Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, December 17, 2017

MAADHIMISHO SIKU YA MAADILI DUNIANI YAFANA MBEYA

 Mkuu wa wilaya ya Mbeya,Paul Ntinika akipanda Miti katika viunga vya Shule ya Sekondari Lyoto jijini Mbeya katika Kilele cha Maadhimishi ya Siku ya Maadili na Haki za binadamu duniani.


 Maafisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(Takukuru),Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma pekee na Ofisi ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) mkoani Mbeya wakishirikiana na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lyoto ya jijini Mbeya kupanda miti katika maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za binadamu.








VIONGOZI mkoani Mbeya wametakiwa kutambua kuwa Jukumu la kusimamia maadili pamoja na mapambano dhidi ya Rushwa si la Taasisi simamizi pekee bali ni jukumu la kila mmoja katika nafasi yake.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya,Paul Ntinika alitoa agizo hilo alipomwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla katika maadhimisho  ya Kilele cha siku ya Maadili na Haki za Binadamu ambayo kimkoa yalifanyika katika Shule ya Sekondari Lyoto jijini hapa yakitanguliwa na Upandaji wa miti katika viunga vya shule hiyo.

Ntinika alisema wapo viongozi ambao wamaekuwa wakijisahau katika kusimamia maadili na mapambano dhidi ya rushwa huku wakiendelea kuwa na dhana potofu kuwa kazi hiyo ni ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(Takukuru) na Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma pekee au Ofisi ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG).

Aalisema ni wakati sasa kwa nafasi aliyo nayo katika jamii kuwa na shauku ya kuwa mfano wa kuigwa kwa uadirifu wake na kwa viongozi ni muhimu kukumbuka kuwa maeneo wanayoongoza na kusimamia ni mali ya umma hivyo jamii inatarajia matokeo chanya na yenye maslahi kwake hivyo lazima kuweka maslahi ya umma mbele na kuepuka kujihusisha na vitendo vya rushwa na migongano ya maslahi hususani kwenye maamuzi.

“Tunaweza kuonesha kwa vitendo kuwa tunazingatia maadili kwa kufanya kazi kwa bidii,kutoa huduma bora kwa umma,kwa wakati bila ya upendeleo.Kutekeleza majukumu yetu kwa uadilifu kwa kuzingatia mipaka ya madaraka tuliyokabidhiwa kwa manufaa ya umma”

“Kila mmoja wetu anapaswa kusimamia vizuri fedha na mali za umma alizokabidhiwa ili kuzuia ubadhirifu usitokee.Tufanye kazi kwa uaminifu na tutumie muda wa kazi kutekeleza majukumu tuliyopewa na si kwa shughuli binafsi”alisema Ntinika.

Mkuu huyo wa wilaya aliiagiza kamati za maadili katika maeneo ya kazi kufanya kazi kwa wakati na kuandaa taarifa zisizo na upendeleo ili kuziwezesha mamlaka za nidhamu kuchukua hatua stahiki.

Aliishauri Takukuru kujenga tabia ya kuchukua taarifa hizo za kamati za maadili kadiri iwezekanavyo ili waweze kuendelea na uchunguzi kwa tuhuma mbalimbali ambazo zina makosa ya rushwa chini ya sheria ya ya Kuzuia na Kupambana namba 11 ya mwaka 2007.

Kwa upande wake Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mbeya,Emmanuel Kayabo aliwapongeza wakazi mkoani hapa akisema wamezidi kuwa na ushirikiano na taaasisi hiyo licha ya uwepo wa wachache ambao bado wanashindwa kuwasilisha taarifa za matukio ya rushwa au kutoa ushahidi.

No comments:

Post a Comment