Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, July 23, 2015

CHARLES MWAKIPESILE ALIPOCHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA CCM KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI

 Safari ya Charles ilianza kwa utofauti kidogo.Wakati wengine wakiziita safari zao za matumaini,yeye aliita ya uhakika na ya ukombozi kwa wanambeya.Ilianzia katika viwanja vya Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini Mbeya alipozungumza na wanahabari kabla ya kwenda kuchukua fomu.
 Mkutano huu wa Charles na wanahabari haukuzuia wakazi wengine kuhudhuria.Waliruhusiwa kufika na kushuhudia mahojiano.
 Ndugu jamaa na marafiki wa Charles pia walijitokeza kumsindikiza kwenye mkutano huu muhimu.Hawakuishia hapo pia waliweza kutembea kwa miguu mpaka eneo la sabasaba zilipo ofisi za CCM Mbeya mjini alikochukua fomu.
 Hawa ni wanafunzi wenzake Charles katika chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino tawi la Mbeya.Charles licha ya kuwa mwanahabari pia anasomea masuala ya sheria kwenye chuo hiki.Ndiyo sababu wanasheria wenzio wakaona ni muhimu kuja kumsindikiza mwenzao katika kuanza safari hii.


Wakati ukafika!Hapa Katibu wa CCM Mbeya mjini Robert Kerenge akimkabidhi kada wa chama hicho Charles Mwakipesile Fomu ya kuwaniua nafasi ya kugombea ubunge kupitia chama hicho.

 Mgombea hakosi wapambe!Charles nae alikuwa nao.Walimsindikiza mpaka ofisini kuhakikisha anachukua fomu.

 Ndugu zangu hiki ndicho kilichotuleta hapa.Hatimaye tumechukua na sasa tukajipange kwaajili ya kampeni ndani ya chama kuziwinda kura za maoni!Alitamka Charles kwa furaha akiwa ameambatana na mkewe,ndugu jamaa na mafrafiki.
 Hapo safari ya Charles ikaendelea kwa kurudi tena Mkapa kwaajili ya kujaza fomu na kisha kuirejesha.

NB:NDUGU MDAU KUMBUKA PIA WEWE AU NDUGU YAKO ANAYO NAFASI YA KUONEKANA KATIKA Lyamba Lya Mfipa.





No comments:

Post a Comment