Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, December 29, 2017

DOGO JANJA KUPAGAWISHA IRINGA MKESHA WA MWAKA MPYA.

Sehemu ni moja tu Iringa pale #club_vip tutapindua mwaka kibazazi na wastaarabu wote huku hsti miliki ya burudani mikononi mwa @dogojanjatz #kiingilio10,000/-... tuuuuu.
Ni siku ya mkesha wa mwaka mpya trh 31december 2017 milango wazi kuanzia SAA 2usiku.Usimwache jirani atakulaumu huyooooo!!!!!



HAYA SASA ALBUM YA MWANAUME MASHINE HII HAPA

Unangoja nini msimu huu wa Sikukuu ? ... Jipatie Bidhaa za Kiburudani zenye Ubora wa Hali ya juu kutoka #BarazaniEntertainment•• Na kwa sasa tumeshakuletea BIDHAA NAMBA 1 ambayo ni FILAMU " QUEEN OF MAASAI " na BIDHAA NAMBA 2 ambayo ni ALBAMU YA MSAGASUMU " MWANAUME MASHINE " •• KUMBUKA: NAMBA YA KAMPUNI 350066 "Kwa Mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa Namba zifuatazo +255 715 947 144 / +255 653114 444 #BarazaniEntertainment #ujioumekufikua ?

Tuesday, December 19, 2017

MAHAFALI YA 16 CHUO KIKUU MZUMBE YALIVYOFANA

Afisa Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Standard Newepaper (TSN)  Kanda ya Nyanda za juu kusini,Dickson Ishengoma(kulia) na wenzake wakifurahi pamoja baada ya kuhitimu Shahada ya Umahiri katika uendeshaji uongozaji wa Mashirika katika Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe tawi la Mbeya yaliyofanyika jijini Mbeya.


UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya umesema bado una nia ya kukipanua zaidi chuo hicho ili kiweze kukidhi mahitaji ya wakazi wa Nyanda za juu kusini na pia nchi jirani za Zambia,Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Mwenyekiti wa Baraza la Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya, Prof Mathew Luhanga alibainisha hayo kwenye mahafali ya 16 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Mbeya.

Prof Luhanga alisema bado chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa miundombinu hususani kumbi za mihadhara,majengo ya madarasa,nyumba za watumishi na pia Hosteli.

Alisema jitihada zinazofanywa na chuo kwa kushirikiana na wadau ili kutatua changamoto hizo ndizo zitawezesha chuo kupata hadhi ya kuwatumikia wahitaji kwa kiwango kinachohitajika.

Aliipongeza Uongozi wa Serikali Kuu,Serikali ya mkoa wa Mbeya na Halmashauri ya jiji akisema umekuwa ukishirikiana kwa karibu na uongozi wa chuo katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo.

“Serikali imetusimamia kupata mkopo wa zaidi ya  bilioni moja lakini pia yenyewe katika mwaka huu wa fedha imetenga bajeti ya shilingi bilioni moja ili kutusaidia katika ujenzi wa jengo la utawala” alisema Prof Luhanga.

Kwa upande wake Makamu mkuu wa Chuo hicho Prof Lugano Kusiluka alisema Chuo pia kinatarajia kuongeza udahili wa wanafunzi sambamba na kuongeza programu zaidi ya 11 zinazotolewa hivi sasa katika tawi hilo.

Kwa mujibu wa Prof Kusiluka katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 734 walihitimu katika ngazi za Astashahada,stashahada na Shahada kati yao wanawake wakiongoza kwa asilimia 50.1 na wanaume asilimia 49.9.

Mmoja wa wahitimu,Afisa Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Standard Newepaper (TSN)  Kanda ya Nyanda za juu kusini,Dickson Ishengoma aliahidi kuitumia taaluma aliyoipata kwa weledi na kwa manufaa ya Taifa hususani wakati huu wa kuelekea uchumi wa viwanda.

Ishengoma aliyehitimu Shahada ya Umahiri katika Biashara na uendeshaji wa Makampuni aliwasihi wahitimu wenzake kutobweteka na badala yake kufikiri ni kwa jinsi gani wanaweza kuisaidia Serikali kufikia hatua ya uchumi wa viwanda.

WACHANGIA DAMU KAMA ZAWADI YA CHRISMASS








HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imeandaa Kampeni ya kukusanya Chupa zaidi ya 100 za Damu kwaajili ya kutoa Zawadi ya Krismasi kwa wagonjwa wenye uhitaji wa Damu wilayani hapa.

Kwa mujibu wa kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali,Emanuel Kishimbo zoezi la kukusanya damu lilianza Desemba 3 mwaka huu katika kata ya Ubaruku na tangu ianze inaendelea vizuri kwa watu mbalimbali kujitokeza kuchangia.

Kishimbo alisema pia Desemba 5 watumishi wa Sekta mbalimbali katika halmashauri ya wilaya walijitokeza kuchangia Damu katika zoezi lililofanyika Nje ya Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri kabla ya kuhamishia Nje ya Hospitali ya wilaya.

“Lengo letu ni kuchangia zawadi katika msimu huu wa skukuu.Watu wengi msimu huu wanaandaa zawadi mbalimbali kwa watu wanaowapenda na kuwathamini.Sisi tumeona tuwape thamani watu wanaohitaji kuongezewa damu kwa kuwapa zawadi ya damu zetu.Hawa ni waliopata ajali,akina mama wanaojifungua na pia wagonjwa wengine hususani watoto”

“Wito wangu kwa wananchi ni kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili kwa sababu sambamba na zoezi la uchangiaji damu watapata pia faida ya kupima afya zao na kuzielewa kama shinikizo la damu,homa ya ini na kaswende na kujua kundi la damu alilo nalo”alisema Kishimbo.

