Watu 14 wamekufa na wengine zaidi ya
40 kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kutoka mnadani katika
kijiji cha Mbuyuni Wilayani Chunya kupinduka katika eneo la Mlima Msangamwelu
barabara ya Mbalizi-Chunya.
Ajali hiyo imetokea jana Septemba 24
mwaka huu majira ya saa 12:00 jioni katika eneo la Mlima Msangamwelu ambapo mmoja
wa mashuhuda wa ajali hiyo, Eden Sanga amesema gali hilo aina ya fuso
lililokuwa limebeba abiria pamoja na mizigo lilishindwa kupanda mlima na
kupinduka kutokana na kufeli kwa breki.
Sanga amesema kulikuwa na magari
mawili yameongozana ambapo wote walikuwa wanatokea mnadani na kwamba fuso
walilokuwa wamepanda wao lilifanikiwa kupanda mlima huo bila matatizo lakini
gari la wenzao lilishindwa kupanda mlima huo na kupinduka.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Anacret Malindisa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo alisema watu 11 walifariki papo hapo mara baada ya ajali hiyo kutokea na wengine watatu walifariki jana asubuhi wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mbalizi.

Amesema
watu hao walikuwa wanasafiri katika lori aina ya fuso lenye namba za usajili T
532 AJF lililokuwa likitokea Mbuyuni Wilayani Chunya ambapo lilikuwa limebeba
mizigo na watu ambao walikuwa wakitoka mdani.
Amewataja watu waliokufa katika ajali hiyo ambao wametambulika kwa jina moja moja kuwa ni Exzavery, Kaloli, Lembo, Masai, Kashinje, Noa,mama Anna Ugalahenga, Mwakalasya, Meshack na Mwakilasa ambvao miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,
Hata hivyo Malindisa amesema kuwa watu wengine watatu waliofariki leo asubihi katika hospitali teuleya ifisi bado majina yao hayajatambuliwa.Aidha alisema uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo bado unaendelea na kwamba taarifa kamili itatolewa baadae.