Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, July 6, 2015

PADRE MWASHILINDI ATAJA SABABU ZA KULIACHA KANISA NA KUUFUATA UBUNGE MBOZI



 Padre wa kanisa la Angikana Jonathan Mwashilindi akizungumza na makada wa Chadema katika kata ya Nanyala wilayani Mbozi alipofika kuelezea nia yake ya kugombea Ubunge wa Mbozi Mashariki
 Padre wa kanisa la Angikana Jonathan Mwashilindi akikabidhi Bendera ya Chama kwa viongozi wa Chadema kata ya Nanyala kama njia ya kukijenga chama hicho.


                                    HABARI KAMILI
Padre wa kanisa la Angikana Jonathan Mwashilindi amesema amechukua uamuzi wa kugombea Ubunge katika jimbo la Mbozi Mashariki ili aweze kupata fursa ya kutumikia makundi mengi ya kijamii zaidi ya kanisani.

Mwashilindi ameyasema hayo katika maeneo na nyakati tofauti alipozungumza na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendele(Chadema) kwenye kata mbalimbali za wilayni Mbozi alizotembelea zikiwamo za Nanyala,Ipunga na Miyovizi.

Akizungumzia nia yake ya kugombea kwa makada wa chama hicho,Pade Mwashilindi amesema kwa miaka 13 aliyolitumikia kanisa la Anglikana amekuwa akihudumia jamii ya aina moja na sasa ameona ni wakati kwake kutanua wigo wa kuitumikia jamii kwa kuingia kwenye siasa badala ya kanisani.

Padre huyo mzaliwa wa kijiji cha Mpanda wilayani Mbozi,amesema wakazi wilayani humo bado wanakabiliwa na changamoto nyingi hali inayotokana na viongozi wa kuchaguliwa kutowajibika ipasavyo.

Moja ya changamoto alizozitaja kuwakabili wakazi wa Mbozi ni pamoja na kutonufaika na shughuli za kilimo ambazo kwa miaka mingi wamekuwa wakijishughulisha nazo na kuzitegemea kama chanzo kikubwa cha pato lao.

Amesema licha ya jamii ya wanambozi kujituma katika shughuli za kilimo,bado hawajanufaika na matunda ya jasho lao kwakuwa upatikanaji wa soko la uhakika la mazao bado ni tatizo kubwa.

No comments:

Post a Comment