Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, October 26, 2023

KenGold wataka kujiimarisha zaidi kileleni Championship



 

NA MWANDISHI WETU


VINARA wa NBC Championship League KenGold FC wamewasili salama mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wao wa mzunguko wa nane dhidi ya Biashara United uliopangwa kuchezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Jumamosi ya Oktoba 28,2023.

Vinara hao wamesema matarajio yao ni kuendeleza ushindi kwenye michezo yake ili kujiweka mahali salama zaidi hivyo wamejipanga kupata matokeo ya ushindi katika mchezo huo wa kesho.

Akizungumza kwa njia ya simu mara baada ya kuwasili Kagera mshambuliaji wa kikosi hicho, Emanuel Mpuka alisema licha ya kusafiri umbali mrefu wachezaji wote wapo na afya njema na morali kubwa kuelekea kwenye mchezo huo.

Aamesema matarajio ya matokeo bora yanatokana na maandalizi waliyoyafanya hata kabla ya kuanza kwa safari huku akisema mabadiliko ya hali ya hewa hayatarajiwi kuwa kikwazo kwao.

"Tunaamini kwenye maandalizi tuliyojiandaa, tumekuja kupambana kusaka alama tatu,hali ya hewa ya huku inautofauti mkubwa sana na Mbeya...kuna muda joto,kuna muda baridi na wakati mwingine mvua inanyesha kabisa. Lakini hiyo haituondoei kwenye nia yetu" Amesema Mpuka

Mshambuliaji huyo mpaka sasa amefunga magoli 3 na Assist 2 kwenye kikosi cha KenGold FC ambacho kinaongoza msimamo wa NBC Championship League kikiwa na alama 16.

CHUNYA YAENDELEA KUWABURUZA WAPINZANI SHIMISEMITA DODOMA

 

Timu ya wanawake ya kuvuta Kamba ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ikiongozwa na Kiongozi mwanamama mwenye misuli Bi Devotha Mwasaga ikiendeleza ubabe wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Jijini Dodoma

NA MWANDISHI WETU, DODOMA


Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bingwa mtetezi wa mchezo wa kuvuta Kamba  SHIMISEMITA msimu uliopita msimu huu bado inaendelea kuwabuluza wapinzani wake katika michezo ya watumishi inayoendela jijini Dodoma baada ya Timu ya wanawake kuvuta Kamba kuingia nusu fainali wakati Timu ya wanaume kuvuta kamba iko Robo Fainali

                          Chunya DC Vs Moshi DC (ME) mshindi CHUNYA DC

                         Chunya DC Vs Tunduma TC (KE) mshindi CHUNYA DC

Kwa matokeo hayo  Chunya Dc wanaume wametinga hatua ya robo fainali (Mtoano) ambapo watakutana uso kwa uso timu ya watumishi kutoka Arusha jiji  huku timu ya Chunya DC wanawake wao wametinga hatua ya nusu fainali ambapo watavaa na timu Kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam (DAR CC) ambayo ni kesho asubuhi.


Kuelekea Mchezo wa Nusu Fainali kepten wa timu ya wanawakeChunya DC Kuvuta kamba Bi Devotha Mwasaga amesema kilichobaki kutoka kwa wanachunya ni dua, Sara na Maombi ili kufanikisha azma ya kuleta ushindi Chunya na hatimaye kuiheshimisha wilaya ya Chunya kwani upande wa Maandalizi hakuna changamoto yoyote timu iko salama.


“Tunachokihitaji kutoka kwa wananchunya ni maombi kila mmoja kwa Imani yake ili timu iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa kwani upande wa maandalizi kila kitu kiko vizuri, wachezaji wana ari na morali wa kuhakikisha ubingwa unakuja Chunya hivyo tuiheshimishe Chunya yetu”.


Kwa upande wa timu wanaume kuvuta kamba kepteni wa Timu hiyo Ridhiwani Mshigati amesema bado timu iko Imara na iki tayari kwa michezo yote iliyo mbele yetu huku lengo ni lile lile kuchukua tena ubingwa katika mashindano hayo hasa kwa upande wa Mchezo wa Kuvuta Kamba.


“Kwenye mchezo wa kuvuta kamba tumeendelea na kutetea ubingwa wetu na ndo maana tumeshinda 2 bila kwa maana ya kwamba tuliocheza nao tumefunga awamu zote mbili, na kamba ina mbinu za kupata ushindi, sisi tumehatika kupata mtaalamu anatuongoza vizuri na kwasasa tuko kambini tunaendelea kupeana mbinu na kutunza nidhamu. kurudi mikono mitupu kwa Mwajiri ni aibu kubwa ambayo sisi hatutaki itokee kwetu kulingana na huduma tulizopewa na mwajili wetu.


Na tunashukuru Halmashauri jirani za Rungwe na Tunduma wanatusapo, ingawa Tunduma Tc walifungwa na timu ya wanawake kuvuta kamba tuliwaomba radhi na kuwambia kwa hili hatuna ujirani tukawatoa, Tunaomba  watu wa Chunya waendelee kutuombea ili kutetee ubingwa wetu na lengo ni siku ya kufungwa kwa Mashindano haya Halmashauri yetu ya Chunya Itajwe na Mgeni rasmi na Bendera yetu iweze kupepea mbela ya Halmashauri zaiidi ya Mia moja zilizoshiriki Mashindano hayo” amesema Mshigati.


Utofauti wa hatua yaani Timu ya wanaume kuwa hatua ya Robo Fainali (Mtoano) huku timu ya wanawake kuwa hatua ya Nusu Fainali umetokana na Idadi ya timu zilizoshiriki mchezo huo kwani Timu za wanawake zilikuwa chache kulinganisha na timu za wanaume hivyo kupelekea  kupelekea baadhi ya hatua za mashindano kuwa na mzunguko mfupi kulingana na timu za wanaume.


Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndiye Bingwa Mtetezi wa Mchezo wa Kuvuta Kamba Taifa kwa msimu wa mwaka 2022 na sasa timu zote ziko hatua nzuri kutetea ubingwa mwaka huu 2023, Maombi, bahati pamoja na kujituma vitaendelea kuhitajika ili timu zetu ziendelee kufanya vizuri