Kwa Upande wake kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Mbarali,Dk Azael Luvanda alisema alisema kwa mahitaji ya damu kwa mwezi wilayani hapa ni kati ya yuniti 10 hadi yuniti 15 na katika kampeni hiyo kwa kata ya Ubaruku pekee waliweza kukusanya yuniti 50.

Dk Luvanda alisema wagonjwa wanaoongoza kwa mahitaji ya damu ni akina mama wajawazito na watu wanaopata ajari huku pia akisema kwa muda mrefu wamekuwa wakitegemea kupata damu kutoka kwa makundi ya wanafunzi.

KHERI YA CHRISMASS NA MWAKA MPYAAAA


Uongozi wa Lyamba Lya Mfipa kwa kushirikiana na Barazani Entartainment unakutakia Kheri ya Chrismass na Mwaka Mpya.
Pia Tunakukumbusha Kuwa Unaweza Kununua Filamu Ya Queen Of Masai Kupitia Simu Yako ya Mkononi kwa Kuingia ktk Menyu ya Pesa ya Mpesa, Tigo Pesa ana Halopesa Kisha Unachagua KULIPIA BILI, Kisha NAMBA YA KAMPUNI, Ingiza 350066, kisha weka KUMBUKUMBU NAMBA, Ambayo ni 1,1111, kisha WEKA KIASI, Weka 3000, Weka NAMBA YAKO YA SIRI kisha OK, Wahudumu Wetu Watakupigia Simu na Kukuletea Filamu Yako Hadi Barazani Kwako.

Sunday, December 17, 2017

FEROOZ,DAZ BABA,SKWIZA KUIBUKIA MBARALI



TANGAZO TANGAZO TANGAZO



FILAMU YA QUEEN OF MASAI ILIVYOINGIA MBEYA KWA KISHINDO

Supervisor wa Kampuni ya Barazani Entertainment wilaya ya Rungwe,Joseph Wikula akihakiki DVD za Filamu ya Queen Of Masai baada ya kukabidhiwa mgawo wa wilaya yake tayari kuwasambazia wateja waliokwisha nunua kupitia simu zao.

Meneja wa Kampuni ya Barazani Entertainment mkoa wa Mbeya,Joachim Nyambo(kushoto) akikabidhi DVD za Filamu ya Queen Of Masai kwa Supervisor wa Kampuni hiyo wilaya ya Rungwe,Joseph Wikula tayari kuwakabidhi mawakala kwaajili ya kuwasambazia wateja waliokwisha nunu filamu hiyo kupitia simu zao.

 Supervisor wa Kampuni ya Barazani Entertainment kanda namba 1 jijini Mbeya,Venance Matinya akihakiki DVD za Filamu ya Queen Of Masai baada ya kukabidhiwa mgawo wa wilaya yake tayari kuwasambazia wateja waliokwisha nunua kupitia simu zao.




MAKALA ATIMIZA AHADI YA MABATI,SARUJI KATA ZA MWASANGA NA IDUDA

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akikabidhi msaada wa Mabati 154 kwa viongozi wa kata kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la zahanati inayojengwa kwa ushirikiano wa wananchi wa kata za Tembela na Mwansanga




 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akikabidhi mifuko 100 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha afya cha kata ya Iduda jijini Mbeya.

MKUU wa mkoa wa Mbeya,Amos Makalla amevitaka vijiji na kata mkoani hapa kuingia katika shindano la kuanzisha Ujenzi wa Zahanati na vituo vya Afya ili Serikali ya mkoa iweze kumalizia ujenzi huo.

Makalla alitangaza Shindano hilo,jana alipotimiza ahadi ya kuchangia Bati 154 kwaajili ya kumalizia ujenzi wa Zahanati inayojengwa kwa ushirikiano wa wakazi wa Kata za Tembela na Mwasanga na pia Mifuko 100 ya Saruji kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata ya Iduda jijini Mbeya.

Makalla alisema hilo ni shindano alilolianzisha lengo likiwa ni kutoa msukumo kwa vijiji na kata zote mkoani hapa kuitikia wito wa kutekeleza mpango wa kila kijiji kuwa na zahanati na kila kata kituo cha afya.

“Nijaribuni kwa kuanzisha ujenzi muone kama sintomalizia,nitapeleka kote mabati na saruji kwaajili ya kumalizia ujenzi kwa wananchi watakaoanzisha.Inawezekana kabisa wapo wadau wana utayari wa kutusaidia vifaa”

“Lakini sintotaka kusikia bati ninazotoa zimepotea au kuibwa,sintotaka kusikia saruji ninayotoa imeibiwa au imeganda.Nikitoa kitu kifanye kazi tumalize ujenzi wananchi waache kupata shida ya matibabu”alisisitiza Makalla.

Mkuu huyo wa mkoa alisema ni jambo lisilowezekana wadau kuendelea kutamka Sera ya hapa kazi tu wakati wananchi wanaumwa au wanapoteza muda mwingi kutembea wakifuata huduma za matibabu.

Alisema iwapo mpango wa ujenzi wa zahanati na vituo vya afya utaendelea kuachiwa Halmashauri itachukua miaka mingi kukamilisha kutokana na ufinyu wa bajeti.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mbeya,Paul Ntinika aliahidi kuanza kutekeleza Shindano la ujenzi wa zahanati na vituo vya afya wilayani kwake mara moja akisema hiyo ni fursa ya kipekee isiyopaswa kuipoteza.