kata ya Rujewa wilayani Mbarali

Afisa Mtendaji wa Kata ya Rujewa wilayani Mbarali,John Mpangala amesema tukio limetokea juzi saa 11 za jioni maeneo yaliyopo jirani na Ikulu ndogo ya wilaya ya Mbarali.

Mpangala amesema kikongwe huyo amevamiwa na tembo hao wakati akitokea shambani kwake na inasadikika kutokana na umri wake mkubwa huenda hakuwaona wanyama hao mapema na pia alishindwa kukimbia baada ya kuvamiwa.

Hata hivyo Afisa mtendaji huyo amesema tukio hilo liligunduliwa na msamaria mwema mmoja aliyepita eneo hilo na kukuta kikongwe huyo akiwa amelala njiani huku amejeruhiwa vibaya kwa kukanyagwa na tembo na ndipo mkazi huyo alikwenda kwa mwenyekiti wa kitongoji na kumjulisha na ndipo wakaenda eneo husika ikiwa ni majira ya saa moja na nusu usiku lakini wakakuta amekufa.

Afisa mtendaji huyo amesema walichokifanya baada ya tukio hilo ni kuwapa taarifa wenyeviti wa vitongoji vya maeneo ya jirani ili waweze kuwapa tahadhali wananchi kuwa bado tembo hawajulikani walipo japo njia waliopikuwa wakielekea inakwenda eneo la Hifadhi ya Mpanga Kipengele hivyo huenda wapo au wamekwenda hifadhini.

Amesema eneo la tukio kwa miaka ya nyuma ilikuwa njia(Shoroba) ya wanyama lakini baada ya shughuli mbalimbali za kibinadamu hususani kilimo na makazi kukithiri wanyama hawakuendelea kupita tena.





Tuesday, April 17, 2018

ABIRIA WAKWAMA KWA MUDA WILAYANI CHUNYA


 CHINI-Mamia ya Abiria wakiwa wamelazimika kutoendelea na safari juzi baada ya gari za abiria na mizigo zinazofanya safari zake kati ya jijini Mbeya-Chunya hadi Tabora na Singida kukwama katika kata ya Matundasi wilayani Chunya kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.




DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisaidiwa kuvuka kwenye daraja la muda alipokuwa akikagua leo daraja la Mto Msimbazi linalounganisha Ulongoni B na Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ambalo ni moja ya madaraja yaliyobomoka kutokana athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha. Mjema alifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua katika wilaya hiyo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA KAMANDA WA MATUKIO BLOG 0715264202

 Mjema akimpa pole mmoja wa akina mama aliyevuka katika daraja la hilo  la muda linalohatarisha usalama wa wananchi wanaopita hapo.
 Mkuu wa Wilaya Mjema, akizungumza na wakazi wa Ulongoni baada ya kuwafuata upande wa pili kwa kutumia daraja hilo hatari.

 Mjema akiondoka baada ya kukagua daraja hilo la Ulongoni B.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema (kulia) akishauriana na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi wa Manisapaa ya wilaya hiyo, Msongela Palela alipofika kukagua daraja la Banguo Pugu Mnadani eneo ambalo mto umeacha kupita darajani na kumega eneo la barabara hali iliyosababisha kukata mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.
 Wakiangalia jinsi mto Msimbazi ulivyoacha mkondo wake wa kawaida na kumega ardhi
maeneo ya makazi ya watu pamoja na kuharibu barabara.
 Baadhi ya nyumba eneo la Bangua ambazo zimo hatarini kubomolewa na mafuriko.
 Nyumba iliyozungukwa na mto kila upande.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa na mtoto nyumba anayoishi na wazazi wake.
Mtoto huyo alisema kuwa hajaenda shule kutokana na eneo hilo kutokuwa na eneo la kuvuka ng'ambo ya pili iliko shule yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa mkondo wa maji ambao umezibwa baada ya baadhi ya wakazi wa Majohe, kuuziba kwa kujenga nyumba kwenye mkondo huo kitendo ambacho kimesababisha maji kuingia kwenye majumba ya watu.
 Mjema akiangalia baadhi yanyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo
la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
 Diwani wa Kata ya Majohe, Waziri Mweneviale akimuonesha Mjema baadhi ya nyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
 Mjema akikagua moja kati ya nyumba zilizojengwa kwenye mkondo wa maji.
 Msingi wa nyumba ukiendelea kujengwa kwenye mkondo wa maji licha ya uongozi wa
serikali ya Kata ya Majohe kuwakataza kujenga katika eneo hilo.
 Wananchi wa Gongo la Mboto wakiangalia jinsi Mto Msimbazi ulivyosababisha
maporomoko baada ya kufurika kufuatia mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha sasa.
 Daraja linalounganisaha Gongo la Mboto na Ulongoni A, limezungushiwa utepe ili watu wasipite baadaya kuathiriwa na mafuriko.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja
 la Ulongoni A.

 Nyumba iliyopo kando ya mto Msimbazi Ulongoni A, ikiezuliwa mabati  baada ya kuona imo hatarini kuathiriwa na mto huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja  la Ulongoni A.
Mjema akisafiri kwa baada ya kumaliza kugua athari za mvua katika daraja la Ulongoni A.
KWA HISANI YA KAMANDA WA MATUKIO BLOG 0715264202